Hadithi

Yakwamba mtu mmoja alikuja kwa Mtume rehema na amani zimfikie, akamsemesha katika baadhi ya mambo, akasema: Akitaka Mwenyezi Mungu na ukataka, akasema Mtume rehema na amani zimfikie: "Umenifanya mimi kuwa mshirika wa Mwenyezi Mungu? sema: Akitaka Mwenyezi Mungu pekee

Chanzo: HadeethEnc.com, Kiswahili v1.18.0

Upokezi wake ni mzuriImepokelewa na Nasai katika Sunan Alkubra na Ibn Majah na Ahmad

Matini ya Kiarabu

عَنِ ابْنِ عَبَّاسٍ رضي الله عنهما: أَنَّ رَجُلًا أَتَى النَّبِيَّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، فَكَلَّمَهُ فِي بَعْضِ الْأَمْرِ، فَقَالَ: مَا شَاءَ اللهُ وَشِئْتَ، فَقَالَ النَّبِيُّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «أَجَعَلْتَنِي لِلَّهِ عَدْلًا؟ قُلْ: مَا شَاءَ اللهُ وَحْدَهُ».

Tafsiri

Imepokelewa kutoka kwa Bin Abbas -Radhi za Allah ziwe juu yao yeye na baba yake-: Yakwamba mtu mmoja alikuja kwa Mtume rehema na amani zimfikie, akamsemesha katika baadhi ya mambo, akasema: Akitaka Mwenyezi Mungu na ukataka, akasema Mtume rehema na amani zimfikie: "Umenifanya mimi kuwa mshirika wa Mwenyezi Mungu? sema: Akitaka Mwenyezi Mungu pekee".

Ufafanuzi

Alikuja mtu mmoja kwa Mtume rehema na amani zimfikie akamsemesha kuhusu jambo lake binafsi, kisha akasema: "Akitaka Mwenyezi Mungu na ukataka wewe", Mtume rehema na amani zimfikie akaikemea kauli hii, na akamueleza kuwa kuunganisha matashi ya kiumbe na matashi ya Mwenyezi Mungu kwa kiunganishi "na" ni shirki ndogo, haifai kwa muislamu kuitamka, kisha akamuelekeza katika kauli ya sawa na ya haki: "Akitaka Mwenyezi Mungu peke yake", ampwekeshe Mwenyezi Mungu katika matashi, na wala asiunganishe matashi ya yeyote kwa aina yoyote ya kiunganishi.

Mafunzo

  • Katazo la kusema: Akitaka Mwenyezi Mungu na ukitaka, na mfano wake katika yale yanayounganisha matashi ya mja katika matashi ya Mwenyezi Mungu kwa "na"; kwani hii ni katika shirki ndogo.
  • Ulazima wa kukemea uovu.
  • Mtume rehema na amani zimfikie alilinda mipaka ya tauhidi, na akaziba njia za ushirikina.
  • Wakati wa kuondoa uovu ni vyema kumuelekeza anayefikishiwa ujumbe katika mbadala wa halali, kwa kumuiga Mtume rehema na amani zimfikie.
  • Kukusanya baina ya kauli yake rehema na amani zimfikie katika hadithi hii: "Akitaka Mwenyezi Mungu peke yake", na kauli yake katika hadithi nyingine: "Sema: Akitaka Mwenyezi Mungu kisha ukitaka wewe" Nikuwa kauli ya mtu: " Akitaka Mwenyezi Mungu kisha ukitaka wewe", hii inafaa, lakini kauli ya: "Akitaka Mwenyezi Mungu peke yake" ndio bora zaidi.
  • Inafaa kusema: "Akitaka Mwenyezi Mungu kisha ukitaka" lakini bora zaidi ni kusema: "Akitaka Mwenyezi Mungu pekee".
Ufafanuzi: العربية

جاءَ رجلٌ إلى النبيِّ صلى الله عليه وسلم فكَلَّمَه في أمرٍ له، ثم قال: "ما شاء الله وشئت"، فأنكر عليه النبيُّ صلى الله عليه وسلم هذا القول، وأخبره أنّ عَطْف مشيئة المخلوق على مشيئة الله بالواو شِركٌ أصغر، لا يجوز للمسلم أن يَتَلَفَّظَ به، ثم أَرْشَدَه إلى القول الحق: "ما شاء الله وحده"، فيُفْرِد الله في مشيئته، ولا يَعْطِف عليه مشيئة أحدٍ بأيِّ نوع من أنواع العَطْف.

  • النهي عن قول: ما شاء الله وشئت، وما أشبهه مما فيه عَطْف مشيئة العبد على مشيئة الله بالواو؛ لأنه شرك أصغر.
  • وجوب إنكار المنكر.
  • رسول الله صلى الله عليه وسلم قد حَمَى حِمَى التوحيد، وسدَّ طرق الشرك.
  • عند إنكار المنكر يحسن توجيه المدعو إلى بديل مباح، اقتداءً بالنبي صلى الله عليه وسلم.
  • الجمع بين قوله صلى الله عليه وسلم في هذا الحديث: «ما شاء الله وَحْدَه»، وقوله في الحديث الآخر: «قل: ما شاء الله ثم شئت» أن قول الشخص: «ما شاء الله ثم شئت» جائز، لكن قوله: «ما شاء الله وحده» أفضل.
  • يجوز أن تقول: «ما شاء الله ثم شئت» ولكن الأفضل قول: «ما شاء الله وحده».

Mada

Ripoti kosa

Zaidi