Chanzo: HadeethEnc.com, Kiswahili v1.18.0
Matini ya Kiarabu
عَن أَبي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه عَنِ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: «لاَ يُشِيرُ أَحَدُكُمْ عَلَى أَخِيهِ بِالسِّلاَحِ، فَإِنَّهُ لاَ يَدْرِي، لَعَلَّ الشَّيْطَانَ يَنْزِعُ فِي يَدِهِ، فَيَقَعُ فِي حُفْرَةٍ مِنَ النَّارِ».
Tafsiri
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake amesema: "Asiashirie mmoja wenu silaha kwa ndugu yake, kwani hajui, huenda Shetani akaipokonya kutoka mkononi mwake, akatumbukia katika shimo la moto".
Ufafanuzi
Ametahadharisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake muislamu kuashiria juu ya ndugu yake muislamu kwa silaha, kwa aina yoyote ile miongoni mwa aina za silaha, kwa sababu yeye hajui huenda Shetani akamsukuma kuitikisa silaha mkononi mwake, akamuuwa ndugu yake au akamuudhi, akatumbukia katika maasi yanayoweza kumpelekea kuingia katika shimo la moto.
Mafunzo
- Kumebainishwa uharamu wa damu muislamu.
- Ulazima wa kumheshimu muislamu na tahadhari ya kumfikishia shari kwake kwa kitendo au kauli, ikiwemo kumuashiria kwa chuma au silaha, hata kama ni kwa mzaha; kwa sababu Shetani anaweza kuutelezesha mkono wake na akampendezeshea kumpiga ndugu yake, au akaipokonya silaha kutoka mkononi mwake ikatua pasina maamuzi yake ikamdhuru ndugu yake.
- Kuziba njia zinazopelekea katika jambo kwa kukataza yanayopelekea katika haramu.
- Pupa ya kuhakikisha usalama wa jamii na kuhifadhi mahusiano baina ya watu, na kutowatisha na kuwaogopesha hata kama ni kwa ishara na kutishia.
Ufafanuzi: العربية
حذر النبي صلى الله عليه وسلم أن يشير المسلم على أخيه المسلم بأي نوع من أنواع السلاح، فإنه لا يعلم لعل الشيطان يحمله على تحريك السلاح في يده، فيقتل أخاه أو يؤذيه، فيقع في المعصية التي تفضي به إلى أن يقع في حفرة من النار.
- بيان حرمة دم المسلم.
- وجوب احترام المسلم والحذر من إيصال الشر إليه بالفعل أو القول، ومن ذلك الإشارة بالحديدة أو بالسلاح، ولو مازحًا؛ لأن الشيطان قد ينزغ بيده ويزين له ضرب أخيه، أو ينزع السلاح من يده فيقع من غير اختياره فيضر أخاه.
- سد الذرائع بالنهي عما يفضي إلى المحظور.
- الحرص على سلامة المجتمع وحفظ العلاقات بين الناس، وعدم تخويفهم وترويعهم ولو بالإشارة والتهديد.