Chanzo: HadeethEnc.com, Kiswahili v1.18.0
Matini ya Kiarabu
عَنْ أَنَسِ بْنِ مَالِكٍ رَضيَ اللهُ عنهُ: أَنَّ رَجُلًا دَخَلَ المَسْجِدَ يَوْمَ جُمُعَةٍ مِنْ بَابٍ كَانَ نَحْوَ دَارِ القَضَاءِ، وَرَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَائِمٌ يَخْطُبُ، فَاسْتَقْبَلَ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَائِمًا، ثُمَّ قَالَ: يَا رَسُولَ اللَّهِ، هَلَكَتِ الأَمْوَالُ وَانْقَطَعْتِ السُّبُلُ، فَادْعُ اللَّهَ يُغِيثُنَا، فَرَفَعَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَدَيْهِ، ثُمَّ قَالَ: «اللَّهُمَّ أَغِثْنَا، اللَّهُمَّ أَغِثْنَا، اللَّهُمَّ أَغِثْنَا» قَالَ أَنَسٌ: وَلا وَاللَّهِ، مَا نَرَى فِي السَّمَاءِ مِنْ سَحَابٍ وَلَا قَزَعَةً، وَمَا بَيْنَنَا وَبَيْنَ سَلْعٍ مِنْ بَيْتٍ وَلَا دَارٍ، قَالَ: فَطَلَعَتْ مِنْ وَرَائِهِ سَحَابَةٌ مِثْلُ التُّرْسِ، فَلَمَّا تَوَسَّطَتِ السَّمَاءَ انْتَشَرَتْ، ثُمَّ أَمْطَرَتْ، فَلَا وَاللَّهِ، مَا رَأَيْنَا الشَّمْسَ سِتًّا، ثُمَّ دَخَلَ رَجُلٌ مِنْ ذَلِكَ البَابِ فِي الجُمُعَةِ، وَرَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَائِمٌ يَخْطُبُ، فَاسْتَقْبَلَهُ قَائِمًا، فَقَالَ: يَا رَسُولَ اللَّهِ، هَلَكَتِ الأَمْوَالُ، وَانْقَطَعَتِ السُّبُلُ، فَادْعُ اللَّهَ يُمْسِكْهَا عَنَّا، قَالَ: فَرَفَعَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَدَيْهِ، ثُمَّ قَالَ: «اللَّهُمَّ حَوَالَيْنَا وَلَا عَلَيْنَا، اللَّهُمَّ عَلَى الآكَامِ وَالظِّرَابِ، وَبُطُونِ الأَوْدِيَةِ، وَمَنَابِتِ الشَّجَرِ» قَالَ: فَأَقْلَعَتْ، وَخَرَجْنَا نَمْشِي فِي الشَّمْسِ، قَالَ شَرِيكٌ: سَأَلْتُ أَنَسَ بْنَ مَالِكٍ: أَهُوَ الرَّجُلُ الأَوَّلُ؟ فَقَالَ: «مَا أَدْرِي».
Tafsiri
Imepokelewa kutoka kwa Anas bin Maalik -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake-: Ya kwamba mtu mmoja aliingia msikitini siku ya Ijumaa kupitia mlango uliokuwa upande wa Dar Al-Kadhaa, na huku Mtume rehema na amani ziwe juu yake amesimama akihutubu, akamuelekea Mtume rehema na amani ziwe juu yake akiwa wima, kisha akasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, mali zimeteketea na njia zote zimekatika, muombe Mwenyezi Mungu atuletee mvua, akanyanyua Mtume rehema na amani ziwe juu yake mikono yake, kisha akasema: "Ewe Mola wetu tunyeshelezee, Ewe Mola wetu tunyeshelezee, Ewe Mola wetu tunyeshelezee". Akasema Anasi: Namuapa Mwenyezi Mungu, hatukua tukiona mbinguni mawingu wala dalili, na kati yetu na Mlima Sal'i hapakuwa na nyumba wala makazi, anasema: Likachomoza wingu nyuma yake mithili ya ngao, lilipofika kati kati ya mawingu likatanda kote, kisha mvua ikaanza kunyesha, namuapa Mwenyezi Mungu hutukuliona Jua kwa muda wa siku , kisha akaingia bwana mmoja kupitia mlango ule ule siku ya Ijumaa na Mtume rehema na amani ziwe juu yake akiwa wima akihutubia, akamuelekea akiwa kasimama akasema ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, mali zimeangamia, na njia zimekatika, muombe Mwenyezi Mungu aizuie kwetu mvua, anasema akanyanyua Mtume rehema na amani ziwe juu yake mikono yake, kisha akasema: "Ewe Mwenyezi Mungu inyeshe pembezoni mwetu na si juu yetu, ewe Mwenyezi Mungu inyeshe katika vichuguu na milima na ndani ya mabonde, na katika maoteo ya miti" Anasema: Mvua ikakata, na tukatoka tukitembea juani, amesema Shariki: Nilimuuliza Anasi, je ni yule yule mtu wa kwanza? Akasema: "Sijui".
Ufafanuzi
Aliingia bedui mmoja msikiti wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake siku ya Ijumaa kupitia mlango wa Magharibi upande wa nyumba ya Omari bin Khattwab radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, na Mtume rehema na amani ziwe juu yake akiwa kasimama anahutubia, yule bwana akamuelekea Mtume rehema na amani ziwe juu yake, na akasema, ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, wanyama wameangamia, na njia zote zimekatika kwa kufa mifugo inayobeba watu, au imedhoofika kutokana na njaa, basi muombe Mwenyezi Mungu atunyeshelezee mvua. Akanyanyua rehema na amani ziwe juu yake mikono yake, kisha akasema: Ewe Mwenyezi Mungu tunyeshelezee, Ewe Mwenyezi Mungu tunyeshelezee, Ewe Mwenyezi Mungu tunyeshelezee. Amesema Anasi bin Maliki radhi za Allah ziwe juu yake: Wallahi hatukua tukiona mbinguni hata kipande cha mawingu, na hapakuwa kati yetu sisi msikitini na Mlima Sal'i ulioko Magharibi mwa msikiti upande ambao hujia mawingu nyumba wala makazi yanayoweza kutuzuia kuona mawingu. Amesema Anasi radhi za Allah ziwe juu yake: Likatokeza nyuma yake wingu la duara mfano wa ngao nayo ni mviringo mdogo, lilipofika kati kati ya mawingu ya Madina likatanda, kisha mvua ikaanza kunyesha, na namuapa Mwenyezi Mungu, hatukuliona Jua tena kutokana na mvua mpaka Ijumaa iliyofuata, kiasi kwamba aliingia tena yule bwana kupitia mlango ule ule, huku rehema na amani ziwe juu yake akiwa kasimama anahutubia, akamuelekea akiwa wima, akasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, mali zimeangamia na njia zimekatika, basi muombe Mwenyezi Mungu aizuie mvua kwetu. Akasema: Akanyanyua rehema na amani ziwe juu yake mikono yake, kisha akasema: Ewe Mwenyezi Mungu igeuze mvua iende pembezoni mwetu ewe Mwenyezi Mungu ielekee katika sehemu zenye miinuko katika Ardhi kama kichuguu, na milima midogo, na ndani ya mabonde, na maoteo ya miti. Akasema Anasi: Yakakatika mawingu ya mvua, na tukatoka tukitembea juani.
Mafunzo
- Kufanya sababu za kutafuta riziki, kama kuomba dua, na kusafiri katika Ardhi, hakupingani na kumtegemea Mwenyezi Mungu Mtukufu.
- Sunna ya kuomba dua kwa kutumia dua hii ya Mtume kwa ajili ya kuomba mvua.
- Kufaa kuomba mvua ikate wakati mvua inapoleta madhara, na kuielekeza mvua iliyobakia katika miinuko na milima na ndani ya mabonde; kwa sababu ndio yanafaa zaidi kwa kilimo na machungo.
- Inafaa kuomba kuombewa dua kutoka kwa wale wanaodhaniwa kuwa wema na wachamungu katika watu waliohai tena walioko karibu yako, na huku ndiko kuomba kupitia mtu (kutawasali) kunakofaa, ama kuomba kupitia cheo cha yeyote katika viumbe, awe hai ama maiti, hili halifai; hili halifai; kwa sababu ni miongoni mwa njia za kuingia katika ushirikina.
- Sheria ya kung'ang'ania katika dua na kuirudiarudia.
- Kufaa kumsemesha hatibu siku ya Ijumaa kwa haja.
- Kumeonekana wazi uwezo wa Mwenyezi Mungu wa ajabu katika kuteremsha mvua na kuizuia.
- Hekima ya Mtume rehema na amani ziwe juu yake kwa kuomba dua kuzuia mvua ikiwa kuna madhara nakuleta ile isiyo na madhara.
- Sheria ya kuomba mvua katika hotuba.
- Kunyanyua mikono katika dua; kwa sababu ndani yake kuna maana ya unyenyekevu, na kutafuta maana ya kupewa ndani yake, na wamekubaliana wanachuoni juu ya kuinyanyua katika sehemu hii.
- Alama miongoni mwa alama za Mtume rehema na amani ziwe juu yake, inayoonyesha utume wake, kwani ilijibiwa dua yake kwa wakati huo huo, katika kuleta mvua na kuiondoa.
Ufafanuzi: العربية
دخل أعرابيٌّ مسجد النبي صلى الله عليه وسلم يوم جمعة من بابٍ غربي المسجد تجاه بيت عمر بن الخطاب رضي الله عنه، والنبي صلى الله عليه وسلم قائم يخطب، فاستقبل الرجل النبي صلى الله عليه وسلم، وقال: يا رسول الله، هلكت المواشي، وتقطعت السبل بموت البهائم التي تنقل الناس أو ضعفها من الجوع، فادع الله أن يسقينا المطر. فرفع صلى الله عليه وسلم يديه، ثم قال: اللهم اسقنا، اللهم اسقنا، اللهم اسقنا. قال أنس بن مالك رضي الله عنه: والله ما نرى في السماء ولا قطعة من غيم، وما بيننا في المسجد وبين جبل سلع غربي المسجد حيث يأتي من جهته السحاب من بيت ولا دار يحجبهم عن رؤيته. قال أنس رضي الله عنه: فطلعت من ورائه سحابة مستديرة مثل التُّرْس وهو الصَفِيْحة الصغيرة، فلما توسطت سماء المدينة انتشرت، ثم أمطرت، فوالله، ما رأينا الشمس من المطر حتى الجمعة الأخرى، حيث دخل ذلك الرجل من ذلك الباب، وهو صلى الله عليه وسلم قائم يخطب، فاستقبله قائمًا، فقال: يا رسول الله، هلكت الأموال، وانقطعت السبل، فادع الله يمسك المطر عنا. قال: فرفع صلى الله عليه وسلم يديه، ثم قال: اللهم اصرف المطر حوالينا ولا علينا، اللهم على ما ارتفع من الأرض كالتَّلِّ، والجبل الصغير، وبطون الأودية، ومنابت الشجر. قال أنس: فانقطعت السحابة الماطرة، وخرجنا نمشي في الشمس.
- فعل الأسباب لطلب الرزق، من الدعاء، والضرب في الأرض، لا ينافي التوكل على الله تعالى.
- استحباب الدعاء بهذا الدعاء النبوي لطلب الغيث.
- جواز الاستصحاء -طلب الصحو وتوقّف المطر- عند الضرر بالمطر، وخص بقاء المطر على الآكام والظراب وبطون الأودية؛ لأنها أوفق للزراعة والرعي.
- جواز طلب الدعاء ممَّن يظن فيهم الصلاح والتقى من الأحياء الحاضرين، وهذا التوسل الجائز، أما التوسل بجاه أحد من المخلوقين، حيًّا أو ميتًا، فهذا لا يجوز؛ لأنه من وسائل الشرك.
- مشروعية الإلحاح في الدعاء وتكراره.
- جواز تكليم الخطيب يوم الجمعة للحاجة.
- ظهور قدرة الله الباهرة في إنزال المطر وإمساكه.
- حكمة النبي صلى الله عليه وسلم بالدعاء بإمساك المطر عما فيه ضرر دون ما لا ضرر فيه.
- مشروعية الاستسقاء في الخطبة.
- رفع اليدين في الدعاء؛ لأن فيه معنى الافتقار، وتحرِّي معنى الإعطاء فيهما، وقد أجمع العلماء على رفعهما في هذا الموقف.
- آية من آيات النبي صلى الله عليه وسلم، الدالة على نبوته، فقد استجيب دعاؤه في الحال، في جلب المطر وفي رفعه.