Hadithi

Hawezi kuwa na imani mmoja wenu mpaka ampendelee ndugu yake anachokipenda yeye katika nafsi yake

Chanzo: HadeethEnc.com, Kiswahili v1.18.0

SahihiWamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake

Matini ya Kiarabu

عَنْ أَبِي حَمْزَةَ أَنَسِ بْنِ مَالِكٍ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ -خَادِمِ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ- عَنْ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: «لاَ يُؤْمِنُ أَحَدُكُمْ، حَتَّى يُحِبَّ لِأَخِيهِ مَا يُحِبُّ لِنَفْسِهِ»

Tafsiri

Kutoka kwa Abuu Hamza Anas bin Maaliki radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake mtumishi wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake, kutoka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake amesema: "Hawezi kuwa na imani mmoja wenu mpaka ampendelee ndugu yake anachokipenda yeye katika nafsi yake".

Ufafanuzi

Amebainisha wazi Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa imani kamili ya Muislamu yeyote haikamiliki mpaka ampendelee nduguye anachokipenda yeye, katika matendo mema, na aina mbalimbali za wema katika dini na dunia, na achukie kwake kinachochukiwa na nafsi yake, na ikiwa ataona kwa ndugu yake Muislamu kuna upungufu katika dini yake, basi ajitahidi kurekebisha, na akiona kuna jambo la kheri basi amtie moyo na amsaidie, na amnasihi katika dini yake au mambo ya dunia yake.

Mafunzo

  • Ulazima wa mtu kumpendelea ndugu yake kile anachokipenda kwa nafsi yake. Kwa sababu kukanushwa imani kwa mtu ambaye hampendelei ndugu yake kile anachopenda yeye mwenyewe kunaonyesha ulazima wa hilo.
  • Udugu kwa ajili ya Mwenyezi Mungu uko juu zaidi kuliko udugu wa nasaba (ukoo), kwani haki yake ni wajibu.
  • Katazo la maneno na vitendo vyote vinavyopingana na upendo huu, kama vile udanganyifu, kusengenya, husuda, na uadui dhidi ya mtu, au mali yake, au heshima yake.
  • Kutumia baadhi ya maneno yanayotia hamasa ya kufanya matendo; kwa kauli yake "Kwa ndugu yake".
  • Amesema Al-Kirmani, Mwenyezi Mungu amrehemu: Pia ni sehemu ya imani kuchukia kwa ndugu yake uovu anaouchukia kwa nafsi yake, na hili (Mtume) hakulitaja, kwa sababu kukipenda kitu kunalazimu kuchukia kinyume chake, hivyo kuacha kutolisema hilo inatosha.
Ufafanuzi: العربية

بَيَّنَ النبيُّ صلى الله عليه وسلم أنّه لا يَتَحقّق الإيمانُ الكامل لأحدٍ من المسلمين حتى يُحبَّ لأخيه ما يحب لنفسه من الطاعات وأنواع الخيرات في الدين والدنيا، ويكره له ما يكره لنفسه، فإن رأى في أخيه المسلم نقصًا في دينه، اجتهد في إصلاحه، وإنْ رأى فيه خيرًا سدَّده وأعانه، ونصحَه في أمر دينِه أو دنياه.

  • وجوب محبة المرء لأخيه ما يحبُّ لنفسه؛ لأن نفي الإيمان عمن لا يحب لأخيه ما يحب لنفسه يدل على وجوب ذلك.
  • الأُخوّة في الله فوق أخوّة النسب، فحقُّها أوجب.
  • تحريم كل ما ينافي هذه المحبة من الأقوال والأفعال كالغش والغيبة والحسد والعدوان على نفس المسلم أو ماله أو عرضه.
  • استخدام بعض الألفاظ المحفِّزة على الفعل؛ لقوله "لأخيه".
  • قال الكِرْماني رحمه الله: ومن الإيمان أيضًا أنْ يُبغِضَ لأخيه ما يبغض لنفسه من الشر، ولم يذكره؛ لأنَّ حب الشيء مستلزم لبغض نقيضه، فترك التنصيص عليه اكتفاء.

Mada

Ripoti kosa

Zaidi