Hadithi

Madhambi makubwa: Ni kumshirikisha Mwenyezi Mungu, na kuwaasi wazazi wawili, na kuuwa nafsi, na kiapo cha uongo

Chanzo: HadeethEnc.com, Kiswahili v1.18.0

SahihiImepokelewa na Al-Bukhaariy

Matini ya Kiarabu

عن عبد الله بن عمرو بن العاص رضي الله عنهما عن النبي صلى الله عليه وسلم قال: «الْكَبَائِرُ: الْإِشْرَاكُ بِاللهِ، وَعُقُوقُ الْوَالِدَيْنِ، وَقَتْلُ النَّفْسِ، وَالْيَمِينُ الْغَمُوسُ».

Tafsiri

Imepokewa kutoka kwa Abdillah Ibn Amri bin Aswi -Radhi za Allah ziwe juu yao wawili- kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-amesema: "Madhambi makubwa: Ni kumshirikisha Mwenyezi Mungu, na kuwaasi wazazi wawili, na kuuwa nafsi, na kiapo cha uongo".

Ufafanuzi

Anabainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- madhambi makubwa, nayo ni yale aliyokemewa mfanyaji wake kwa kemeo la adhabu kali duniani au Akhera. La kwanza lake "Ni kumshirikisha Mwenyezi Mungu": Nalo ni kukielekeza chochote katika aina za ibada kwa asiyekuwa Allah, na kumfanya kuwa sawa na Allah asiyekuwa Allah katika yale ambayo ni maalumu kwa Allah katika uungu wake na uumbaji wake na majina yake na sifa zake. Na la pili lake "Ni kuwaasi wazazi wawili": Nalo ni kila linalopelekea kuwaudhi wazazi wawili sawa sawa iwe kauli au kitendo, na kuacha kuwatendea wema. Na la tatu lake: "Ni kuua nafsi": Bila hatia, kama kuuwa kwa dhulma na uadui. Na la nne lake "Kiapo cha uongo": Nako ni kuapia uongo huku ukijua kuwa ni uongo, umeitwa hivyo; Kwa sababu humzamisha mfanyaji wake katika madhambi au motoni.

Mafunzo

  • Kiapo cha uongo hakina kafara; kwa ubaya wa hatari yake, bali kinatoba.
  • Kuishia kutaja madhambi makubwa haya manne katika hadithi ni kwa sababu ya ukubwa wa dhambi zake, na si kwa kudhibiti idadi yake.
  • Madhambi yanagawanyika makubwa na madogo, na dhambi kubwa ni: Kila dhambi lenye adhabu duniani, kama kusimamishiwa sheria na laana, au ahadi ya adhabu ya Akhera, kama ahadi ya adhabu ya moto, pia madhambi makubwa yana daraja, baadhi yake ni mazito kuliko mengine katika uharamu, na madhambi madogo nayo ni yale yasiyokuwa makubwa.
Ufafanuzi: العربية

يُبَيِّنُ النبيُّ صلى الله عليه وسلم كبائر الذنوب، وهي التي تُوُعِّدَ فاعلُها بوعيد شديد في الدنيا أو الآخرة. فأوَّلُها "الإِشرَاكُ بِالله": وهو صَرْفُ أيِّ نوع من أنواع العبادة لغير الله، وتسوية غير الله بالله فيما هو من خصائص الله في ألوهيته وربوبيته وأسمائه وصفاته. وثانيها "عُقُوقُ الوَالِدَينِ": وهو كلُّ ما يوجب الأذى للأبوين قولًا كان أو فعلًا، وترك الإحسان إليهما. وثالثها "قَتْل النَّفْس": بغير حق، كالقتل ظلمًا وعدوانًا. ورابعها "اليَمِين الغَمُوسُ": وهي الحلف كاذبًا على علم منه بكذبه، سميت بذلك؛ لأنَّها تَغْمِسُ صاحبَها في الإِثم أو في النار.

  • اليمين الغموس لا كفارة لها؛ لشدة خطرها وجرمها، وإنما فيها التوبة.
  • الاقتصار على ذكر هذه الكبائر الأربع في الحديث لعظيم إثمها، وليس لحصرها.
  • الذنوب تنقسم إلى كبائر وصغائر، والكبيرة هي: كلُّ ذنب فيه عقوبة دنيوية، كالحدود واللعن، أو وعيد أُخروي، كالوعيد بدخول النار، وأن الكبائر دركات بعضها أغلظ من بعض في التحريم، وصغائر الذنوب هي ما سوى الكبائر.

Mada

Ripoti kosa

Zaidi