Chanzo: HadeethEnc.com, Kiswahili v1.18.0
SahihiImepokelewa na Al-Bukhaariy
Matini ya Kiarabu
عَنْ أَبِي مُوسَى الأَشْعَرِيِّ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ عَنِ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: «أَطْعِمُوا الجَائِعَ، وَعُودُوا المَرِيضَ، وَفُكُّوا العَانِيَ».
Tafsiri
Imepokewa kutoka kwa Abuu Mussa Al-Ash'ary -radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Mlisheni mwenye njaa, na mtembeleeni mgonjwa, na mwacheni huru mateka".
Ufafanuzi
Amebainisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa katika haki za Muislamu kwa ndugu yake Muislamu ni kumlisha mwenye njaa na kumtembelea mgonjwa, na kumuacha huru mateka.
Mafunzo
- Himizo la Waislamu kusaidizana.
- Himizo la kumlisha chakula mwenye njaa na uhitaji, huyu imeamrishwa kumlisha.
- Sheria ya kumtembelea mgonjwa; ili kumpa faraja, na kumuombea dua na kupata malipo, na mengineyo.
- Kufanya pupa kumwacha huru mateka aliyetekwa na makafiri, na hiyo ima kwa kulipa gharama inayohitajika ili kumuondoa mikononi mwao, au kwa kubadilisha nao na mateka wa kikafiri, yaani: Kwa njia ya kubadilishana.
Ufafanuzi: العربية
بيَّن النبي صلى الله عليه وسلم أن من حق المسلم على أخيه المسلم أن يطعم الجائع، ويزور المريض، ويفك الأسير.
- الحث على التعاون بين المسلمين.
- الحث على إطعام الجائع المحتاج إلى الطعام، فهذا مأمورٌ بإطعامه.
- مشروعية العيادة للمريض؛ جبرًا لخاطره، والدعاء له، وحصول الأجر، وغير ذلك.
- الحرص على فك الأسير إذا أسَره الكفار، وذلك إما بدفع مقابل لتخليصه منهم، أو بمقابلته بمأسور من الكفار، أي: على سبيل المبادلة.