Hadithi

Sijawahi kumuona mwenye nywele ndefu na vazi jekundu zuri kuliko Mtume wa Mwenyezi Mungu rehema na amani ziwe juu yake

Chanzo: HadeethEnc.com, Kiswahili v1.18.0

SahihiWamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake

Matini ya Kiarabu

عَنِ الْبَرَاءِ رَضيَ اللهُ عنه قَالَ: مَا رَأَيْتُ مِنْ ذِي لِمَّةٍ أَحْسَنَ فِي حُلَّةٍ حَمْرَاءَ مِنْ رَسُولِ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، شَعْرُهُ يَضْرِبُ مَنْكِبَيْهِ، بَعِيدَ مَا بَيْنَ الْمَنْكِبَيْنِ، لَيْسَ بِالطَّوِيلِ وَلَا بِالْقَصِيرِ.

Tafsiri

Imepokelewa kutoka kwa Baraa -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake amesema: Sijawahi kumuona mwenye nywele ndefu na vazi jekundu zuri kuliko Mtume wa Mwenyezi Mungu rehema na amani ziwe juu yake, nywele zake zinapigapiga mabega yake, na mabega yake yako mbali mbali, si mrefu wala mfupi.

Ufafanuzi

Anaeleza Baraa bin Azibi radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake ya kwamba hajawahi kumuona yeyote nywele za kichwa chake ni ndefu zimefika katika mabega yake, na anayevaa kikoi na shuka jeusi na lenye mistari myekundu zuri kuliko Mtume wa Mwenyezi Mungu rehema na amani ziwe juu yake, na kwamba miongoni mwa sifa zake za kimaumbile ni kwamba mabega yake yalikuwa mbali mbali, mwenye kifua kipana, na alikuwa na kimo cha kati na kati, kati mrefu na mfupi.

Mafunzo

  • Hapa kumebainishwa baadhi ya sifa nzuri za Mtume- rehema na amani ziwe juu yake- katika muonekano, kama uzuri wa nywele na upana wa kifua, na uzuri wa kimo, na mengineyo.
  • Mapenzi ya Maswahaba watukufu kwa Mtume- rehema na amani ziwe juu yake-, kiasi kwamba mpaka walikuwa wakielezea na wakiwanukulia waliokuja baada yao miongoni mwa muonekano wake na sifa zake za kimwili na za kimaana (zisizoonekana).
Ufafanuzi: العربية

يخبر البراء بن عازب رضي الله عنه أنه ما رأى أحدًا شَعَرُ رأسِه طويل قد وَصَل إلى منكبيه، ويلبس إزارًا ورداءً أسود وفيه خطوط حمراء أحسن من رسول الله صلى الله عليه وسلم، وأن من صفته الخَلْقية أنه كان بعيدَ ما بين المنكبين، واسع الصدر، وكان متوسط القَامَة بين الطويل والقصير.

  • بيان بعض صفات النبي صلى الله عليه وسلم الجميلة في الظاهر من حسن الشعر ورَحَابة الصدر، وحسن القامة، وغير ذلك.
  • محبة الصحابة الكرام رضي الله عنهم للنبي صلى الله عليه وسلم، حتى أنهم يحكون وينقلون لمن بعدهم شمائله وأوصافه الجسدية والمعنوية.

Mada

Ripoti kosa

Zaidi