Hadithi

Basi itakapokuja Ramadhani, basi fanya Umra, kwani Umra ndani ya Ramadhani ni sawa na Hija.”

Chanzo: HadeethEnc.com, Kiswahili v1.18.0

SahihiWamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake

Matini ya Kiarabu

عَنِ ابْنِ عَبَّاسٍ رضي الله عنهما قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ لِامْرَأَةٍ مِنَ الْأَنْصَارِ سَمَّاهَا ابْنُ عَبَّاسٍ فَنَسِيتُ اسْمَهَا: «مَا مَنَعَكِ أَنْ تَحُجِّي مَعَنَا؟» قَالَتْ: لَمْ يَكُنْ لَنَا إِلَّا نَاضِحَانِ فَحَجَّ أَبُو وَلَدِهَا وَابْنُهَا عَلَى نَاضِحٍ وَتَرَكَ لَنَا نَاضِحًا نَنْضِحُ عَلَيْهِ، قَالَ: «فَإِذَا جَاءَ رَمَضَانُ فَاعْتَمِرِي، فَإِنَّ عُمْرَةً فِيهِ تَعْدِلُ حَجَّةً».

Tafsiri

Imepokelewa kutoka kwa bin Abbas -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -rehema na amani ziwe juu yake- kumwambia mwanamke mmoja miongoni mwa Ansari (Watu wa Madina) ambaye bin Abbas alimtaja kwa jina, lakini mimi nimelisahau jina lake: “Ni nini kilikuzuia kuhiji pamoja nasi?” Akasema: Sisi tulikuwa na vilemba viwili tu, basi baba wa mwanawe na mwanawe walihiji kwa kilemba hicho na akatuachia kilemba kimoja ili tukifue.” Akasema: «Basi itakapokuja Ramadhani, basi fanya Umra, kwani Umra ndani ya Ramadhani ni sawa na Hija.”

Ufafanuzi

Mtume, rehema na amani ziwe juu yake, aliporejea kutoka katika Hija ya kuaga, alimwambia mwanamke mmoja wa Ansari ambaye hakuhiji: Ni nini kilikuzuia kuhiji pamoja nasi? Akatoa udhuru kwa sababu walikuwa na ngamia wawili, hivyo mume wake na mwanawe walihiji kwa mmoja wao, na kumwacha mwingine akichota maji kisimani. Mtume, Rehema na amani ziwe juu yake, akamwambia kuwa kufanya Umra katika mwezi wa Ramadhani ni sawa na malipo ya Hija.

Mafunzo

  • Fadhila za Umra ndani ya mwezi wa Ramadhani.
  • Umra ndani ya Ramadhani inalingana sawa na Hija katika malipo, haina maana ya kuondosha uwajibu wa Hija.
  • Malipo ya matendo huzidi kulingana na utukufu wa nyakati, ikiwemo matendo yanayofanywa ndani ya Ramadhani.
Ufafanuzi: العربية

لمَّا رَجَعَ النبيُّ صلى الله عليه وسلم من حَجة الوداع، قال لامرأةٍ من الأنصار لم تحج: ما الذي منعك من الحج معنا؟ فاعتذرت بأن لهم بَعيرين، فحج زوجها وابنها على أحدهما، وترك الآخر ليستقوا به الماء من البئر. فأخبرها النبي عليه الصلاة والسلام أن أداء العمرة في شهر رمضان يماثل أجرُها أجرَ حجة.

  • فضيلة العمرة في شهر رمضان.
  • العمرة في رمضان تساوي حجةً في الثواب، لا في إسقاط فرض الحج.
  • ثواب الأعمال يزيد بزيادة شرف الأوقات، ومن ذلك الأعمال في رمضان.

Mada

Ripoti kosa

Zaidi