Hadithi

Amesema Allah Aliyetakasika na kutukuka: Nimewaandalia waja wangu wema, vitu ambavyo jicho halijawahi kuona, wala sikio kusikia, wala haijawahi kupita katika fikira ya moyo wa binadamu yeyote

Chanzo: HadeethEnc.com, Kiswahili v1.18.0

SahihiWamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake

Matini ya Kiarabu

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ عَنْ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: «قَالَ اللَّهُ تَبَارَكَ وَتَعَالَى: أَعْدَدْتُ لِعِبَادِي الصَّالِحِينَ، مَا لاَ عَيْنٌ رَأَتْ، وَلاَ أُذُنٌ سَمِعَتْ، وَلاَ خَطَرَ عَلَى قَلْبِ بَشَرٍ» قَالَ أَبُو هُرَيْرَةَ: اقْرَؤُوا إِنْ شِئْتُمْ: {فَلاَ تَعْلَمُ نَفْسٌ مَا أُخْفِيَ لَهُمْ مِنْ قُرَّةِ أَعْيُنٍ} [السجدة: 17].

Tafsiri

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, kutoka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake amesema: "Amesema Allah Aliyetakasika na kutukuka: Nimewaandalia waja wangu wema, vitu ambavyo jicho halijawahi kuona, wala sikio kusikia, wala haijawahi kupita katika fikira ya moyo wa binadamu yeyote" Akasema Abuu Huraira: Someni mkitaka: "Basi nafsi yoyote haijui yale waliyofichiwa miongoni mwa mambo yenye kutuliza macho" [As-Sajida: 17).

Ufafanuzi

Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa Mwenyezi Mungu Aliyetakasika na kutukuka amesema: Nimetayarisha na nimeandaa kwa ajili ya kuwatukuza waja wangu wema peponi mambo ambayo uhalisia wake hakuna jicho liliwahi kuona, na wala sikio lolote kusikia wasifu wake, wala kutokea wala kupita ndani ya moyo wa binadamu yeyote uhalisia wake. Akasema Abuu Huraira radhi za Allah ziwe juu yake: Someni mkitaka: "Nafsi yoyote haijui yale waliyofichiwa miongoni mwa mambo yenye kutuliza macho" [As-Sajda: 17]

Mafunzo

  • Hadithi hii ni katika zile anazozipokea Mtume rehema na amani ziwe juu yake kutoka kwa Mola wake Mlezi, na huitwa Hadithil Qudsi au Hadithil Ilahi, nayo ni ile ambayo tamko lake na maana yake inatoka kwa Allah, isipokuwa haina upekee kama wa Qur'ani inaojipambanua nayo kwa vingine, kama kisomo chake kutumika katika ibada, na kuwa twahara kabla ya kusoma, na kuwashinda watu kwa changamoto zake, na mengineyo.
  • Himizo la kufanya matendo ya utiifu na kuacha maovu; ili kufaulu kwa kuyapata yale aliyoyaandaa Mwenyezi Mungu kwa waja wake wema.
  • Mwenyezi Mungu hakutuonyesha ndani ya kitabu chake wala mafundisho ya Mtume wake yote yaliyoko peponi, na kwamba ambayo hatujayafahamu ni makubwa kuliko tuliyoyafahamu.
  • Kumebainishwa ukamilifu wa neema za peponi, na kwamba wakazi wake watapata katika mambo ya kufurahisha yasiyokuwa na tabu wala mawazo ya namna kupatikana kwake.
  • Starehe za dunia ni zenye kuisha na Akhera ndio bora na yenye kubakia.
Ufafanuzi: العربية

أخبر النبي صلى الله عليه وسلم أن الله تبارك وتعالى قال: هيّأت وأعددت تشريفًا لعبادي الصالحين في الجنة ما لم يبصر ذاته عين، ولا سمعت وصفه أذنٌ، ولا وقع ولا مر على قلب بشر ماهيته. قال أبو هريرة رضي الله عنه: اقرؤوا إن شئتم: {فَلَا تَعْلَمُ نَفْسٌ مَا أُخْفِيَ لَهُمْ مِنْ قُرَّةِ أَعْيُنٍ} [السجدة: 17].

  • هذا الحديث مما يرويه النبي صلى الله عليه وسلم عن ربه، ويسمى بالحديث القدسي أو الإلهي، وهو الذي لفظه ومعناه من الله، غير أنه ليست فيه خصائص القرآن التي امتاز بها عما سواه، من التعبد بتلاوته والطهارة له والتحدي والإعجاز وغير ذلك.
  • الحث على عمل الطاعات وترك المنكرات؛ للفوز بما أعده الله لعباده الصالحين.
  • الله تعالى لم يُطلعنا في كتابه وسُنَّة رسوله على كل ما في الجَنَّة، وأنَّ ما لم نعلمه أعظم مما عَلِمْنَاه.
  • بيان كمال نعيم الجَنَّة، وأن أهلها يَجدون من المَسَرَّات الخَالية من كَدر أو قَلق.
  • مَتَاع الدنيا زائل والآخرة خيرٌ وأبقى.

Mada

Ripoti kosa

Zaidi