Chanzo: HadeethEnc.com, Kiswahili v1.18.0
Matini ya Kiarabu
عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «إِنَّمَا بُعِثْتُ لِأُتَمِّمَ مَكَارِمَ الْأَخْلَاقِ».
Tafsiri
Kutoka kwa Abuu Huraira radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Amesema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Kwa hakika nimetumwa ili kutimiliza tabia njema"
Ufafanuzi
Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kwamba, hakika Mwenyezi Mungu Aliyetakasika na kutukuka alimtuma yeye ili akamilishe mambo bora na tabia zilizo njema; kiasi kwamba alitumwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake ili atimize yale waliyokuwa nayo Mitume, na alikuja kukamilisha tabia njema za waarabu, kwani walikuwa wakipenda kutenda kheri na wakichukia shari, walikuwa ni watu wenye utu na ukarimu na utukufu; akatumwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake ili kukamilishe mapungufu yaliyoko katika tabia zao, kama kujifaharisha kwao kwa nasaba, na kujikweza na kumdharau fakiri na nyinginezo.
Mafunzo
- Himizo la kuwa na tabia njema, na katazo la kinyume chake.
- Kumebainishwa umuhimu wa tabia njema katika sheria ya Uislamu na kwamba ni katika vipaumbele vyake.
- Watu wa zama za ujinga walikuwa na mabaki ya tabia njema, ikiwemo ukarimu na ushujaa na mengineyo, Uislamu ukaja kuyakamilisha.
Ufafanuzi: العربية
أخبر النبي صلى الله عليه وسلم أنه إنما أرسله الله عز وجل ليكمل فضائل ومحاسن الأخلاق؛ حيث بُعث النبي صلى الله عليه وسلم تتمّة لما قبله من الرُّسل، ومكمّلًا لأخلاق العرب الحسنة، فكانوا يحبون الخير ويَمْقتون الشر، أهل مروءة وكرم وشهامة؛ فبُعث النبي صلى الله عليه وسلم لإكمال النقائص التي في أخلاقهم، كتفاخرهم بالأنساب، والتكبر واحتقار الفقير وغير ذلك.
- الحث على مكارم الأخلاق، والنهي عن ضدها.
- بيان أهمية الأخلاق الحسنة في شريعة الإسلام وأنها من أولوياته.
- أهل الجاهلية كان عندهم بقايا من الأخلاق الحسنة، ومنها الكرم والشجاعة وغير ذلك فجاء الإسلام ليكملها.