Hadithi

Hakuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake na maneno machafu wala mwenye kujilazimisha machafu, wala hakuwa na makelele masokoni, na wala alikuwa halipi ubaya kwa ubaya, lakini alikuwa akisamehe na kufuta kosa

Chanzo: HadeethEnc.com, Kiswahili v1.18.0

SahihiImepokelewa na Tirmidhiy na Ahmad

Matini ya Kiarabu

عَن أَبي عَبْدِ اللهِ الْجَدَلِيِّ قَالَ: سَأَلْتُ عَائِشَةَ أُمِّ المؤْمنينَ رَضيَ اللهُ عنها عَنْ خُلُقِ رَسُولِ اللهِ صلى الله عليه وسلم فَقَالَتْ: لَمْ يَكُنْ فَاحِشًا وَلَا مُتَفَحِّشًا وَلَا صَخَّابًا فِي الْأَسْوَاقِ، وَلَا يَجْزِي بِالسَّيِّئَةِ السَّيِّئَةَ وَلَكِنْ يَعْفُو وَيَصْفَحُ.

Tafsiri

Kutoka kwa Abuu Abdillah Al-Jadali amesema: Nilimuuliza Aisha mama wa waumini radhi za Allah ziwe juu yake kuhusu tabia za Mtume rehema na amani ziwe juu yake, akasema: Hakuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake na maneno machafu wala mwenye kujilazimisha machafu, wala hakuwa na makelele masokoni, na wala alikuwa halipi ubaya kwa ubaya, lakini alikuwa akisamehe na kufuta kosa.

Ufafanuzi

Aliulizwa mama wa waumini Aisha radhi za Allah ziwe juu yake kuhusu tabia za Mtume rehema na amani ziwe juu yake akasema: Haikuwa katika tabia zake uchafu na ubaya wa kauli na vitendo, na wala hakuwa akijilazimisha machafu wala kuyakusudia, wala hakuwa mpiga kelele kwa kunyanyua sauti yake masokoni, na wala alikuwa halipi ubaya kwa ubaya; lakini alikuwa akilipa ubaya kwa wema, na akisamehe ndani ya moyo, na akifuta kosa na kulipuuza katika dhahiri.

Mafunzo

  • Kumebainishwa tabia alizokuwa nazo Mtume rehema na amani ziwe juu yake, tabia za juu na kuwa kwake mbali na tabia mbaya.
  • Himizo la kufanya tabia njema na kujiweka mbali na tabia mbaya.
  • Kumekemewa kujilazimisha machafu katika kauli na maneno machafu.
  • Kumekemewa kunyanyua sauti juu ya watu na kuwapigia makelele.
  • Himizo la kuukabili ubaya kwa wema, na kusamehe na kufuta kosa.
Ufafanuzi: العربية

سُئلت أم المؤمنين عائشة رضي الله عنها عن خُلق النبي صلى الله عليه وسلم فقالت: لم يكن في طبعه الفحش والقبح بأقواله وأفعاله، ولا يتكلف الفحش ولا يتعمده، ولا صيّاحًا يرفع صوته في الأسواق، ولا يجزي بالسيئة السيئة؛ ولكن يجزي بالحسنة، ويعفو في الباطن، ويصفح ويعرض عنه في الظاهر.

  • بيان ما كان عليه النبي صلى الله عليه وسلم من الخلق الرفيع والبعد عن الأخلاق الذميمة.
  • الحث على فعل الأخلاق الحسنة والابتعاد عن الأخلاق السيئة.
  • ذم التكلم بالبذيء من القول والكلام القبيح.
  • ذم رفع الصوت على الناس والصياح عليهم.
  • الحث على مقابلة الإساءة بالحسنة والعفو والمسامحة.

Mada

Ripoti kosa

Zaidi