Hadithi

Ewe Hakim, hakika mali hii ni kijani kibichi kitamu

Chanzo: HadeethEnc.com, Kiswahili v1.18.0

SahihiWamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake

Matini ya Kiarabu

عَنْ حَكِيمِ بْنِ حِزَامٍ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ قَالَ: سَأَلْتُ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فَأَعْطَانِي، ثُمَّ سَأَلْتُهُ فَأَعْطَانِي، ثُمَّ قَالَ لِي: «يَا حَكِيمُ، إِنَّ هَذَا المَالَ خَضِرٌ حُلْوٌ، فَمَنْ أَخَذَهُ بِسَخَاوَةِ نَفْسٍ، بُورِكَ لَهُ فِيهِ، وَمَنْ أَخَذَهُ بِإِشْرَافِ نَفْسٍ لَمْ يُبَارَكْ لَهُ فِيهِ، وَكَانَ كَالَّذِي يَأْكُلُ وَلاَ يَشْبَعُ، وَاليَدُ العُلْيَا خَيْرٌ مِنَ اليَدِ السُّفْلَى»، قَالَ حَكِيمٌ: فَقُلْتُ: يَا رَسُولَ اللَّهِ، وَالَّذِي بَعَثَكَ بِالحَقِّ لاَ أَرْزَأُ أَحَدًا بَعْدَكَ شَيْئًا حَتَّى أُفَارِقَ الدُّنْيَا، فَكَانَ أَبُو بَكْرٍ يَدْعُو حَكِيمًا لِيُعْطِيَهُ العَطَاءَ، فَيَأْبَى أَنْ يَقْبَلَ مِنْهُ شَيْئًا، ثُمَّ إِنَّ عُمَرَ دَعَاهُ لِيُعْطِيَهُ، فَيَأْبَى أَنْ يَقْبَلَهُ، فَقَالَ: يَا مَعْشَرَ المُسْلِمِينَ، إِنِّي أَعْرِضُ عَلَيْهِ حَقَّهُ الَّذِي قَسَمَ اللَّهُ لَهُ مِنْ هَذَا الفَيْءِ، فَيَأْبَى أَنْ يَأْخُذَهُ. فَلَمْ يَرْزَأْ حَكِيمٌ أَحَدًا مِنَ النَّاسِ بَعْدَ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ حَتَّى تُوُفِّيَ رَحِمَهُ اللَّهُ.

Tafsiri

Imepokelewa kutoka kwa Hakiim Bin Hizaam radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake amesema: Nilimuomba Mtume rehema na amani ziwe juu yake akanipa, kisha nikamuomba tena akanipa, kisha akasema kuniambia: "Ewe Hakim, hakika mali hii ni kijani kibichi kitamu, atakayeichukua kwa ukarimu wa nafsi, basi atabarikiwa ndani yake, na atakayeichukua kwa kujikweza hatobarikiwa ndani yake, na atakuwa sawa na yule anayekula wala hashibi, na mkono wa juu ni bora kuliko mkono wa chini", Hakim anasema: Nikasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, ninamuapa yule aliyekutuma kwa haki, sitompunguzia yeyote mali yake baada yako kamwe mpaka ntakapoondoka duniani, akawa Abubakari akimuita Hakim ili ampe chochote, akawa anakataa kupokea chochote kutoka kwake, kisha Omari alimuita ili ampe, akakataa kupokea, akasema: Enyi Waislamu, hakika mimi ninamletea haki yake ambayo Mwenyezi Mungu kamgawia katika ngawira, anakataa kuichukua. Hakim hakumuomba tena mtu yeyote baada ya Mtume rehema na amani ziwe juu yake, mpaka alipofariki Mwenyezi Mungu amrehe

Ufafanuzi

Hakim bin Hizam alimuomba Mtume rehema na amani ziwe juu yake mahitaji ya kidunia akampatia, kisha akamuomba mara nyingine akampatia, kisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake akasema kumwambia: Ewe Hakim, hakika mali hii huvutia na hupendwa sana, atakayeipata bila kuomba na akaichukua pasina kujikweza na pupa, basi atabarikiwa ndani yake, na atakayeichukua kwa pupa na tamaa ya nafsi basi hatobarikiwa ndani yake, na atakuwa kama yule anayekula wala hashibi, na mkono wa juu wenye kutoa ni bora mbele ya Mwenyezi Mungu kuliko mkono wa chini unaoomba, anasema Hakim: Nikasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, namuapa yule aliyekutuma kwa haki, sitopunguza mali ya yeyote kwa kumuomba chochote baada yako mpaka niondoke duniani. Basi akawa khalifa wa Mtume wa Mwenyezi Mungu Abubakari radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, akimuita Hakim ili ampatie sadaka, anakataa kupokea chochote, kisha kiongozi wa Waumini Omari radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake alimuita ili ampatie mali, akakataa kuchukua, basi Omari akasema: Enyi Waislamu, hakika mimi nimemletea haki yake aliyomgawia Mwenyezi Mungu kutoka katika mali ya Ngawira waliyoipata Waislamu kutoka kwa Makafiri pasina vita wala mapigano, akakataa kuichukua, Hakim hakupunguza mali ya yeyote kwa kumuomba baada ya Mtume rehema na amani ziwe juu yake, mpaka alipofariki radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake.

Mafunzo

  • Kuchukua mali na kuikusanya kwa njia za kisheria hakupingani na kuiepuka dunia; kwa sababu kuipa mgongo dunia ni ukwasi wa nafsi na moyo kutofungamana na mali.
  • Kumebainishwa ukubwa wa ukarimu wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake, na kwamba alikuwa akitoa utoaji wa mtu asiyeogopa umasikini kamwe!
  • Kutoa nasaha na kupupia katika kuwanufaisha ndugu, wakati wa kutoa msaada; kwa sababu wakati huo nafsi huwa imejiandaa kupokea maneno mazuri.
  • Kujizuia kuwaomba watu, na kuchukia kufanya hivyo, hasa hasa panapokuwa hakuna haja.
  • Hapa kuna ubaya wa kupupia mali na kuombaomba sana.
  • Muombaji atakapolazimisha kuomba, hakuna tatizo kumnyima na kumfelisha, na kumpa nasaha, na kumuamrisha kujizuia kuomba, na kuacha pupa ya kutaka kuchukua.
  • Hastahiki yeyote kuchukua chochote kutoka katika Hazina ya mali za Waislamu isipokuwa baada ya kupepwa na kiongozi, na ama kabla kuwagawanywa kwa ngawira, hastahiki pia kufanya hivyo.
  • Inafaa kuomba kukiwa na haja.
  • Amesema bin Hajari: Ndani ya kisa hiki nikuwa, inatakiwa kwa kiongozi kutombainishia muombaji madhara yaliyoko katika uombaji isipokuwa baada ya kukidhi haja yake ili mawaidha yake yafike mahala pake, ili asifikirie kuwa huenda hiyo ndio sababu ya kumnyima shida yake.
  • Ubora wa Hakim radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na kushikamana kwake na ahadi aliyomuahidi Mwenyezi Mungu na Mtume wa Mwenyezi Mungu rehema na amani ziwe juu yake.
  • Amesema Is-haka bin Rahawaihi: Alifariki Hakim radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake ulipofikia wakati wa kufa, na hakika alikuwa amekwisha kuwa tajiri mwenye mali nyingi kuliko Makuraishi wote.
Ufafanuzi: العربية

سأل حكيم بن حزام رضي الله عنه النبي صلى الله عليه وسلم من متاع الدنيا فأعطاه، ثم سأله أخرى فأعطاه، ثم قال له النبي صلى الله عليه وسلم: يا حكيم، إن هذا المال مُشتهى مرغوب فيه، فمن جاءه بغير مسألة وأخذه بغير شَرَهِ نَفْسٍ وإلحاح، بورك له فيه، ومن أخذه بتطلع نفس وطمع لم يبارك له فيه، وكان كالذي يأكل ولا يشبع، واليد العليا المنفقة خير عند الله من اليد السفلى السائلة، قال حكيم: فقلت: يا رسول الله، والذي بعثك بالحق لا أنقص مال أحدٍ بالطلب منه بعدك حتى أفارق الدنيا. فكان خليفة رسول الله أبو بكر رضي الله عنه يدعو حكيمًا ليعطيه العطاء، فيأبى أن يقبل منه شيئًا، ثم إن أمير المؤمنين عمر رضي الله عنه دعاه ليعطيه، فيأبى أن يقبله، فقال عمر: يا معشر المسلمين، إني أعرض عليه حقه الذي قسم الله له من مال الفيء الذي حصل للمسلمين من الكفار من غير حرب ولا جهاد، فيأبى أن يأخذه، فلم ينقص حكيم مال أحدٍ بالطلب منه بعد النبي صلى الله عليه وسلم حتى توفي رضي الله عنه.

  • أخذ المال وجمعه بطرق مشروعة لا يتعارض مع الزهد في الدنيا؛ لأن الزهد سَخاوة النفس وعدم تعلق القلب بالمال.
  • بيان عظيم كرم النبي صلى الله عليه وسلم، وأنه يعطي عطاء من لا يخشى الفقر أبدًا.
  • بذل النصيحة والحرص على نفع الإخوان عند تقديم العون؛ لأن النفس تكون مهيأة للانتفاع بالكلم الطيب.
  • التعفف عن سؤال الناس والتنفير عنه ولا سيما لغير حاجة.
  • فيه ذم الحرص على المال وكثرة السؤال.
  • السائل إذا ألَحَّ بالسؤال، فلا بأس برده وتخييبه وموعظته، وأمره بالتعفف وترك الحرص على الأخذ.
  • لا يستحق أحد أخذ شيء من بيت المال إلا بعد أن يعطيه الإمام إياه، وأما قبل قسمة الغنيمة فليس ذلك مستحقًا له.
  • جواز السؤال للحاجة.
  • قال ابن حجر: فيه أنه ينبغي للإمام أن لا يبين للطالب ما في مسألته من المفسدة إلا بعد قضاء حاجته لتقع موعظته له الموقع، لئلا يتخيل أن ذلك سبب لمنعه من حاجته.
  • فضيلة حكيم رضي الله عنه والتزامه العهد مع الله ومع رسول الله صلى الله عليه وسلم.
  • قال إسحاق بن راهويه: مات حكيم رضي الله عنه حين مات، وإنه لمن أكثر قريش مالًا.

Mada

Ripoti kosa

Zaidi