Hadithi

Dini ni nasaha

Chanzo: HadeethEnc.com, Kiswahili v1.18.0

SahihiImepokelewa Imamu Muslim

Matini ya Kiarabu

عَنْ أَبِي رُقَيَّةَ تَمِيمِ بْنِ أَوْسٍ الدَّارِيِّ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ أَنَّ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: «الدِّينُ النَّصِيحَةُ» قُلْنَا: لِمَنْ؟ قَالَ: «لِلهِ وَلِكِتَابِهِ وَلِرَسُولِهِ وَلِأَئِمَّةِ الْمُسْلِمِينَ وَعَامَّتِهِمْ».

Tafsiri

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Ruqaiyya Tamim Ausi Ad-dari -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Yakuwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Dini ni nasaha" Tukasema: Kwa ajili ya nani? Akasema: "Kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na kitabu chake, na Mtume wake, na kwa viongozi wa waislamu na watu wote."

Ufafanuzi

Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa dini imesimama katika msingi wa utakasifu wa nia na ukweli, ili itekelezwe kama alivyowajibisha Mwenyezi Mungu kikamilifu pasina mapungufu au udanganyifu. Pakasemwa kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake: Zinakuwa kwa nani nasaha? Akasema: Kwanza: Nasaha ni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu Aliyetakasika na kutukuka: Kwa kutakasa matendo kwa ajili yake, na kutomshirikisha, na tuamini ulezi wake na uungu wake na majina yake na sifa zake, na kutukuza amri zake, na kuwaita watu kuja katika kumuamini. Pili: Nasaha kwa ajili ya kitabu chake ambacho ni Qur'ani tukufu: Tuitakidi kuwa ni maneno yake, na ni kitabu chake cha mwisho, na kwamba kimefuta sheria zote zilizokuwa kabla yake, na tunakitukuza na kukisoma haswa ipasavyo, na tunazifanyia kazi aya zake,zilizo wazi na tunazikubali zenye kutatiza na tunapingana na tafsiri mbaya ya wenye kuzipotosha, na tunachukua mazingatio kwa mawaidha yake, na kuisambaza elimu yake, na kuwalingania watu kwayo. Tatu: Nasaha kwa ajili ya Mtume wake Muhammadi rehema na amani ziwe juu yake: Kwa sisi kuitakidi kuwa yeye ni mwisho wa Mitume, na kumuamini kwa yale aliyokuja nayo, na tutekeleza amri yake, na tuepuke makatazo yake, na tusimuabudu Mwenyezi Mungu isipokuwa kwa yale aliyokuja nayo, na tunaitukuza na tunaiheshimu, na tunautangaza ujumbe wake, na kuisambaza sheria yake, na kupinga tuhuma zote dhidi yake. Nne: Nasaha kwa viongozi wa Waislamu: Kwa kuwasaidia katika haki, na kutozozana nao katika uongozi, na kuwasikiliza na kuwatii katika kumtii Mwenyezi Mungu. Tano: Nasaha kwa Waislamu: Kwa kuwatendea wema na kuwalingania, na kuacha kuwaudhi, na kuwapendelea heri, na kusaidizana nao katika wema na uchamungu.

Mafunzo

  • Amri ya kunasihiana ni kwa watu wote.
  • Ukubwa na utukufu wa nafasi ya nasaha katika dini.
  • Dini imekusanya mambo ya itikadi, maneno, na matendo.
  • Miongoni mwa nasaha ni kujinasihi mwenyewe kutomfanyia udanganyifu yule mwenye kunasihiwa pamoja na kumtakia kheri.
  • Uzuri wa mafundisho ya Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-, kiasi kwamba anataja jambo kwa ujumla kisha analifafanua.
  • Kuanza na lenye umuhimu zaidi kisha linalofuata, kwani alianza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kwa nasaha kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, kisha kitabu chake, kisha Mtume wake -Rehema na amani ziwe juu yake- kisha viongozi wa waislamu, kisha watu wote kwa ujumla.
Ufafanuzi: العربية

أَخبَرَ النبيُّ صلى الله عليه وسلم بأنَّ الدين قائمٌ على الإخلاص والصدق، حتى يؤدَّى كما أوجب الله، كاملًا دون تقصير أو غش. فقيل للنبي صلى الله عليه وسلم: لمن تكون النصيحة؟ فقال: أولًا: النصيحة لله سبحانه وتعالى: بإخلاص العمل له، وعدم الإشراك به، وأن نؤمن بربوبيته وألوهيته وأسمائه وصفاته، وتعظيم أمره، والدعوة إلى الإيمان به. ثانيًا: النصيحة لكتابه وهو القرآن الكريم: بأن نعتقد أنه كلامُه، وآخِرُ كتبِه، وأنه ناسخ لجميع الشرائع قبله، ونعظِّمه، ونتلوه حق تلاوته، ونعمل بمُحْكَمِه، ونسلم بمتشابهه، ونَذُبُّ عن تأويل المُحرِّفين له، ونعتبر بمواعظه، وننشر علومه، وندعو إليه. ثالثًا: النصيحة لرسوله محمد صلى الله عليه وسلم: بأن نعتقدَ أنه آخِرُ الرسل، ونصدِّقَه فيما جاء به، ونَمتَثِلَ أمرَه، ونجتنبَ نهيَه، وأن لا نتعبدَ لله إلا بما جاء به، ونُعظِّمَ حقَّه، ونوقرَه، ونَبُثَّ دعوته، ونَنشُرَ شريعتَه، ونَنفيَ التُّهَمَ عنه. رابعًا: النصيحة لأئمة المسلمين: بمعاونتهم على الحق، وعدم منازعتهم الأمر، والسمع والطاعة لهم في طاعة الله. خامسًا: النصيحة للمسلمين: بالإحسان إليهم ودعوتهم، وكَفِّ الأذى عنهم، ومحبة الخير لهم، والتعاون معهم على البر والتقوى.

  • الأمر بالنصيحة للجميع.
  • عِظَم منزلة النصيحة من الدين.
  • اشتمال الدين على الاعتقادات والأقوال والأعمال.
  • من النصيحة تصفية النفس من الغش للمنصوح له وإرادة الخير له.
  • حسن تعليم الرسول صلى الله عليه وسلم حيث يذكر الشيء مُجملًا ثم يُفصّله.
  • البداءة بالأهم فالأهم، حيث بدأ النبي صلى الله عليه وسلم بالنصيحة لله، ثم لكتابه، ثم لرسوله صلى الله عليه وسلم ثم لأئمة المسلمين، ثم عامتهم.

Mada

Ripoti kosa

Zaidi