Chanzo: HadeethEnc.com, Kiswahili v1.18.0
Matini ya Kiarabu
عَنْ أَنَسٍ رَضيَ اللهُ عنه أَنَّ النَّبِيَّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: «لَا تَقُومُ السَّاعَةُ حَتَّى يَتَبَاهَى النَّاسُ فِي الْمَسَاجِدِ».
Tafsiri
Kutoka kwa Anasi bin Maliki -radhi za Allah ziwe juu yake- Ya kwamba Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Hakitosimama Kiyama mpaka watu wajifaharishe katika Misikiti".
Ufafanuzi
Anaeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake: Kuwa miongoni mwa dalili za kukaribia kwa Kiyama na kumalizika kwa Dunia, ni watu kujifaharisha kwa kuipamba Misikiti yao, au kujifaharisha kwa dunia yao ndani ya misikiti ambayo haikujengwa ila kwa ajili ya kumtaja Mwenyezi Mungu.
Mafunzo
- Uharamu wa kujifaharisha kwa Misikiti, na kwamba ni jambo lisilokubalika; kwa sababu kitendo hicho hakikufanyika kwa ajili ya Mwenyezi Mungu.
- Katazo la kuipamba Misikiti kwa rangi na vito na nakshi, na maandishi; kwa sababu ndani yake kuna kuwashughulisha wenye kuswali wanapoyatazama.
- Amesema Assanadi: Hadithi ni miongoni mwa zile ambazo uhalisia unashuhudia yaliyosemwa, ni miongoni mwa miujiza ya kushangaza ya Mtume rehema na amani ziwe juu yake.
Ufafanuzi: العربية
يخبر النبي صلى الله عليه وسلم: أن من علامات قرب يوم القيامة وانتهاء الدنيا تفاخر الناس بزخرفة مساجدهم، أو تفاخرهم بدنياهم داخل المساجد التي لم تبنَ إلا لذكر الله.
- تحريم التَّباهي بالمساجد، وأنه عَمل غير مقبول؛ لأنَّه لم يُعمل لله.
- النَّهي عن زَخْرَفة المساجد بالألوان والأصْبَاغ والنُّقوش، والكتابات؛ لما فيها من إشغال المصلين عند النظر إليها.
- قال السندي: هذا الحديث مما يشهد بصدقه الوجود، فهو من جملة المعجزات الباهرة له صلى الله عليه وسلم.