Hadithi

“Ninaapa kwa yule ambaye nafsi yangu iko mkononi mwake, hakika, hiyo ni sawa na theluthi moja ya Qur'ani

Chanzo: HadeethEnc.com, Kiswahili v1.18.0

SahihiImepokelewa na Al-Bukhaariy

Matini ya Kiarabu

عَنْ أَبِي سَعِيدٍ الخُدْرِيِّ رَضيَ اللهُ عنهُ: أَنَّ رَجُلًا سَمِعَ رَجُلًا يَقْرَأُ: {قُلْ هُوَ اللَّهُ أَحَدٌ} يُرَدِّدُهَا، فَلَمَّا أَصْبَحَ جَاءَ إِلَى رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فَذَكَرَ ذَلِكَ لَهُ، وَكَأَنَّ الرَّجُلَ يَتَقَالُّهَا، فَقَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «وَالَّذِي نَفْسِي بِيَدِهِ إِنَّهَا لَتَعْدِلُ ثُلُثَ القُرْآنِ».

Tafsiri

Kutoka kwa Abuu Saidi Al Khudri -radhi za Allah ziwe juu yake-: Ya kuwa mwanamume mmoja alimsikia mtu akisoma: "Sema: Yeye Mwenyezi Mungu ni wa pekee." Huku akiirudiarudia. Ilipofika asubuhi, alimjia Mtume wa Mwenyezi Mungu, rehema na amani ziwe juu yake, na akamueleza hilo. Na ni kana kwamba mwanamume huyo aliona jambo hilo ni jambo dogo. Basi Mtume wa Mwenyezi Mungu, rehema na amani ziwe juu yake akasema: “Ninaapa kwa yule ambaye nafsi yangu iko mkononi mwake, hakika, hiyo ni sawa na theluthi moja ya Qur'ani."

Ufafanuzi

Ameeleza Abuu Saidi Al-Khudri radhi za Allah ziwe juu yake kwamba mtu mmoja alimsikia bwana mmoja akisoma suratu: "Qul-huwallaahu Ahad" akiikariri kila usiku na wala hazidishi sura nyingine, palivopambazuka alikuja kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akamsimulia tukio hilo, ni kana kwamba muulizaji anaiona kuwa ndogo, akatoa kiapo rehema na amani ziwe juu yake kwa maana ya kuonyesha msisitizo, akasema: Namuapa yule ambaye nafsi yangu iko mkononi mwake hakika sura hiyo inalingana na theluthi ya Qur'ani.

Mafunzo

  • Fadhila za Suratul Ikhlaswi, na kuwa inalingana sawa na theluthi ya Qur'ani
  • Inafaa kusoma katika kisimamo cha usiku walau kwa aya chache na kuzirudia rudia, na kutokuziona ndogo.
  • Amesema Al-Maaziri: Inasemekana maana yake: Nikuwa Qur'ani iko katika sehemu tatu; visa na hukumu na sifa za Mwenyezi Mungu Mtukufu, na (Qul-huwallaahu Ahad) imejikita kwa ajili ya sifa za Mwenyezi Mungu, hivyo ni theluhti, na ni moja kati ya sehemu tatu, na imesemekana maana yake kuwa: Thawabu za kuisoma kwake hulipwa mara dufu kwa kiasi cha kusoma theluthi ya Qur'ani bila kuzidishwa.
Ufafanuzi: العربية

ذكر أبو سعيد الخدري رضي الله عنه أن رجلًا سمع آخر يقرأ سورة: {قُلْ هُوَ اللَّهُ أَحَدٌ} يرددها كل الليل لا يزيد عليها، فلما أصبح جاء إلى رسول الله صلى الله عليه وسلم فذكر ذلك له، وكأن السائل يرى أنها قليلة، فقال صلى الله عليه وسلم يمينًا على معنى التأكيد: والذي نفسي بيده إنها تساوي ثلث القرآن.

  • فضل سورة الإخلاص، وأنها تعدِل ثلث القرآن.
  • جواز القراءة في قيام الليل ولو بيسير الآيات وترديدها، وعدم تقليل ذلك.
  • قال المازري: قيل: معناه: أن القرآن على ثلاثة أنحاء؛ قصص وأحكام وصفات لله تعالى، و{قُلْ هُوَ اللَّهُ أَحَدٌ} متمحضة -يعني لصفات الله-، فهي ثلث، وجزء من ثلاثة أجزاء، وقيل: معناه: أن ثواب قراءتها يضاعف بقدر ثواب قراءة ثلث القرآن بغير تضعيف.

Mada

Ripoti kosa

Zaidi