Chanzo: HadeethEnc.com, Kiswahili v1.18.0
Matini ya Kiarabu
عَنْ أُمِّ عَطِيَّةَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا قَالَتْ: نُهِينَا عَنِ اتِّبَاعِ الجَنَائِزِ، وَلَمْ يُعْزَمْ عَلَيْنَا.
Tafsiri
Kutoka kwa Ummu Atwiya radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake amesema: Tulikatazwa kusindikiza jeneza, na hatukusisitiziwa katazo hilo.
Ufafanuzi
Anaeleza Ummu Atwiya Muanswari (mzaliwa wa Madina) radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, ya kwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake aliwakataza wanawake kusindikiza jeneza; na hii ni kwa sababu ya mitihani inayohofiwa juu yao, na uchache wa subira yao, kisha akaeleza radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake kuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake hakutilia mkazo katika katazo hili kama anavyofanya katika matakazo mengine.
Mafunzo
- Kuwakataza wanawake kusindikiza jeneza, nalo ni katazo la jumla la kulisindikiza, kuanzia linapoandaliwa na kuswaliwa, na mpaka makaburini linapozikwa.
- Sababu ya katazo, ni kwa sababu wanawake hawawezi kuhimili mfano wa sehemu kama hizi zenye kuhuzunisha, na mazingira yenye kuathiri; huenda kukaonekana kwao kulalamika, na kupaparika, mambo yanayokwenda kinyume na subira inayohitajika.
- Asili ya katazo huwa ni uharamu, isipokuwa Ummu Atwiya radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake alielewa kutokana na viashiria vya hali halisi kuwa katazo lao la kusindikiza jeneza si la mkazo uliosisitizwa, lakini zimekuja hadithi zilizoonyesha kutilia mkazo katika kusindikiza jeneza zaidi kuliko jinsi inavyoonyesha hadithi hii.
Ufafanuzi: العربية
تخبر أم عطية الأنصارية رضي الله عنها أن النبي صلى الله عليه وسلم نهى النساء عن المشي مع الجنائز؛ وذلك لما يُخشى في ذلك من الفتنة لهن وبهن، وقلّة صبرهن، ثم أخبرت رضي الله عنها أن النبي صلى الله عليه وسلم لم يؤكد في المنع كما يفعل في سائر المنهيات.
- نهي النساء عن اتباع الجنائز، وهو عام في اتباعها إلى حيث تجهز ويصلى عليها، وإلى المقبرة حيث تدفن.
- علة النهي أن النساء لا يُطِقْن مثل هذه المشاهد المحزنة والمواقف المؤثرة؛ فربما ظهر منهن من التسخط والجزع ما ينافي الصبر الواجب.
- الأصل في النهي التحريم إلا أن أم عطية رضي الله عنها فهمت من قرينة الحال أن نهيهن عن اتباع الجنائز ليس جازمًا مؤكَّدًا، لكن قد وردت أحاديث أدلّ على التشديد في اتباع الجنائز أكثر مما يدل عليه هذا الحديث.