ٱلْقَارِعَةُ
Inayogonga!
Sikiliza na urudie
Kusikiliza tu: rekodi hii ya kufundishia haina muda wa aya unaoaminika. Ukirudia, sura nzima inaanza upya.
Inayogonga!
بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَـٰنِ ٱلرَّحِيمِ
ٱلْقَارِعَةُ
Inayogonga!
مَا ٱلْقَارِعَةُ
Ni nini inayogonga?
وَمَآ أَدْرَىٰكَ مَا ٱلْقَارِعَةُ
Na ni nini kitachokujulisha ni nini inayogonga?
يَوْمَ يَكُونُ ٱلنَّاسُ كَٱلْفَرَاشِ ٱلْمَبْثُوثِ
Siku ambayo watu watakuwa kama nondo waliotawanywa;
وَتَكُونُ ٱلْجِبَالُ كَٱلْعِهْنِ ٱلْمَنفُوشِ
Na milima itakuwa kama sufu zilizochambuliwa!
فَأَمَّا مَن ثَقُلَتْ مَوَٰزِينُهُۥ
Basi yule ambaye mizani yake itakuwa nzito.
فَهُوَ فِى عِيشَةٍ رَّاضِيَةٍ
Huyo atakuwa katika maisha ya kupendeza.
وَأَمَّا مَنْ خَفَّتْ مَوَٰزِينُهُۥ
Na yule ambaye mizani zake zitakuwa hafifu.
فَأُمُّهُۥ هَاوِيَةٌ
Huyo maskani yake yatakuwa Moto wa Hawiya!
وَمَآ أَدْرَىٰكَ مَا هِيَهْ
Na ni nini kitachokujulisha ni nini hiyo?
نَارٌ حَامِيَةٌۢ
Ni Moto mkali!
Tafsiri ya Kiswahili - Kituo cha Tafsiri cha Rowwad, toleo la 1.0.5, QuranEnc.com. Maandishi yaliyochapishwa hayajabadilishwa.