Chanzo: HadeethEnc.com, Kiswahili v1.18.0
Matini ya Kiarabu
عَنْ أَبِي مَسْعُودٍ عُقْبَةَ بْنِ عَمْرٍو الأَنْصَارِيِّ البَدْرِيِّ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ: «إِنَّ مِمَّا أَدْرَكَ النَّاسُ مِنْ كَلاَمِ النُّبُوَّةِ الأُولَى: إِذَا لَمْ تَسْتَحْيِ فَاصْنَعْ مَا شِئْتَ».
Tafsiri
Kutoka kwa Abuu Masoud Uqba ni Amri Al-Answari Al-Badri radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu: "Hakika katika yale waliyoyakuta watu miongoni mwa maneno ya kiutume ya mwanzo, usipokuwa na haya basi fanya ulitakalo".
Ufafanuzi
Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa katika yale yaliyokuja na usia ndani yake kutoka kwa Manabii waliotangulia, na yakaenea kwa watu na watu wakarithishana kutoka kwao karne baada ya karne, mpaka yakamfikia wa mwanzo katika umma huu, ni; tazama unayotaka kuyafanya, ikiwa yatakuwa ni katika mambo ambayo si aibu basi fanya, na ikiwa ni katika mambo ya aibu basi acha; kwa sababu kinachozuia kufanya matendo mabaya ni haya, atakayekosa aibu basi hutumbukia katika kila machafu na maovu.
Mafunzo
- Kuwa na Haya ndio asili ya tabia njema.
- Haya ni sifa miongoni mwa sifa za Manabii amani iwe juu yao, nayo ni katika mambo yaliyopokelewa kutoka kwao.
- Haya ni ile inayomfanya muislamu kufanya yanayompa muonekano mzuri na wa kupendeza, na kuacha yanayomchafua na kuharibu muonekano.
- Amesema Imam Nawawi: Amri iliyoko ndani yake ni ya uhalali, maana yake: Ukitaka kufanya jambo, ikiwa ni jambo ambalo hutoona haya kwa Mwenyezi Mungu au kwa watu, basi lifanye, vinginevyo usifanye, na huu ndio mwenendo wa Uislamu, na muongozo wa hayo ni kuwa amri zote na wajibu na sunna, ni aibu kuziacha, na yaliyokatazwa na haramu na haya ni aibu kuyafanya, na ama ya halali kuona haya kuifanya inajuzu, na vile vile kuiacha, Hadithi hii imekusanya hukumu tano, na imesemwa kuwa: Ni amri ya kutishia, na maana yake nikuwa: Iwapo staha itaondolewa, basi fanya chochote unachotaka; kwani Mwenyezi Mungu atakulipa kwa hilo, na ikasemwa kuwa: Ni amri kwa maana ya habari, maana yake: Asiyekuwa na haya anafanya apendavyo.
Ufafanuzi: العربية
أَخْبَرَ النبيُّ صلى الله عليه وسلم أنَّ مما جاء فيه الوصية عن الأنبياء المتقدِّمين، وتَدَاوَلَه الناس بينهم وتوارثوه عنهم قرنًا بعد قرن، حتى وصل إلى أوّل هذه الأمة، انظر إلى ما تريد أنْ تَفعلَه، فإنْ كان ممّا لا يُستَحى منه فافعله، وإنْ كان ممّا يُستَحى منه فَدَعْه؛ فإنَّ المانع مِن فِعْل القبائح هو الحياء، فمَن لم يكن له حياءٌ، انْهَمَك في كلّ فَحْشاء ومُنكر.
- الحياء أصل الأخلاق الكريمة.
- الحياء صفة من صفات الأنبياء عليهم السلام، وهو من المأثور عنهم.
- الحياء هو الذي يجعل المرء المسلم يفعل ما يُجَمِّلُ ويَزِيْن، ويَترك ما يُدّنِّس ويَشَيْن.
- قال النووي: الأمر فيه للإباحة، أي: إذا أردت فعل شيء فإن كان مما لا تستحي إذا فعلتَه من الله ولا من الناس فافعله، وإلا فلا، وعلى هذا مدار الإسلام، وتوجيه ذلك أنَّ المأمورَ به الواجب والمندوب يُستحيَى مِن تَرْكِه، والمنهي عنه الحرام والمكروه يُستحيى من فعله، وأما المباح فالحياء من فعله جائز، وكذا مِن تركه، فتضمن الحديث الأحكام الخمسة، وقيل: هو أمرُ تهديد، ومعناه: إذا نُزِع مِنك الحياء فافعل ما شئت؛ فإنّ الله مجازيك عليه، وقيل: هو أمرٌ بمعنى الخبر، أي: مَن لا يَستحيي يَصنع ما أراد.