Hadithi

Anapoingia mtu nyumbani kwake akamtaja Mwenyezi Mungu wakati wa kuingia kwake na wakati wa chakula chake, Shetani husema: Hakuna malazi kwenu, wala chakula cha usiku

Chanzo: HadeethEnc.com, Kiswahili v1.18.0

SahihiImepokelewa Imamu Muslim

Matini ya Kiarabu

عَنْ جَابِرِ بْنِ عَبْدِ اللهِ رضي الله عنهما أَنَّهُ سَمِعَ النَّبِيَّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَقُولُ: «إِذَا دَخَلَ الرَّجُلُ بَيْتَهُ، فَذَكَرَ اللهَ عِنْدَ دُخُولِهِ وَعِنْدَ طَعَامِهِ، قَالَ الشَّيْطَانُ: لَا مَبِيتَ لَكُمْ، وَلَا عَشَاءَ، وَإِذَا دَخَلَ، فَلَمْ يَذْكُرِ اللهَ عِنْدَ دُخُولِهِ، قَالَ الشَّيْطَانُ: أَدْرَكْتُمُ الْمَبِيتَ، وَإِذَا لَمْ يَذْكُرِ اللهَ عِنْدَ طَعَامِهِ، قَالَ: أَدْرَكْتُمُ الْمَبِيتَ وَالْعَشَاءَ».

Tafsiri

ImepokelewaKutoka kwa Jabir radhi za Allah ziwe juu yake yeye na baba yake, hakika yeye alimsikia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akisema: "Anapoingia mtu nyumbani kwake akamtaja Mwenyezi Mungu wakati wa kuingia kwake na wakati wa chakula chake, Shetani husema: Hakuna malazi kwenu, wala chakula cha usiku, na anapoingia na hakumtaja Mwenyezi Mungu wakati wa kuingia kwake, Shetani husema: Mmepata malazi, na asipomtaja Mwenyezi Mungu wakati wa chakula chake, husema: Mmepata malazi na chakula cha usiku".

Ufafanuzi

Ameamrisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kumtaja Allah wakati wa kuingia nyumbani na kabla ya kupata chakula, nakuwa mtu akimtaja Mwenyezi Mungu kwa kusema: (Bismillaah) -Naanza kwa jina la Mwenyezi Mungu- wakati wa kuingia nyumbani kwake na wakati wa chakula chake, Shetani husema kuwaambia wasaidizi wake: Hamna bahati leo ya kupata malazi wala chakula cha usiku ndani ya nyumba hii ambayo mwenye nyumba kajilinda kutokana nanyi kwa kumtaja Mwenyezi Mungu Mtukufu. Na ama mtu akiingia nyumbani kwake na akawa hakumtaja Mwenyezi Mungu wakati wa kuingia kwake wala wakati wa kupata kwake chakula, Shetani huwaeleza wasaidizi wake kuwa wamepata mahali pa kulala, na chakula cha usiku ndani ya nyumba hii.

Mafunzo

  • Ni sunna kumtaja Mwenyezi Mungu wakati wa kuingia nyumbani na wakati wa chakula, kwani Shetani hulala ndani ya majumba, na hula katika chakula cha wenye nyumba ikiwa hawatomtaja Mwenyezi Mungu Mtukufu.
  • Shetani humfuatilia mwanadamu katika matendo yake na harakati zake na katika mambo yake yote, akijisahau kumtaja Allah papo hapo hupata lengo lake kwake.
  • Kumtaja Allah humfukuza Shetani.
  • Kila Shetani anawafuasi na ana vipenzi ambao huchukua ushauri wake na kufuata amri yake.
Ufafanuzi: العربية

أَمَرَ النبيُّ صلى الله عليه وسلم بِذِكْر الله عند دخول البيت وقبل تَنَاوُلِ الطعام، وأنه إذا ذَكَرَ اللهَ بقوله: (باسم الله) عند دخوله لبيتِه وعند بدء طعامِه، قال الشيطان لأعوانه: لا حَظَّ لكم بالمبيت ولا العشاء في هذا البيت الذي تَحَصَّنَ صاحبُه منكم بذكر الله تعالى. وأما إذا دخل الرجل بيته فلم يذكر الله عند دخوله ولا عند تناوله الطعام، فيخبر الشيطان أعوانه أنهم أدركوا المبيت، والعشاء في هذا البيت.

  • استحباب ذِكرِ الله عند دخول البيت وعند الطعام، فإن الشيطان يبيت في البيوت، ويأكل من طعام أهلها إذا لم يذكروا اسم الله تعالى.
  • الشيطان يُراقِبُ ابنَ آدم في عملِهِ وتَصَرُّفِه وفي أموره كلِّها، فإذا غَفَل عن الذكر نال مُرادَه منه.
  • الذكر يطرد الشيطان.
  • لكل شيطان أتباع وأولياء يستبشرون بقوله ويَتَّبعون أمرَه.

Mada

Ripoti kosa

Zaidi