Hadithi

Hakika Mwenyezi Mungu Mtukufu amefaradhisha faradhi basi msizipoteze, na akaweka mipaka basi msiivuke, na akaharamisha vitu basi msivivamie, na akayanyamazia mambo kwa kukuhurumieni si kwa kusahau basi msiyatafute

Chanzo: HadeethEnc.com, Kiswahili v1.18.0

Amesema Imamu Nawawi: Hadithi hii ni hasanImepokelewa na Addar- Alqutni katika Sunanu yake na wengineo

Matini ya Kiarabu

عَنْ أَبِي ثَعْلَبَةَ الخُشَنِيِّ جُرْثُومِ بن نَاشِرٍ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ عَنْ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَال: «إِنَّ اللَّهَ فَرَضَ فَرَائِضَ فَلَا تُضَيِّعُوهَا، وَحَدَّ حُدُودًا فَلَا تَعْتَدُوهَا، وَحَرَّمَ أَشْيَاءَ فَلَا تَنْتَهِكُوهَا، وَسَكَتَ عَنْ أَشْيَاءَ رَحْمَةً لَكُمْ غَيْرَ نِسْيَانٍ فَلَا تَبْحَثُوا عَنْهَا».

Tafsiri

Kutoka kwa Abuu Tha'laba Al-Khushani Jurthuum bin Naashiri radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake kutoka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake amesema: "Hakika Mwenyezi Mungu Mtukufu amefaradhisha faradhi basi msizipoteze, na akaweka mipaka basi msiivuke, na akaharamisha vitu basi msivivamie, na akayanyamazia mambo kwa kukuhurumieni si kwa kusahau basi msiyatafute".

Ufafanuzi

Anaeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake ya kwamba Mwenyezi Mungu amewajibisha mambo na akafaradhisha faradhi basi shikamaneni nazo na wala msifanye uzembe katika hayo kwa kuyaacha au kuzembea ndani yake, na akakuwekeeni vizuizi na makemeo yaliyokadiriwa yanayokuzuieni na kukukemeeni katika yale asiyoyaridhia, msizidishe zaidi ya yale yaliyoamrishwa na sheria, na akaharamisha maharamisho kadhaa msiyachukue na wala msiyakaribie, na yasiyokuwa hayo kayaacha na akayanyamazia kwa kuwahurumia waja wake, hivyo yanabakia katika asili ya uhalali wake basi msiyatafute.

Mafunzo

  • Hadithi ni ushahidi kuwa Mwenyezi Mungu ndiye mleta sheria, hivyo amri iko mkononi mwake Yeye Mtukufu.
  • Hadithi imekusanya kanuni za sheria kwa kutoa hukumu na kuhalalisha, hivyo: Hukumu ya kisheria ima iwe imewachwa bila kusemwa au iwe imeelezwa wazi kwa uwajibu au sunna, na ama katazo kwa lazima au kwa hiari, au yaliyokatazwa kwa uharamu au machukizo, au halali.
  • Nikuwa aliyoyanyamazia Mwenyezi Mungu akawa hakuyafaradhisha, na hakuyawekea mpaka, na wala hakuyakataza, basi hayo ndio halali.
  • Uzuri wa ufafanuzi wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake kiasi ambacho ameileta hadithi kwa migawanyiko hii ya wazi.
  • Uwajibu wa kuhifadhi faradhi za Mwenyezi Mungu Mtukufu.
  • Uharamu wa kuvuka mipaka ya Mwenyezi Mungu Mtukufu.
Ufafanuzi: العربية

يخبر النبي صلى الله عليه وسلم أن الله أوجب أشياء وفرض فرائض فالتزموها ولا تفرطوا فيها بالترك أو التهاون فيها، وجعل لكم حواجز وزواجر مقدرةً تحجزكم وتزجركم عما لا يرضاه، فلا تزيدوا عليها عمَّا أمر به الشرع، وحرم محرمات فلا تتناولوها ولا تقربوها، وما عدا ذلك تركها وسكت عنها رحمة بعباده، فتبقى على أصل إباحتها فلا تبحثوا عنها.

  • الحديث دليل على أن الله هو المشرع فالأمر بيده سبحانه.
  • تضمن الحديث قواعد الشرع حكمًا وإباحةً؛ إذ الحكم الشرعي إمَّا مسكوتٌ عنه أو متكلَّم به، وهو إما: مأمورٌ به وجوبًا أو ندبًا، أو منهيٌّ عنه تحريمًا أو كراهةً، أو مباحٌ.
  • أن ما سكت الله عنه فلم يفرضه، ولم يحده، ولم ينه عنه فهو الحلال.
  • حسن بيان النبي صلى الله عليه وسلم حيث ساق الحديث بهذا التقسيم الواضح البين .
  • وجوب المحافظة على فرائض الله تعالى.
  • تحريم التعدي على حدود الله تعالى.

Mada

Ripoti kosa

Zaidi