Hadithi

Kafara ya nadhiri ndio kafara ya kiapo

Chanzo: HadeethEnc.com, Kiswahili v1.18.0

SahihiImepokelewa Imamu Muslim

Matini ya Kiarabu

عَنْ عُقْبَةَ بْنِ عَامِرٍ رَضيَ اللهُ عنه عَنْ رَسُولِ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: «كَفَّارَةُ النَّذْرِ كَفَّارَةُ اليَمِينِ».

Tafsiri

Imepokelewa kutoka kwa Uqba bin Aamir -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake amesema: "Kafara ya nadhiri ndio kafara ya kiapo".

Ufafanuzi

Amebainisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa kafara ya kiapo cha jumla kisipoambatanishwa na kile anachokitaka au kukitaja: Ni kama kafara ya kiapo.

Mafunzo

  • Nadhiri: Kisheria: Ni mtu anayelazimika kubeba sheria kujilazimisha yeye mwenyewe kwa hiari yake jambo fulani kwa ajili ya Mwenyezi Mungu Mtukufu.
  • Kafara ya kiapo: Ni kulisha masikini kumi au kuwavisha kama nguo, au kumuacha huru mtumwa kutoka katika utumwa, asipoweza basi ni kufunga siku tatu.
  • Hekima na sababu ya kuwekwa kafara ni Muislamu aiheshimu nadhiri, hivyo asiizoee, na isikae ulimini mwake.
  • Aina za nadhiri: 1- Nadhiri isiyoanishwa: Kama mtu kusema: "Nimetia nadhiri ikiwa nitapona" na akanyamaza akawa hakunuia nadhiri maalumu huyu atatakiwa kutoa kafara ya kiapo endapo atapona. 2- Nadhiri ya hamaki na ghadhabu: Nayo ni mtu kutundika nadhiri katika sharti, akiwa na lengo la kukataza jambo kutofanyika au kuwa msukumo wa jambo lifanyike, kama kusema: "Ikiwa nitakusemesha basi nifunge mwezi mzima", na hukumu yake: Apewe hiari kati kufanya alichojiwekea, au atoe kafara ya kiapo wakati atakapomsemesha. 3- Nadhiri ya halali: Mfano: "Natoa nadhiri kwa Mwenyezi Mungu kuwa nitavaa nguo yangu", na hukumu yake: Atapewa hiari kati ya kuvaa nguo au kutoa kafara ya kiapo. 4- Nadhiri ya machukizo: "Naweka nadhiri kwa Mwenyezi Mungu ya kumpa talaka mke wangu", na hukumu yake: Ni sunna kwake kutoa kafara ya kiapo na asifanye alichotia nadhiri, na akikifanya hatolazimika kutoa kafara. 5- Nadhiri ya maasi: Mfano "Naweka nadhiri kwa Mwenyezi Mungu ntakuja kuiba", na hukumu yake ni haramu kuitekeleza, na atatoa kafara ya kiapo, na akitekeleza atapata dhambi lakini hatolazimika kutoa kafara. 6- Nadhiri ya kumtii Mwenyezi Mungu: Mfano: "Naweka nadhiri kwa Mwenyezi Mungu ya kuswali rakaa kadhaa" anakusudia kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, akiitundika katika sharti kama kupona kwa mgonjwa basi ni wajibu kutekeleza endapo sharti litapatikana, na asipoiambatanisha na chochote basi itakuwa wajibu kuitekeleza moja kwa moja.
Ufafanuzi: العربية

بيَّن النبي صلى الله عليه وسلم أن كفارة النذر المطلق إذا لم يُحدَّد فيما يريد منه ولم يسمِّه: هي كفارة اليمين.

  • النذر: شرعًا: إلزام مكلَّف مختارٍ نفسَهُ شيئًا لله تعالى.
  • كفارة اليمين: إطعام عشرة مساكين أو توفير كسوة لهم من ثياب أو تحرير مملوك من الرق، فإن لم يستطع فصيام ثلاثة أيام.
  • الحكمة من الكفارة أن يحترم المسلم النذر فلا يعود فيه، ولا يكون على لسانه.
  • أنواع النذر: 1. النذر المطلق: كقوله: (لله عليَّ نذرٌ إن شُفيتُ) وَسَكَتَ ولم يَنْوِ نذرًا معيّنًا فعليه كفارة يمين عند حصول الشفاء، 2. نذر لجاجٍ وغَضَبٍ: وهو أن يعلِّق النذر بشرطٍ، يقصد المنع من فعل شيء أو الحمل على فعله كقوله: (إن كلَّمتك فعليَّ صيام شهر)، وحكمه: أن يخيَّر بين فعل ما التزم به، أو يكفر كفارة يمين عند تكليمه، 3. نذر مباحٍ: مثل: (لله عَلَيَّ أن ألبس ثوبي)، وحكمه: يخير بين لبس الثوب، أو كفارة يمين، 4. نذر مكروهٍ: مثل: (لله عَلَيَّ أن أطلق زوجتي)، وحكمه: تسنُّ له كفارة يمين ولا يفعل ما نذر، وإن فعله فلا كفارة عليه، 5. نذر معصيةٍ: مثل: (لله عليَّ أن أسرق) وحكمه: يحرم الوفاء به ويكفر كفارة يمين، وإن فعل أثِمَ ولا كفارة عليه، 6. نذر طاعةٍ: مثل: (لله عليَّ أن أصلي كذا) بقصد التقرب لله، فإن علَّقه بشرطٍ كشفاءِ مريض وجب الوفاء به إن حصل الشرط، وإن لم يُعَلِّقه وجب الوفاء مطلقًا.

Mada

Ripoti kosa

Zaidi