Hadithi

Hakika imeteremshwa juu yangu aya ni aya ninayoipenda zaidi kuliko dunia nzima

Chanzo: HadeethEnc.com, Kiswahili v1.18.0

SahihiImepokelewa Imamu Muslim

Matini ya Kiarabu

عَنْ أَنَسِ بْنِ مَالِكٍ رَضيَ اللهُ عنهُ قَالَ: لَمَّا نَزَلَتْ: {إِنَّا فَتَحْنَا لَكَ فَتْحًا مُبِينًا لِيَغْفِرَ لَكَ اللهُ} إِلَى قَوْلِهِ {فَوْزًا عَظِيمًا} [الفتح: ١-٥] مَرْجِعَهُ مِنَ الْحُدَيْبِيَةِ، وَهُمْ يُخَالِطُهُمُ الْحُزْنُ وَالْكَآبَةُ، وَقَدْ نَحَرَ الْهَدْيَ بِالْحُدَيْبِيَةِ، فَقَالَ: «لَقَدْ أُنْزِلَتْ عَلَيَّ آيَةٌ هِيَ أَحَبُّ إِلَيَّ مِنَ الدُّنْيَا جَمِيعًا».

Tafsiri

Imepokelewa kutoka kwa Anas bin Maalik -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Ilipoteremka: "Hakika Sisi tumekufungulia wewe, ewe Mtume, ufunguzi ulio waziwazi, ili akusamehe Mwenyezi Mungu" mpaka katika kauli yake: "Ushindi mkubwa" [Fat-hi: 1-5] marejeo ya hili ni katika suluhu ya Hudaibia, na wao wakiwa wamejawa na huzuni na unyonge, na alichinja vichinjwa vyake hapo Hudaibia, akasema: "Hakika imeteremshwa juu yangu aya ni aya ninayoipenda zaidi kuliko dunia nzima".

Ufafanuzi

Ameeleza Anasi bin Maaliki radhi za Allah ziwe juu yake ya kwamba ilipoteremka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake kauli yake Mtukufu: "Hakika sisi tumekufungulia ewe Muhammadi ufunguzi wa wazi wazi (1) Ili akusameheme Mwenyezi Mungu yaliyotangulia katika madhambi yako na yajayo, na akutimizie neema zake, na akuongoe katika njia iliyonyooka (2) Na Mwenyezi Mungu akunusuru nusura yenye nguvu (3) Yeye ndiye aliyeteremsha utulivu katika nyoyo za Waumini ili wazidi imani juu ya imani yao. Na Mwenyezi Mungu ndiye mwenye majeshi ya mbingu na ardhi. Na Mwenyezi Mungu ni mwenye ujuzi, mwenye hekima (4) Ili awaingize Waumini wanaume na Waumini wanawake katika Bustani zipitazo mito kati yake, wadumu humo, na awafutie makosa yao. Na huko ndiko kufuzu kukubwa mbele ya Mwenyezi Mungu (5) [Al-Fat-hi: 1-5]. Hili lilikuwa Wakati wa kurejea kwake kutoka Hudaibia, na wakati Maswahaba wakiwa wamegubikwa na huzuni na unyonge, wakiwa wamezuiliwa kutekeleza Umra, kwa sababu ya yale waliyokubaliana katika mkataba, na dhana yao ilikuwa; yote hayo hayana masilahi na Waislamu, na walichinja vichinjwa vyao hapo Hudaibia, akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: Kwa hakika imeteremshwa juu yangu aya ni aya inayopendeka zaidi kwangu kuliko dunia nzima, kisha akaisoma.

Mafunzo

  • Kumebainishwa ukubwa wa yale aliyomneemesha Mwenyezi Mungu Mtukufu Mtume wake Muhammadi rehema na amani ziwe juu yake katika ushindi mkubwa katika suluhu ya Hudaibia; pale aliposema kumwambia: "Hakika sisi tumekufungulia ufunguzi wa wazi wazi". mpaka mwisho wa aya mbili.
  • Kumebainishwa yale aliyowaneemesha Mwenyezi Mungu Mtukufu Maswahaba radhi za Allah ziwe juu yao, walipotii amri yake na wakanyenyekea, kiasi ambacho aliteremsha kwao kauli yake Mtukufu: "Ili awaingize waumini wa kiume na waumini wa kike Pepo zinazopita chini yake mito" mpaka mwisho wa aya.
  • Kumebainishwa fadhila za Mwenyezi Mungu juu ya Nabii wake, na kwa waumini kwa kuwaahidi ufunguzi na ushindi.
  • Amesema Assa'di katika kuitafsiri kwake aya hii: "Hakika sisi tumekufungulia ewe Muhammadi ufunguzi wa wazi wazi" [Al-Fatha], Ushindi huu uliotajwa hapa ni Mkataba wa amani wa Hudaibia, pale washirikina walipomzuilia Mtume wa Mwenyezi Mungu – rehema na amani ziwe juu yake – alipokuja kwa ajili ya kufanya Umra, katika kisa kirefu, ambacho mwisho wake ulikuwa kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, - alifanya nao suluhu juu ya kumaliza vita kati yake na wao kwa muda wa miaka kumi, na kwamba atafanya Umra katika mwaka uliofuata, na kwamba anayetaka kuingia katika mkataba wa kusaidiana na Makuraishi, ana ruhusa ya kufanya hivyo, na anayetaka kuingia katika mkataba wa kusaidiana na Mtume wa Mwenyezi Mungu – rehema na amani ziwe juu yake, basi anaweza kufanya hivyo. Na sababu ya hilo kwamba pindi watu walipopata amani kutokana na wao kwa wao, eneo la kulingania kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu likapanuka, na akawa kila Muumini katika sehemu yoyote iliyopo katika nchi hizo anaweza kufanya hivyo, na likamwezesha mwenye uchu wa kuujua ukweli wa Uislamu kuujua. Kwa hivyo watu wakaingia katika dini ya Mwenyezi Mungu kwa makundi wakati wa kipindi hicho. Ndiyo maana Mwenyezi Mungu akauita (mkataba huo) ushindi, na akauelezea kwamba ni ushindi ulio wazi. Kwa sababu makusudio ya kuziteka nchi za washirikina ni kuimarisha dini ya Mwenyezi Mungu na kuwapa ushindi Waislamu, na hili lilitokea kwa ushindi huo.
Ufafanuzi: العربية

أخبر أنس بن مالك رضي الله عنه أنه لمّا نزل على رسول الله صلى الله عليه وسلم قوله تعالى: {إِنَّا فَتَحْنَا لَكَ فَتْحًا مُبِينًا (١) لِيَغْفِرَ لَكَ اللَّهُ مَا تَقَدَّمَ مِنْ ذَنْبِكَ وَمَا تَأَخَّرَ وَيُتِمَّ نِعْمَتَهُ عَلَيْكَ وَيَهْدِيَكَ صِرَاطًا مُسْتَقِيمًا (٢) وَيَنْصُرَكَ اللَّهُ نَصْرًا عَزِيزًا (٣) هُوَ الَّذِي أَنْزَلَ السَّكِينَةَ فِي قُلُوبِ الْمُؤْمِنِينَ لِيَزْدَادُوا إِيمَانًا مَعَ إِيمَانِهِمْ وَلِلَّهِ جُنُودُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَكَانَ اللَّهُ عَلِيمًا حَكِيمًا (٤) لِيُدْخِلَ الْمُؤْمِنِينَ وَالْمُؤْمِنَاتِ جَنَّاتٍ تَجْرِي مِنْ تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ خَالِدِينَ فِيهَا وَيُكَفِّرَ عَنْهُمْ سَيِّئَاتِهِمْ وَكَانَ ذَلِكَ عِنْدَ اللَّهِ فَوْزًا عَظِيمًا} [الفتح: ١-٥]، وقت رجوعه من الحديبية، والصحابة يخالطهم الحزن والكآبة، وقد حِيل بينهم وبين أداء العمرة، بسبب ما وقع عليه الصلح وظنهم أنه ليس في صالح المسلمين، وقد ذبحوا الهدي بالحديبية، فقال صلى الله عليه وسلم: لقد أنزلت علي آية هي أحب إلي من الدنيا جميعًا ثم قرأها.

  • بيان عظم ما أنعم الله سبحانه وتعالى على نبيه محمد صلى الله عليه وسلم من الفتح العظيم في صلح الحديبية؛ حيث قال له: {إِنَّا فَتَحْنَا لَكَ فَتْحًا مُبِينًا} الآيتين.
  • بيان ما مَنَّ الله تعالى على الصحابة رضي الله عنهم لمّا خضعوا لأمره وانقادوا، حيث أنزل لهم قوله تعالى: {لِيُدْخِلَ الْمُؤْمِنِينَ وَالْمُؤْمِنَاتِ جَنَّاتٍ تَجْرِي مِنْ تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ} الآية.
  • بيان فضل الله على نبيه، وعلى المؤمنين بأنْ وعدَهم الفتح والنصر.
  • قال السعدي في تفسيره على هذا الآية: {إِنَّا فَتَحْنَا لَكَ فَتْحًا مُبِينًا} [الفتح ١]، هذا الفتح المذكور هو صلح الحديبية، حين صد المشركون رسول الله صلى الله عليه وسلم لما جاء معتمرًا في قصة طويلة، صار آخر أمرها أن صالحهم رسول الله صلى الله عليه وسلم على وضع الحرب بينه وبينهم عشر سنين، وعلى أن يعتمر من العام المقبل، وعلى أن من أراد أن يدخل في عهد قريش وحلفهم دخل، ومن أحب أن يدخل في عهد رسول الله صلى الله عليه وسلم وعقده فعل. وبسبب ذلك لما أمن الناس بعضهم بعضًا، اتسعت دائرة الدعوة لدين الله عز وجل، وصار كل مؤمن بأي محل كان من تلك الأقطار، يتمكن من ذلك، وأمكن الحريص على الوقوف على حقيقة الإسلام، فدخل الناس في تلك المدة في دين الله أفواجًا، فلذلك سماه الله فتحًا، ووصفه بأنه فتح مبين أي: ظاهر جلي، وذلك لأن المقصود في فتح بلدان المشركين إعزاز دين الله، وانتصار المسلمين، وهذا حصل بذلك الفتح.

Mada

Ripoti kosa

Zaidi