Hadithi

Chelewesheni kula daku, hakika katika kuchelewesha kula daku kuna baraka

Chanzo: HadeethEnc.com, Kiswahili v1.18.0

SahihiWamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake

Matini ya Kiarabu

عن أَنَسِ بْنِ مَالِكٍ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ قَالَ: قَالَ النَّبِيُّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «تَسَحَّرُوا، فَإِنَّ فِي السَّحُورِ بَرَكَةً».

Tafsiri

Imepokelewa kutoka kwa Anasi bin Maliki -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-: "Chelewesheni kula daku, hakika katika kuchelewesha kula daku kuna baraka".

Ufafanuzi

Amehimiza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kula daku, nako ni kula mwisho wa usiku ili kujiandaa kwa ajili ya swaumu; kwa sababu ndani yake kuna baraka, na kheri nyingi, yakiwemo malipo na thawabu, na kusimama katika wakati wa mwisho kwa ajili ya kuomba dua, na kupata nguvu kwa ajili ya swaumu, na kupata uchangamfu kwa ajili yake, na kupunguza uzito wake.

Mafunzo

  • Sunna ya kula daku na kutekeleza amri ya sheria kwa kufanya hivyo.
  • Amesema bin Hajari katika kitabu Fat-hulbaari: Baraka katika daku zinapatikana kwa namna nyingi: Nayo ni kufuata sunna na kwenda kinyume na Mayahudi na Wakristo, na kupata nguvu kutokana na daku kwa ajili ya ibada, na kuongeza uchangamfu, na kuondoa tabia mbaya inayosababishwa na njaa, na kuwa sababu ya kutoa sadaka kwa mwenye kuomba kwa wakati huo, au akajumuika pamoja naye katika chakula, na ni sababu ya kufanya dhikri na dua katika wakati ambao kuna matarajio makubwa ya kujibiwa, na kuipata nia ya kufunga kwa yule aliyejisahau kabla ya kulala.
  • Uzuri wa mafundisho ya Mtume rehema na amani ziwe juu yake, kiasi kwamba alikuwa akioanisha hukumu kwa hukumu; ili mioyo ya watu ikunjuke, na ujulikane utukufu wa sheria.
  • Amesema bin Hajari: Daku inapatikana kwa chochote kidogo atakachokula mtu, katika vyakula au vinywaji.
Ufafanuzi: العربية

حَثَّ النبيُّ صلى الله عليه وسلم على السَّحُور وهو الأكل آخِر الليل استعدادًا للصيام؛ لأن فيه (بركة) خيرًا كثيرًا مِن الأجر والثواب، والقيام في وقت آخر الليل للدعاء، والتَّقَوِّي على الصوم، والتَّنَشُّط له، وتخفيف مشقَّته.

  • استحباب السَّحُورِ وامتثال الأمر الشرعي بفعله.
  • قال ابن حجر في فتح الباري: البركة في السحور تحصل بجهات متعددة، وهي اتباع السنة، ومخالفة أهل الكتاب، والتقوِّي به على العبادة، والزيادة في النشاط، ومدافعة سوء الخُلُق الذي يُثيره الجوع، والتسبُّب بالصدقة على مَن يسأل إذ ذاك أو يجتمع معه على الأكل، والتسبب للذِّكْر والدعاء وقت مظنة الإجابة، وتَدَارُك نية الصوم لمن أغفلها قبل أن ينام.
  • حسن تعليم النبي صلى الله عليه وسلم حيث يَقْرِن الحُكْم بالحكمة؛ لينشرح به الصدر، ويُعرف به سموُّ الشريعة.
  • قال ابن حجر: يحصل السحور بأقل ما يتناوله المرء من مأكول ومشروب.

Mada

Ripoti kosa

Zaidi