Hadithi

Imani ni zaidi ya vitengo sabini au zaidi ya sitini, bora yake ni kauli ya Laa ilaaha illa llaah, na ya chini yake ni kuondoa udhia barabarani

Chanzo: HadeethEnc.com, Kiswahili v1.18.0

SahihiWamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake

Matini ya Kiarabu

عن أبي هريرة رضي الله عنه قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم: «الْإِيمَانُ بِضْعٌ وَسَبْعُونَ -أَوْ بِضْعٌ وَسِتُّونَ- شُعْبَةً، فَأَفْضَلُهَا قَوْلُ لَا إِلَهَ إِلَّا اللهُ، وَأَدْنَاهَا إِمَاطَةُ الْأَذَى عَنِ الطَّرِيقِ، وَالْحَيَاءُ شُعْبَةٌ مِنَ الْإِيمَانِ».

Tafsiri

Imepolelewa Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: amesema: Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Imani ni zaidi ya vitengo sabini au zaidi ya sitini, bora yake ni kauli ya Laa ilaaha illa llaah, na ya chini yake ni kuondoa udhia barabarani, na haya ni sehemu katika imani".

Ufafanuzi

Anaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa imani ina sehemu moja pamoja na mambo mengi, yanakusanya matendo itikadi na kauli. Nakuwa jambo la juu zaidi katika mambo ya imani ni kauli ya: Laa ilaaha illa llaah", kwa kujua maana yake, na kufanyia kazi matakwa yake, yakuwa Mwenyezi Mungu ndiye Mola Mlezi Mmoja wa pekee mwenye kustahaki kuabudiwa peke yake pasina mwingine zaidi yake. Nakuwa tendo dogo kabisa katika matendo ya imani ni kila chenye kuwaudhi watu katika njia zao. Kisha akaeleza -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa haya ni katika mambo ya imani, nayo ni tabia inayomsukuma mtu kufanya mazuri na kuacha mabaya.

Mafunzo

  • Imani inadaraja baadhi yake ni bora kuliko zingine.
  • Imani ni kauli na matendo na itikadi.
  • Kumuonea haya Allah Mtukufu hupelekea: Kuwa asikuone pale alipokukataza, na asikukose pale alipokuamrisha.
  • Kutajwa idadi hakumaanishi kuishia hapo, bali inamaanisha wingi wa matendo ya imani, kwani waarabu wanaweza kutaja idadi ya kitu na wasimaanishe kukanusha idadi nyingine isiyokuwa hiyo.
Ufafanuzi: العربية

يُخبرُ النبيُّ صلى الله عليه وسلم أنَّ الإيمانَ شُعَبٌ وخِصَالٌ كثيرة، تشتمل على أعمالٍ واعتقاداتٍ وأقوالٍ. وأنَّ أعلى خِصال الإيمان وأفضلَها قول: «لا إله إلا الله»، عالمًا بمعناها، عاملًا بمقتضاها، مِن أنّ الله هو الإله الواحد الأحد المستحق للعبادة وحده دون ما سواه. وأن أقلَّ أعمال الإيمان هو تَنْحِيَةُ كلِّ ما يؤذي الناسَ في طرقاتِهم. ثم أخبر صلى الله عليه وسلم أنَّ الحياءَ مِن خِصال الإيمان، وهو خُلُقٌ يبعث على فعل الجميل وترك القبيح.

  • الإيمان مراتب بعضها أفضل من بعض.
  • الإيمان قول وعمل واعتقاد.
  • الحياء من الله تعالى يقتضي: ألّا يراكَ حيث نهاك، وألّا يَفْقِدَكَ حيث أمرك.
  • ذِكْرُ العدد لا يعني الاقتصار عليه، بل يدلُّ على كثرة أعمال الإيمان، فإن العرب قد تذكر للشيء عددًا ولا تريد نفي ما سواه.

Mada

Ripoti kosa

Zaidi