Chanzo: HadeethEnc.com, Kiswahili v1.18.0
Matini ya Kiarabu
عَنْ أَنَسِ بْنِ مَالِكٍ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ قَالَ: مَا خَطَبَنَا نَبِيُّ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ إِلَّا قَالَ: «لَا إِيمَانَ لِمَنْ لَا أَمَانَةَ لَهُ، وَلَا دِينَ لِمَنْ لَا عَهْدَ لَهُ».
Tafsiri
Kutoka kwa Anasi bin Maliki radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Hakuwahi kutuhutubia sisi Mtume rehema na amani ziwe juu yake isipokuwa alisema: "Hana imani asiyekuwa na uaminifu, na hana dini asiyekuwa na ahadi (za kweli)".
Ufafanuzi
Anaeleza Anasi bin Maliki radhi za Allah ziwe juu yake kuwa ni mara chache sana akihutubia Mtume rehema na amani ziwe juu yake au atoe mawaidha isipokuwa alikuwa akitaja mambo mawili: La kwanza: Hana imani mtu ambaye ndani ya nafsi yake kuna hiyana na mtu katika mali yake au nafsi yake au familia yake. La pili: Hana dini kamili mwenye kufanya hiyana katika ahadi na mikataba na kuivunja.
Mafunzo
- Himizo la kutekeleza amana na kutimiza ahadi, kwani kuivunja hupunguza imani.
- Tahadhari ya kutofanya hiyana na kuvunja ahadi, na kwamba hilo ni katika madhambi makubwa.
- Hadithi hii inakusanya kutunza amana na ahadi zilizo kati ya Mwenyezi Mungu na mja wake, na zile zilizo kati ya viumbe wao kwa wao.
Ufafanuzi: العربية
يُخبر أنس بن مالك رضي الله عنه أنه قَلَّ أن يخطب النبي صلى الله عليه وسلم أو يَعِظ إلا ذَكَر أمرين: الأول: لا إيمان كامل لمن كانت في نفسه خيانة لأحد في ماله أو نفسه أو أهله. الثاني: لا دين كامل لمن يَخون العهود والمواثيق وينقضُها.
- الحث على أداء الأمانة والإيفاء بالعهد، فإن نقضهم يُنقِص الإيمان.
- التحذير من خيانة الأمانة ونقض العهد، وأن ذلك من كبائر الذنوب.
- يشمل الحديث المحافظة على الأمانة والعهد الذي بين الله وبين عبده، والذي بين الخلق بعضهم البعض.