Hadithi

Inapokuja Ramadhani hufunguliwa milango ya pepo na hufungwa milango ya moto, na mashetani hufungwa minyororo

Chanzo: HadeethEnc.com, Kiswahili v1.18.0

SahihiWamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake

Matini ya Kiarabu

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ أَنَّ رَسُولَ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، قَالَ: «إِذَا جَاءَ رَمَضَانُ فُتِّحَتْ أَبْوَابُ الْجَنَّةِ، وَغُلِّقَتْ أَبْوَابُ النَّارِ، وَصُفِّدَتِ الشَّيَاطِينُ».

Tafsiri

Kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- yakwamba Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Inapokuja Ramadhani hufunguliwa milango ya pepo na hufungwa milango ya moto, na mashetani hufungwa minyororo".

Ufafanuzi

Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa unapoingia mwezi wa Ramadhani hutokea mambo matatu: La kwanza: Hufunguliwa milango ya pepo na haufungwi mlango wowote katika milango hiyo. La pili: Hufungwa milango ya moto na haufunguliwi mlango wowote katika hiyo. La tatu: Hufungwa minyororo mashetani na majini wakaidi, hawaachwi kuendelea na yale waliyokuwa nayo katika miezi mingine isiyokuwa Ramadhani. Na yote hiyo ni kwa kuutukuza mwezi wa Ramadhani, na kumhamasisha mtendaji kukithirisha ibada, kama swala na sadaka, na dhikiri na kusoma Qur'ani na mengineyo; na kujitenga mbali na madhambi na maasi.

Mafunzo

  • Fadhila za mwezi wa Ramadhani.
  • Habari njema kwa wafungaji ndani yake kuwa mwezi huu mtukufu ni msimu wa ibada na kheri.
  • Katika kufungwa mashetani ndani ya Ramadhani ni ishara ya kuondolewa udhuru kwa kila aliyelazimishwa kutekeleza sheria na ni kana kwamba anamwambia:
  • Amesema Al-Qurtubi: Ikiwa patasemwa: Inakuwaje tunaona shari na maasi yanatokea ndani ya Ramadhani kwa wingi, na kama mashetani yangefungwa basi tusingeona? Jawabu: Ni kuwa maasi hupungua kwa wafungaji swaumu ambayo zimehifadhiwa sharti zake na zikazingatiwa adabu zake, au nikuwa wanaofungwa ni baadhi ya mashetani nao ni wale wakaidi na si wote kama ilivyotangulia katika baadhi ya riwaya, au makusudio yake ni kupungua kwa shari ndani yake, na jambo hili linaonekana, kwani kutokea kwake ni mara chache kuliko miezi mingine, kwani si lazima kufungwa wote kuwa kusitokee shari wala maasi; kwa sababu hilo lina sababu zingine zisizokuwa mashetani kama nafsi chafu na mazoea mabaya na mashetani wa kibinadamu.
Ufafanuzi: العربية

أخبرَ النبيُّ صلى الله عليه وسلم أنه إذا دخل شهر رمضان حصلت ثلاثة أمور: الأول: تفتح أبواب الجنة فلم يغلق منها باب. الثاني: تغلق أبواب النيران فلم يفتح منها باب. الثالث: تشد الشياطين ومردة الجن بالسلاسل، فلا يخلصون إلى ما كانوا يخلصون إليه في غير رمضان. وكل ذلك تعظيم لهذا الشهر، وترغيب للعاملين بكثرة الطاعات من صلاة وصدقة وذكر وقراءة للقرآن وغير ذلك؛ وبالابتعاد عن الذنوب والمعاصي.

  • فضل شهر رمضان.
  • بشارة للصائمين فيه بأن هذا الشهر المبارك موسم عبادة وخير.
  • في تصفيد الشياطين في رمضان إشارة إلى رفع عذر المكلف وكأنه يقال له: قد كُفّت الشياطين عنك فلا تعتذر بهم في ترك الطاعة ولا في فعل المعصية.
  • قال القرطبي: فإن قيل: كيف نرى الشرور والمعاصي واقعة في رمضان كثيرًا فلو صفدت الشياطين لم يقع ذلك؟ فالجواب: أنها إنما تقل عن الصائمين الصوم الذي حوفظ على شروطه وروعيت آدابه، أو المصفد بعض الشياطين وهم المردة لا كلهم كما تقدم في بعض الروايات، أو المقصود تقليل الشرور فيه، وهذا أمر محسوس، فإن وقوع ذلك فيه أقل من غيره، إذ لا يلزم من تصفيد جميعهم أن لا يقع شر ولا معصية؛ لأن لذلك أسبابًا غير الشياطين كالنفوس الخبيثة والعادات القبيحة والشياطين الإنسية.

Mada

Ripoti kosa

Zaidi