Chanzo: HadeethEnc.com, Kiswahili v1.18.0
Matini ya Kiarabu
عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ بُسْرٍ رَضِيَ اللَّهِ عَنْهُ قَالَ: أَتَى النَّبِيَّ رَجُلٌ، فَقَالَ: يَا رَسُولَ اللَّهِ! إِنَّ شَرَائِعَ الإِسْلَامِ قَدْ كَثُرَتْ عَلَيْنَا، فَبَابٌ نَتَمَسَّكُ بِهِ جَامِعٌ؟ قَالَ: «لاَ يَزَالُ لِسَانُكَ رَطْبًا مِنْ ذِكْرِ اللَّهِ». وفي رواية: مِنْ حَدِيثِ مُعَاذِ بْنِ جَبَلٍ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ: آخِرُ مَا فَارَقْتُ عَلَيْهِ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ أَنْ قُلْتُ: أَيُّ الأَعْمَالِ خَيْرٌ وَأَقْرَبُ إِلَى اللَّهِ؟ قَالَ: «أَنْ تَمُوتَ وَلِسَانُكَ رَطْبٌ مِنْ ذِكْرِ اللَّهِ عَزَّ وَجَلَّ».
Tafsiri
Kutoka kwa Abdallah bin Busri radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake amesema: Mtu mmoja alikuja kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake, akasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu! Hakika sheria za Uislamu zimekuwa nyingi kwetu, ni mlango gani tushikamane nao uliokusanya mambo mengi? Akasema: "Ulimi wako usiache kuwa mbichi kwa kumtaja Mwenyezi Mungu". Na katika riwaya nyingine: Miongoni mwa hadithi za Muadhi radhi za Mwneyezi Mungu ziwe juu yake: Maneno ya mwisho niliochana na Mtume rehema na amani ziwe juu yake nilisema: Ni amali ipi bora na iko karibu zaidi na Mwenyezi Mungu? Akasema: "Ni ufe hali yakuwa ulimi wako ni mbichi kwa kumtaja Mwenyezi Mungu Aliyetakasika na Kutukuka".
Ufafanuzi
Mtu mmoja alilalamika kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa ibada za sunna zimekuwa nyingi kwake mpaka zikamshinda kwa sababu ya udhaifu wake, kisha akamuuliza Mtume rehema na amani ziwe juu yake amuelekeze katika amali nyepesi itakayompa thawabu nyingi atakayoshikamana nayo na adumu nayo. Mtume rehema na amani ziwe juu yake akamuelekeza kuwa ulimi wake uwe mbichi utikisike kwa kudumu kumtaja Mwenyezi Mungu Mtukufu kila wakati na kila hali; kama kumsabihi na kumhimidi na kumtaka msamaha na kumuomba na mfano wake.
Mafunzo
- Fadhila za kudumu na kumtaja Mwenyezi Mungu Mtukufu.
- Miongoni mwa fadhila za Mwenyezi Mungu ni kufanya sababu za kupata malipo kuwa nyepesi.
- Watu kuzidiana katika mafungu yao katika milango ya wema na kheri.
- Kumtaja Mwenyezi Mungu kwa wingi kwa ulimi, kwa kumsabihi na kumhimidi, na kukiri kuwa hapana mola muabudiwa wa haki ila yeye, na kumtukuza, na mengineyo pamoja na moyo kwenda sambamba na ulimi, hili linakaa nafasi ya ibada nyingi za sunna.
- Kuchunga kwake Mtume rehema na amani ziwe juu yake hali ya muulizaji kwa kumjibu kila linalomfaa.
Ufafanuzi: العربية
شَكَى رجلٌ إلى النبيِّ صلى الله عليه وسلم بأن نوافل العبادات قد كَثرت عليه حتى عجز عنها لضعفه، ثم سألَ النبيَّ صلى الله عليه وسلم أنْ يَدلَّه على عملٍ يسيرٍ مُسْتجلِبٍ لثواب كثير يتعلق به ويستمسك. فأرشده صلى الله عليه وسلم بأن يكون لسانه طَرِيًّا متحركًا من دوام ذكر الله سبحانه وتعالى في كل وقت وحال؛ من تسبيح وتحميد واستغفار ودعاء ونحو ذلك.
- فضل المداومة على ذكر الله تعالى.
- من عظيم فضل الله تيسير أسباب الأجر.
- تفاضل العباد في نصيبهم من أبواب البر والخير.
- كثرة ذكر الله باللسان تسبيحًا وتحميدًا وتهليلًا وتكبيرًا وغير ذلك مع مواطأة القلب يقوم مقام كثير من نوافل الطاعات.
- مراعاته صلى الله عليه وسلم للسائلين بإجابة كلٍّ بما يناسبه.