Chanzo: HadeethEnc.com, Kiswahili v1.18.0
Matini ya Kiarabu
عَنْ أُمِّ عَطِيَّةَ رَضيَ اللهُ عنها قَالَتْ: تُوُفِّيَتْ إِحْدَى بَنَاتِ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، فَخَرَجَ النَّبِيُّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فَقَالَ: «اغْسِلْنَهَا ثَلاَثًا، أَوْ خَمْسًا أَوْ أَكْثَرَ مِنْ ذَلِكَ، إِنْ رَأَيْتُنَّ بِمَاءٍ وَسِدْرٍ، وَاجْعَلْنَ فِي الآخِرَةِ كَافُورًا -أَوْ شَيْئًا مِنْ كَافُورٍ-، فَإِذَا فَرَغْتُنَّ فَآذِنَّنِي»، قَالَتْ: فَلَمَّا فَرَغْنَا آذَنَّاهُ، فَأَلْقَى إِلَيْنَا حِقْوَهُ، فَقَالَ: «أَشْعِرْنَهَا إِيَّاهُ»، وَقَالَتْ: وَجَعَلْنَا رَأْسَهَا ثَلاَثَةَ قُرُونٍ.
Tafsiri
Kutoka kwa Ummu Atwiya radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake amesema: Alifariki mmoja kati ya mabinti wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake, akatoka Mtume rehema na amani ziwe juu yake akasema: "Muosheni mara tatu, au mara tano au zaidi ya hapo, mkiona kuna haja ya kuzidisha, kwa maji na mkunazi, na mwisho muweka kafuri -au chochote katika kafuri-, mkimaliza nipeni idhini" Anasema: tulipomaliza tulimpa idhini, akatupatia kikoi chake, akasema: "Mfunikeni kwa kikoi hiki", anasema: Na tukafanya (nywele za) kichwa chake kuwa mafungu matatu.
Ufafanuzi
Alifariki Zainab binti wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake, akaingia rehema na amani ziwe juu yake kwa wanawake waliotakiwa kumuosha, akasema: Muosheni kwa maji na Mkunazi kwa witiri mara tatu, au mara tano au zaidi ya hapo, ikiwa kuna haja ya kufanya hivyo, na muweke katika muosho wa mwisho chochote katika kafuri, na mkimaliza nijulisheni. Walipomaliza kumuosha wakampa idhini, akawapa waoshaji kikoi chake, na akasema: Mzungushieni ndani yake na muifanye kuwa ndio nguo inayofuata mwili wake, kisha kikafanywa kichwa chake kuwa na mafungu matatu ya nywele.
Mafunzo
- Uwajibu wa kumuosha maiti wa kiislamu, na kuwa hilo ni faradhi kifaya (wakipatikana wanaotosheleza madhambi yanawaondokea wengine).
- Mwanamke haoshwi ila na wanawake wenzake, na mwanaume haoshwi ila wanaume, isipokuwa wale walioruhusiwa kama mwanamke pamoja na mume wake, na mjakazi na bosi wake, hao wote kila mmoja anaruhusiwa kumuosha mwenzake.
- Josho linakuwa kwa miosho mitatu, isipotosha, basi mitano, na isipotosha, itazidishwa zaidi ya hapo, kulingana na masilahi na haja ya kufanya hivyo, na baada ya hapo ikiwa najisi itatoka katika mwili wake, itazibwa sehemu unapotoka udhia huo.
- Atakamilisha muoshaji uoshaji wake kwa witiri, tatu, au tano, au saba.
- Amesema Assanadi: Hakuna kikomo katika kumuosha maiti bali kinachotakiwa ni kumsafisha, lakini ni lazima kuzingatia witiri.
- Maji yawe pamoja na Mkunazi; kwa sababu hutakatisha, na kuufanya mwili wa maiti kuwa mkavu.
- Maiti hutiwa manukato kwa josho lake la mwisho, ili maji yasimalizike, na marashi yawe ya kafuri, kwa sababu pamoja na harufu nzuri, huukaza mwili, na kuufanya usiharibike haraka.
- Kuanza kwa kuosha viungo vitukufu, navyo ni vile vya kulia, na viungo vya udhu.
- Kupendeza kuchana nywele za maiti na kuzifunga mafundo matatu, na kuziweka nyuma ya maiti.
- Inafaa kusaidizana katika kumuosha maiti lakini asihudhurie ila yule anayehitajika.
- Kutaka baraka kupitia athari za Mtume rehema na amani ziwe juu yake kama mavazi yake, na hili ni jambo maalumu kwake, halivuki kwenda kwa mtu mwingine katika wanachuoni na watu wema; kwa sababu mambo hayo yanahitaji msingi wa sheria, na Maswahaba hawakuwahi kulifanya hilo na yeyote katu; na ni kwa sababu kufanywa hilo na mtu mwingine ni sababu ya kuingia katika ushirikina na fitina kwa atakayetakwa baraka.
- Inafaa kumpa kazi mtu mwaminifu kwa kile alichoaminiwa kwacho, ikiwa anastahiki kupewa kazi.
Ufafanuzi: العربية
توفيت زينب بنت النبي صلى الله عليه وسلم، فدخل صلى الله عليه وسلم على النسوة اللاتي سيغسلنها فقال لهن: اغسلنها بماء وسدر وترًا ثلاثًا، أو خمسًا أو أكثر من ذلك، إن كان هناك حاجة، واجعلن في الغسلة الآخرة شيئًا من كافور، فإذا فرغتنَّ فأخبرنني. فلما فرغن من تغسيلها آذناه، فأعطى إزاره المغسلات، وقال: ألففنها فيه واجعلْنه هو الثوب الذي يلي جسدها، ثم جُعل رأسها ثلاثة ظفائر.
- وجوب غسل الميت المسلم، وأنه فرض كفاية.
- المرأة لا يغسلها إلا النساء، والرجل لا يغسله إلا الرجال، إلا ما استثنى من المرأة مع زوجها، والأمَة مع سيدها، فلكل منهما غسل صاحبه.
- يكون الغسل بثلاث غسلات، فإن لم يكفِ، فخمس، فإن لم يكفِ، زِيدَ على ذلك، بحسب المصلحة والحاجة، وبعد ذلك إن كان ثَمَّ شيء من النجاسات خرج من الجسد، سُدَّ المحل الذي يخرج منه الأذى.
- يقطع الغاسل غسلاته على وتر، ثلاثٍ، أو خمسٍ، أو سبعٍ.
- قال السندي: يدل الحديث على أنه لا تحديد في غسل الميت بل المطلوب التنظيف لكن لا بد من مراعاة الإيتار.
- يكون مع الماء سِدر؛ لأنه يُنَقي، ويُصلب جسد الميت.
- يُطَيَّبَ الميت مع آخر غسلاته، لئلا يذهب الماءُ، ويكون الطيب من كافور، لأنه -مع طيب رائحته- يشد الجسد، فلا يسرع إليه الفساد.
- البداءة بغسل الأعضاء الشريفة، وهي: الميامن، وأعضاء الوضوء.
- استحباب تسريح شعر الميتة وضفره ثلاث ضفائر، وجعله خلف الميتة.
- جواز التعاون في غسل الميت لكن لا يحضر إلا من يحتاج إليه.
- التبرك بآثار النبي صلى الله عليه وسلم كملابسه، وهذا شيء خاصٌّ به، فلا يتعدَّاه إلى غيره من العلماء والصالحين؛ لأن هذه الأشياء توقيفية، والصحابة لم يعملوها مع غيره قط؛ ولأنه مع غيره وسيلة للشرك وفتنة لمن تُبرك به.
- جواز تفويض الشخص الأمين في العمل بما أؤتمن عليه إذا كان أهلًا للتفويض.