Hadithi

Hawaingii Malaika nyumba ambayo ndani yake kuna mbwa au picha

Chanzo: HadeethEnc.com, Kiswahili v1.18.0

SahihiWamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake

Matini ya Kiarabu

عَنْ أَبِي طَلْحَةَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ عَنِ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: «لاَ تَدْخُلُ المَلاَئِكَةُ بَيْتًا فِيهِ كَلْبٌ وَلاَ صُورَةٌ».

Tafsiri

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Hawaingii Malaika nyumba ambayo ndani yake kuna mbwa au picha"

Ufafanuzi

Alieleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa Malaika wa rehema hawaingii nyumba ambayo ndani yake kuna mbwa au picha za viumbe hai; Hii ni kwa sababu sura ya kitu ambacho kina roho ni dhambi kubwa, na kuna uigaji wa uumbaji wa Mwenyezi Mungu, na ni njia katika njia za ushirikina, na baadhi yake ni picha ya vile vinavyoabudiwa kinyume na Mwenyezi Mungu. Ama sababu ya kujiepusha na nyumba ambayo ndani yake kuna mbwa; ni kwa sababu anakula uchafu mwingi, na ni kwa sababu baadhi mbwa huitwa mashetani; Na malaika wako dhidi ya mashetani. Na kwa sababu ya harufu mbaya ya mbwa; Malaika wanachukia harufu mbaya, na kwa sababu ni haramu kuwafuga; Hivyo mwenye kuwafuga akaadhibiwa kwa kunyimwa Malaika kuingia nyumbani kwake, na kuswali humo, na kumuombea msamaha, kumbariki yeye na nyumba yake, na kumzuilia udhia wa Shetani.

Mafunzo

  • Uharamu wa kufuga mbwa isipokuwa mbwa wa mawindo au mifugo au mazao.
  • Kuwa na picha ni miongoni mwa mambo maovu ambayo Malaika huchukizwa nayo, na kuwepo kwake mahali hapo ni sababu ya kunyimwa huruma, na hivyo hivyo kwa mbwa.
  • Malaika ambao hawaingii ndani ya nyumba ambayo ndani yake kuna mbwa au picha ni Malaika wa rehema, lakini kwa walinzi na wengine ambao wana kazi kama Malaika wa mauti, wanaingia kila nyumba.
  • Uharamu wa kutundika picha za viumbe wenye roho juu ya kuta na kwingineko.
  • Amesema Al-Khattwabi: Bali Malaika hawaingii ndani ya nyumba ambayo ndani yake kuna mbwa au picha, jambo linalopelekea uharamu wa kumiliki mbwa na picha, ama mbwa wasiokuwa haramu ni kama vile mbwa wa kuwinda, wa mazao, na wa mifugo, na picha zinazotumika katika zulia, mito, na vitu vingine, kwa kukanyagwa na kudhalilishwa hizi haziwezi kuwa sababu ya kuzuia Malaika kuingia.
Ufafanuzi: العربية

‏أَخْبَرَ النبيُّ صلى الله عليه وسلم أنَّ ملائكة الرحمة لا تدخل بيتًا فيه كلبٌ ولا صورة ذَوَات الأرواح؛ وذلك أن صورة ما فيه روح: معصية فاحشة، وفيها مضاهاة لخلق الله، ووسيلة من وسائل الشرك، وبعضها صورة ما يعبد من دون الله، وأما سبب امتناعهم من بيت فيه كلب: لكثرة أكله النجاسات، ولأن بعضها يُسمى شيطانًا؛ والملائكة ضد الشياطين، ولقبح رائحة الكلب؛ والملائكة تكره الرائحة القبيحة، ولأنها منهيٌّ عن اتخاذها؛ فعُوقِب متخذها بحرمانه دخول ملائكة الرحمة بيته، وصلاتها فيه، واستغفارها له، وتبريكها عليه وفي بيته، ودفعها أذى الشيطان عنه.

  • تحريم اقتناء الكلب إلا كلب صيد أو ماشية أو زرع.
  • اتخاذ الصور من الأمور الخبيثة التي تَنْفِر منها الملائكة، ويكون وجودها في المكان سبب لحرمان الرحمة، ومثل ذلك الكلب.
  • الملائكة الذين لا يدخلون بيتًا فيه كلب أو صورة هم ملائكة الرحمة، وأما الحَفَظَة وغيرُهم ممن لهم وظيفة كمَلَك الموت فيدخلون في كل بيت.
  • تحريم تعليق صور ذوات الأرواح على الجدران وغيرها.
  • قال الخطابي: وإنما لا تدخل الملائكة بيتًا فيه كلب أو صورة مما يحرم اقتناؤه من الكلاب والصور، فأما ما ليس بحرام من كلب الصيد والزرع والماشية والصورة التي تمتهن في البساط والوسادة وغيرهما فلا يمتنع دخول الملائكة بسببه.

Mada

Ripoti kosa

Zaidi