Hadithi

Mfano wa mtu mnafiki, ni kama Mbuzi mwenye kutangatanga baina ya makundi mawili ya Mbuzi, wakati mwingine huwa na kundi hili na wakati mwingine huwa na kundi lile

Chanzo: HadeethEnc.com, Kiswahili v1.18.0

SahihiImepokelewa Imamu Muslim

Matini ya Kiarabu

عَنِ ابْنِ عُمَرَ رضي الله عنهما عَنِ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، قَالَ: «مَثَلُ الْمُنَافِقِ، كَمَثَلِ الشَّاةِ الْعَائِرَةِ بَيْنَ الْغَنَمَيْنِ تَعِيرُ إِلَى هَذِهِ مَرَّةً وَإِلَى هَذِهِ مَرَّةً».

Tafsiri

Imepokelewa kutoka kwa Bin Omar -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na baba yake- kutoka kwa Mtume Rehema na amani ziwe juu yake-amesema: "Mfano wa mtu mnafiki, ni kama Mbuzi mwenye kutangatanga baina ya makundi mawili ya Mbuzi, wakati mwingine huwa na kundi hili na wakati mwingine huwa na kundi lile."

Ufafanuzi

Anaweka wazi Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- hali za wanafiki, na kuwa mnafiki ni kama Mbuzi mwenye kutangatanga na asiyejua afuate kundi gani la Mbuzi, wakati mwingine huenda kundi hili na wakati mwingine huenda na kundi lingine, Wanafiki hutangatanga baina ya imani na ukafiri, hivyo hawapo na waumini kwa wazi wazi wala kwa kujificha, wala hawapo na makafiri kwa wazi wala kwa kujificha, bali kwa muonekano wa nje wanaonekana wapo na waumini, na kwa ndani (kwa siri) wapo kwenye shaka na kutanga tanga, wakati mwingine, na wakati mwingine wanaelemea kwa hawa na wakati mwingine kwenye kundi hili.

Mafunzo

  • Miongoni mwa miongozo ya Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- ni kupiga mfano ili kufahamu haraka.
  • Kuweka wazi hali za wanafiki za kutangatanga kuwa na mashaka na kutokuwa na utulivu.
  • Kuchukua tahadhari kutokana na hali za wanafiki na kuhimizwa kuwa na imani nje na ndani.
Ufafanuzi: العربية

بَيَّن النبي صلى الله عليه وسلم حال المنافق وأنه كالشاة المُترددة لا تدري تتبع أي القطيعين من الغنم، تذهب إلى هذا القطيع تارةً وإلى الآخر تارةً أخرى، فهم متحيرون بين الإيمان والكفر، فلا هم مع المؤمنين ظاهرًا وباطنًا، ولاهم مع الكفار ظاهرًا وباطنًا، بل ظواهرهم مع المؤمنين، وبواطنهم في شك وتردد، فتارة يميل إلى هؤلاء، وتارة يميل إلى هؤلاء.

  • من هدي النبي صلى الله عليه وسلم ضرب المثل لتقريب المعاني.
  • بيان حال المنافقين من التردد والشك وعدم الاستقرار.
  • التحذير من حال المنافقين والحث على الصدق والعزم في الإيمان ظاهرًا وباطنًا.

Mada

Ripoti kosa

Zaidi