Hadithi

Hivi nikuhadithieni hadithi kuhusu Dajali ambayo hajawahi kuhadithia Nabii yeyote watu wake! Hakika yeye ni chongo, na hakika atakuja akiwa pamoja na mfano wa pepo na moto,

Chanzo: HadeethEnc.com, Kiswahili v1.18.0

SahihiWamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake

Matini ya Kiarabu

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «أَلاَ أُحَدِّثُكُمْ حَدِيثًا عَنِ الدَّجَّالِ، مَا حَدَّثَ بِهِ نَبِيٌّ قَوْمَهُ؟ إِنَّهُ أَعْوَرُ، وَإِنَّهُ يَجِيءُ مَعَهُ بِمِثَالِ الجَنَّةِ وَالنَّارِ، فَالَّتِي يَقُولُ إِنَّهَا الجَنَّةُ هِيَ النَّارُ، وَإِنِّي أُنْذِرُكُمْ كَمَا أَنْذَرَ بِهِ نُوحٌ قَوْمَهُ».

Tafsiri

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Hivi nikuhadithieni hadithi kuhusu Dajali ambayo hajawahi kuhadithia Nabii yeyote watu wake! Hakika yeye ni chongo, na hakika atakuja akiwa pamoja na mfano wa pepo na moto, anayoisema kuwa ni pepo huo ndio moto, na hakika mimi ninakutahadharisheni kama alivyo watahadharisha Nabii Nuhu watu wake".

Ufafanuzi

Anawaeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake Maswahaba zake kuhusu Dajali, sifa zake, na dalili zake, kwa mambo ambayo hakuna Nabii yeyote aliyetangulia kuyasimulia kabla yake, miongoni mwa hayo ni: Chongo wa jicho. Na Mwenyezi Mungu kampa kitu mfano wa Pepo na Moto, kulingana na mtazamo wa macho. Bali Pepo yake ni Moto na Moto wake ni Pepo, mwenye kumtii atamuingiza katika Pepo hii kama watu wanavyoiona, lakini uhalisia wake ni Moto wenye kuunguza, na atakayemuasi atamuingiza Motoni kama watu wanavyouona, lakini kwa uhalisia ni Pepo nzuri. Kisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake akatuonya dhidi ya fitina yake kama vile Nuhu alivyowaonya watu wake kuhusu hilo.

Mafunzo

  • Ukubwa wa fitina ya Dajali.
  • Kuokoka kutokana na fitina ya Dajali kupo katika imani ya kweli, na kukimbilia kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, na kutafuta hifadhi kwa Mwenyezi Mungu dhidi yake katika tashahudi ya mwisho, na kuhifadhi aya kumi za mwanzo wa Suratul-Kahf.
  • Pupa kubwa ya Mtume rehema na amani ziwe juu yake kwa umma wake, alipowawekea wazi Waislamu sifa za Dajali ambazo hakuna mtume kabla yake aliyewahi kuzieleza.
Ufafanuzi: العربية

يُخبِرُ النبيُّ صلى الله عليه وسلم أصحابه عن الدجال وصفاته وعلاماته بما لم يحدِّث به نبي قبله، فمن ذلك: أنه أعور العين. وأن الله تعالى جعل معه مثل الجنة والنار، بحسب رؤيا العين. لكن جنته نار، وناره جنة، من أطاعه أدخله هذه الجنة فيما يرى الناس، ولكنها نار محرقة، ومن عصاه أدخله النار فيما يراه الناس، ولكنها جنة طيبة، ثم حذرنا النبي صلى الله عليه وسلم من فتنته كما حذّر به نوح قومه.

  • عظم فتنة الدجال.
  • النجاة من فتنة الدجال تكون بصدق الإيمان واللجوء إلى الله تعالى والاستعاذة بالله منه في التشهد الأخير، وحفظ عشر آيات من أول سورة الكهف.
  • شدة حرص النبي صلى الله عليه وسلم على أمته، حيث بين للمسلمين من صفات الدجال ما لم يبينه نبي قبله.

Mada

Ripoti kosa

Zaidi