Hadithi

Atakayesema: Laa ilaah illa llaah, na akayapinga yote yanayoabudiwa kinyume na Mwenyezi Mungu itakuwa haramu mali yake na damu yake, na hesabu yake itakuwa juu ya Allah

Chanzo: HadeethEnc.com, Kiswahili v1.18.0

SahihiImepokelewa Imamu Muslim

Matini ya Kiarabu

عن طارق بن أشيم الأشجعي رضي الله عنه قال: سمعت رسول الله صلى الله عليه وسلم يقول: «مَنْ قَالَ: لَا إِلَهَ إِلَّا اللهُ، وَكَفَرَ بِمَا يُعْبَدُ مِنْ دُونِ اللهِ حَرُمَ مَالُهُ وَدَمُهُ، وَحِسَابُهُ عَلَى اللهِ».

Tafsiri

Kutoka kwa Twariki bin Ashiyam Al-Ashjai Radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Nilimsikia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akisema: "Atakayesema: Laa ilaah illa llaah, na akayapinga yote yanayoabudiwa kinyume na Mwenyezi Mungu itakuwa haramu mali yake na damu yake, na hesabu yake itakuwa juu ya Allah".

Ufafanuzi

Anaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa atakayesema na akashuhudia kwa ulimi wake yakuwa "Hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu", Yaani: Hakuna muabudiwa kwa haki isipokuwa Allah, na akayakanusha yote yanayoabudiwa kinyume na Mwenyezi Mungu, na akajitenga na dini zote isipokuwa Uislamu, itakuwa haramu mali yake na damu yake kwa muislamu, hatumiliki isipokuwa dhahiri katika matendo yake, hapokonywi mali yake na wala haimwagwi damu yake, isipokuwa atakapofanya uhalifu au jinai linalopelekea hivyo kwa mujibu wa hukumu za Uislamu. Na Allah atasimamia hesabu yake siku ya Kiyama, akiwa ni mkweli atamlipa, na akiwa mnafiki atamuadhibu.

Mafunzo

  • Kutamka Laa ilaaha illah llaah, na kuyapinga yanayoabudiwa kinyume na Mwenyezi Mungu, ni sharti la kuingia katika Uislamu.
  • Maana ya (Laa ilaaha illa llaah) ni kupinga kila kinachoabudiwa kinyume na Allah yakiwamo masanamu na makaburi na mengineyo, na kumpwekesha yeye Mtukufu kwa ibada.
  • Atakayeileta tauhidi na akashikamana na sheria zake kwa dhahiri ni wajibu kujizuia kutomtendea baya mpaka yabainike yanayokwenda kinyume na hilo.
  • Uharamu wa kula mali ya Muislamu na kumwaga damu yake na kuvunja heshima yake ila kwa haki.
  • Hukumu duniani ni kwa yale yanayoonekana, na akhera ni katika nia na makusudio.
Ufafanuzi: العربية

يُخبِرُ النَّبيُّ صلَّى اللهُ عليه وسلَّمَ أنَّ مَن قالَ وشَهِدَ بلِسانِه أنَّه «لا إلهَ إلَّا اللهُ»، أي: لا مَعبودَ بِحَقٍّ إلا اللهُ، وكفَرَ بما يُعبَدُ من دُونِ اللهِ، وتَبرَّأ من كلِّ الأديانِ سِوى الإسلامِ، فقد حَرُمَ مالُه ودمُه على المُسلِمينَ، فليس لنا إلا الظاهر من عمله، فلا يُسلَبُ مالُه ولا يُسفَكُ دمُه، إلَّا إذا ارتكَبَ جَريمةً أو جِنايةً توجب ذلك بمُوجِبِ أحكامِ الإسلامِ. والله يتولَّى حسابَهُ يوم القيامة، فإن كان صادقًا أثابه، وإن كان منافقًا عَذَّبه.

  • النُّطْقُ بلا إله إلا الله، والكفر بكلِّ ما يُعبد من دون الله، شرطٌ في دخول الإسلام.
  • معنى (لا إله إلا الله) هو الكفر بكل ما يُعبد من دون الله من الأصنام والقبور وغيرها، وإفراده سبحانه بالعبادة.
  • من أتى بالتوحيد والتَزمَ شرائعه ظاهرًا وَجَبَ الكَفُّ عنه حتى يَتَبَيَّنَ منه ما يخالف ذلك.
  • حُرْمةُ مالِ المسلم ودمِه وعرضِه إلا بحق.
  • الحُكْم في الدنيا على الظاهر، وفي الآخرة على النيات والمقاصد.

Mada

Ripoti kosa

Zaidi