Hadithi

Kutakuwa mwisho wa umma wangu na watu, wakikuhadithieni mambo ambayo humkuwahi kuyasikia nyinyi wala baba zenu, ole wenu na ole wao

Chanzo: HadeethEnc.com, Kiswahili v1.18.0

SahihiImepokelewa Imamu Muslim

Matini ya Kiarabu

عَنْ ‌أَبِي هُرَيْرَةَ عَنْ رَسُولِ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ أَنَّهُ قَالَ: «سَيَكُونُ فِي آخِرِ أُمَّتِي أُنَاسٌ يُحَدِّثُونَكُمْ مَا لَمْ تَسْمَعُوا أَنْتُمْ وَلَا آبَاؤُكُمْ، فَإِيَّاكُمْ وَإِيَّاهُمْ».

Tafsiri

Kutoka kwa Abuu Huraira kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Kutakuwa mwisho wa umma wangu na watu, wakikuhadithieni mambo ambayo humkuwahi kuyasikia nyinyi wala baba zenu, ole wenu na ole wao".

Ufafanuzi

Ameeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa watatokea watu katika zama za mwisho katika umma wake wakizua uongo, na wakisema mambo ambayo hakuyasema yeyote kabla yao, wataeleza simulizi za uongo na za kutunga, akatuamrisha -Rehema na amani ziwe juu yake- tujiweke mbali nao na wala tusikae nao, na wala tusisikilize mazungumzo yao; ili hadithi hizo za kutunga tusiziweke ndani ya nafsi, tukashindwa kujiepusha nazo.

Mafunzo

  • Kuna alama miongoni mwa alama za utume, kiasi kwamba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- alieleza yatakayotokea katika umma wake, na yamekuwa kama alivyoeleza.
  • Kujitenga mbali na watu wanaomzulia uongo Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- na dini ya Uislamu, na kutosikiliza uongo wao.
  • Tahadhari na kukubali simulizi au kuzisambaza ila baada ya kuzihakiki kupata usahihi wake na kuthibiti kwake.
Ufafanuzi: العربية

أَخْبَرَ النبيُّ صلى الله عليه وسلم بأنه سيَظهر أُناسٌ في آخِر أُمتِه يَفْتَرون الكذب، ويقولون ما لم يقلْه أحدٌ من قبلهم، فيُخبِرون بالأحاديث المكذوبة والمُخْتَلَقة، فأمَرَنا عليه الصلاة والسلام أنْ نَبْتَعِدَ عنهم ولا نجالسهم، ولا نسمع أحاديثهم؛ لئلا يتقرر ذلك الحديث المختلق في النفوس، فنعجز عن التخلُّص منه.

  • فيه عَلَم من أعلام النبوة، حيث إن النبي صلى الله عليه وسلم أخبر بما سيقع في أمته، فكان كما أخبر.
  • الابتعاد عمّن يَكْذِبُ على رسول الله صلى الله عليه وسلم وعلى دين الإسلام، وعدم الاستماع لكذبهم.
  • التحذير من قبولِ الأحاديث أو نشرِها إلا بعد التأكُّد من صحتِها وثبوتِها.

Mada

Ripoti kosa

Zaidi