Chanzo: HadeethEnc.com, Kiswahili v1.18.0
Matini ya Kiarabu
عَنْ جَابِرِ بْنِ عَبْدِ اللَّهِ رَضيَ اللهُ عنهُما قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «مَا أَسْكَرَ كَثِيرُهُ فَقَلِيلُهُ حَرَامٌ».
Tafsiri
Kutoka kwa Jaabir bin Abdillah radhi za Allah ziwe juu yake yeye na baba yake, amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake: "Kinacholewesha kikiwa kingi, basi hata kidogo ni haramu".
Ufafanuzi
Amebainisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake yakuwa kila kinywaji au chakula kinachoondosha akili wakati wa kukitumia kingi chake, basi kukitumia kidogo chake ni haramu, hata kisipoondosha akili.
Mafunzo
- Sheria imehifadhi akili za watu.
- Kufaa kuzingatia mlango wa kuzuia sababu zinazopelekea katika maovu, na hiyo ni kwa kufunga kila njia inayopelekea katika machafu hayo.
- Kumeharamishwa kichache katika kilevi; kwa sababu ndio njia ya kulewa.
- Kisipolewesha si kidogo wala kingi, basi hicho si haramu.
Ufafanuzi: العربية
بيَّن النبي صلى الله عليه وسلم أن أي مشروب أو مأكول يُذهِب العقل عند تناول الكثير منه، فتناول القليل منه مُحرَّم حتى لو لم يُذهب العقل.
- حِفَاظ الشريعة على عقول الناس.
- صحة اعتبار سَدّ الذرائع، وذلك بغَلْق كل ما يؤدّي إلى تلك الخبائث.
- تحريم القليل من المسكر؛ لأنه وسيلة للسُّكْر.
- إذا لم يُسكر لا القليل ولا الكثير، فإنه ليس بحرام.