Hadithi

Hakika majina yenu yanayopendeza zaidi kwa Mwenyezi Mungu ni Abdullah na Abdul-Rahman

Chanzo: HadeethEnc.com, Kiswahili v1.18.0

SahihiImepokelewa Imamu Muslim

Matini ya Kiarabu

عَنِ ابْنِ عُمَرَ رَضيَ اللهُ عنهما قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «إِنَّ أَحَبَّ أَسْمَائِكُمْ إِلَى اللهِ عَبْدُ اللهِ وَعَبْدُ الرَّحْمَنِ».

Tafsiri

kutoka kwa bin Omari radhi za Allah ziwe juu yao yeye na baba yake, amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu rehema na amani ziwe juu yake: "Hakika majina yenu yanayopendeza zaidi kwa Mwenyezi Mungu ni Abdullah na Abdul-Rahman".

Ufafanuzi

Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake ya kwamba majina yanayopendeza zaidi kwa Mwenyezi Mungu ni kumuita mtoto wa kiume: Abdullah, au Abdul-Rahman (Mja wa Allah au Mja wa Rahman).

Mafunzo

  • Amesema Al-Qurtubi: Yanaunganishwa na majina haya mawili yote yanayokuwa mfano wake kama Abdul-Rahiim, na Abdul-Maliki na Abdul-Swamad, na yamekuwa pendwa kwa Mwenyezi Mungu, kwa sababu yanaambatana na wasifu wa wajibu kwa Mwenyezi Mungu na wasifu kwa mwanadamu na ni wajibu kwake ambao ni utumwa, kisha mja akaambatanishwa kwa Mola Mlezi kuambatanishwa halisi, yakasadikisha majina haya, na yakapata utukufu kwa kuunganishwa huku, na yakapata fadhila hii, na wamesema wengineo: Hekima ya kufupisha kwa majina mawili ni kuwa haikuwahi kutokea kuambatanishwa ndani ya Qur'ani utumwa na Mwenyezi Mungu isipokuwa majina haya mawili, amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Na kwamba pindi aliposimama mja wa Mwenyezi Mungu akimuomba" na akasema katika aya nyingine: "Na waja wa Al-Rahman (Mwingi wa rehema) na inaungwa mkono na kauli yake Mtukufu: "Sema muombeni Allah au muombeni Al-Rahmaan".
Ufafanuzi: العربية

أخبر النبي صلى الله عليه وسلم أن أحب الأسماء إلى الله هي تسمية الذَّكَر: عبدالله، أو: عبدالرحمن.

  • قال القرطبي: يلتحق بهذين الاسمين ما كان مثلهما كعبد الرحيم وعبد الملك وعبد الصمد، وإنما كانت أحب إلى الله، لأنها تضمنت ما هو وصف واجب لله وما هو وصف للإنسان وواجب له وهو العبودية، ثم أضيف العبد إلى الرب إضافة حقيقية فصدَّقت أفراد هذه الأسماء وشرفت بهذا التركيب فحصلت لها هذه الفضيلة، وقال غيره: الحكمة في الاقتصار على الاسمين أنه لم يقع في القرآن إضافة عبد إلى اسم من أسماء الله تعالى غيرهما، قال الله تعالى: {وَأَنَّهُ ‌لَمَّا ‌قَامَ عَبْدُ اللَّهِ يَدْعُوهُ} وقال في آية أخرى: {وَعِبَادُ ‌الرَّحْمَنِ} ويؤيده قوله تعالى: { ‌قُلِ ‌ادْعُوا ‌اللَّهَ أَوِ ادْعُوا الرَّحْمَنَ}.

Mada

Ripoti kosa

Zaidi