Hadithi

Hili ni jiwe lililotupwa Motoni muda wa (miaka) sabini iliyopita, na sasa linaanguka Motoni mpaka litafika katika kina chake

Chanzo: HadeethEnc.com, Kiswahili v1.18.0

SahihiImepokelewa Imamu Muslim

Matini ya Kiarabu

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه قَالَ: كُنَّا مَعَ رَسُولِ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، إِذْ سَمِعَ وَجْبَةً، فَقَالَ النَّبِيُّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «تَدْرُونَ مَا هَذَا؟» قَالَ: قُلْنَا: اللهُ وَرَسُولُهُ أَعْلَمُ، قَالَ: «هَذَا حَجَرٌ رُمِيَ بِهِ فِي النَّارِ مُنْذُ سَبْعِينَ خَرِيفًا، فَهُوَ يَهْوِي فِي النَّارِ الْآنَ حَتَّى انْتَهَى إِلَى قَعْرِهَا».

Tafsiri

Kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Tulikuwa pamoja na Mtume rehema na amani ziwe juu yake ghafla akasikia kishindo, akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: “Je, mnajua ni nini hiki?” Akasema: Tukasema: Mwenyezi Mungu na Mtume wake wanajua zaidi, akasema: «Hili ni jiwe lililotupwa Motoni muda wa (miaka) sabini iliyopita, na sasa linaanguka Motoni mpaka litafika katika kina chake.

Ufafanuzi

Mtume rehema na amani ziwe juu yake alisikia sauti ya kushtua kama kuanguka kwa mwili, akawauliza Masahaba aliokuwa nao Mwenyezi Mungu awawie radhi kuhusu sauti hiyo, wakasema: Mwenyezi Mungu na Mtume wake ndio wajuzi zaidi. Akawaambia rehema na amani ziwe juu yake: Sauti hii mliyoisikia ni ya jiwe lililorushwa kutoka ukingo wa Jahannam miaka sabini iliyopita lilikuwa likiporomoka na kuanguka humo, hivi sasa mliposikia kishindo ndio limefika katika kina chake.

Mafunzo

  • Himizo la kujiandaa na siku ya mwisho kwa amali njema, na kutahadhari na Jahannam.
  • Ni sunna kuiegemeza elimu kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu katika yale ambayo mtu hana elimu nayo.
  • Mwalimu anatakiwa kuamsha hisia na umakini kwa wanafunzi kabla ya kuwaeleza; ili uwe ni msukumo wa wao kuelewa.
Ufafanuzi: العربية

سَمِعَ النبيُّ صلى الله عليه وسلم صوتًا مُزْعِجًا كسقوطِ جسمٍ من الأجسام، فسأل مَن عنده من الصحابة رضي الله عنهم عن ذلك الصوت، فقالوا: الله ورسوله أعلم. فقال لهم صلى الله عليه وسلم: إنَّ هذا الصوت الذي سمعتموه هو لحَجَرٍ رُمي به من شَفِيْر جهنم منذ سبعين عامًا، فهو يهوي ويسقط فيها، حتى انتهى إلى قَعرِها الآن حين سمعتم الصوت.

  • الحث على الاستعداد لليوم الآخر بالعمل الصالح، والتحذير من جهنم.
  • استحباب إسناد العلم إلى الله تعالى فيما لا علم للإنسان به.
  • إثارة المعلّم الاهتمام والانتباه قبل البيان؛ ليكون أدعى إلى الإفهام.

Mada

Ripoti kosa

Zaidi