Hadithi

Hakika Allah na Mtume wake ameharamisha kuuza pombe, na mzoga na nguruwe na masanamu

Chanzo: HadeethEnc.com, Kiswahili v1.18.0

SahihiWamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake

Matini ya Kiarabu

عَنْ جَابِرِ بْنِ عَبْدِ اللَّهِ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُمَا أَنَّهُ سَمِعَ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، يَقُولُ عَامَ الفَتْحِ وَهُوَ بِمَكَّةَ: «إِنَّ اللَّهَ وَرَسُولَهُ حَرَّمَ بَيْعَ الخَمْرِ، وَالمَيْتَةِ وَالخِنْزِيرِ وَالأَصْنَامِ»، فَقِيلَ: يَا رَسُولَ اللَّهِ، أَرَأَيْتَ شُحُومَ المَيْتَةِ، فَإِنَّهَا يُطْلَى بِهَا السُّفُنُ، وَيُدْهَنُ بِهَا الجُلُودُ، وَيَسْتَصْبِحُ بِهَا النَّاسُ؟ فَقَالَ: «لاَ، هُوَ حَرَامٌ»، ثُمَّ قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ عِنْدَ ذَلِكَ: «قَاتَلَ اللَّهُ اليَهُودَ إِنَّ اللَّهَ لَمَّا حَرَّمَ شُحُومَهَا جَمَلُوهُ، ثُمَّ بَاعُوهُ، فَأَكَلُوا ثَمَنَهُ».

Tafsiri

Kutoka kwa Jabiri bin Abdillah radhi za Allah ziwe juu yao na baba yake, yakwamba yeye alimsikia Mtume rehema na amani ziwe juu yake, akisema siku ya ufunguzi wa mji wa Makka, akiwa Makka: "Hakika Allah na Mtume wake ameharamisha kuuza pombe, na mzoga na nguruwe na masanamu", Wakasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, wasemaje kuhusu samli (mafuta ya wanyama), kwani hutumika kupaka boti, na hupakwa ngozi, na watu huyatumia kuwasha taa? Akasema: "Hapana, hayo ni haramu", kisha baada ya hapo akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Mwenyezi Mungu awalaani Mayahudi, kwani Mwenyezi Mungu alipowaharamishia samli (mafuta ya wanyama) waliyayeyusha, kisha wakayauza, na wakala thamani yake".

Ufafanuzi

Jabiri bin Abdillah Mwenyezi Mungu awe radhi nao wote wawili, alimsikia Mtume rehema na amani ziwe juu yake akisema katika mwaka wa ufunguzi akiwa Makka: Hakika Mwenyezi Mungu na Mtume wake amekataza kuuza pombe, na mzoga na nguruwe na masanamu, wakasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, je inajuzu kwetu kuuza mafuta ya wanyama waliokufa? Kwa sababu yanatumika kupaka boti (Mitumbwi), na ngozi na watu huwasha taa zao kwayo. Akasema: Hapana, kuyauza ni haramu, kisha akasema: Mwenyezi Mungu amewalaani Mayahudi, Mwenyezi Mungu alipowaharamishia mafuta ya wanyama, waliyayeyusha, kisha wakayauza na kula thamani yake.

Mafunzo

  • Amesema Imam Nawawi: Mzoga na pombe na nguruwe: Wamekubaliana waislamu wote kuwa ni haramu kuuza chochote katika hivi.
  • Amesema Kadhi: Hadithi hii inamaanisha kuwa kila kisichohalali kukila na kunufaika nacho basi haifai kukiuza, na wala si halali kula thamani yake, kama ilivyo katika mafuta yaliyotajwa katika hadihi
  • Amesema bin Hajari: Mlolongo wa hadithi inaonesha kuwa ibara ya mwanzo inaguvu zaidi kwa makusudio ya kuwa kauli yake: "Ni haramu" Yaani: Kuuza na si kunufaika.
  • Kila ujanja unaotumika kuhalalisha haramu basi ni batili.
  • Amesema Imam Nawawi: Wamesema wanachuoni: Na katika ujumla wa uharamu wa kuuza mzoga nikuwa ni haramu kuuza maiti ya kafiri tutakapomuuwa na makafiri wakaomba kumnunua, au kutoa fidia, na imekuja katika hadithi: Yakwamba Naufal bin Abdillah Al-Makhazuumi waislamu walimuua siku ya vita vya Khandaq, makafiri wakatoa Dirham elfu kumi ili kupewa mwili wake kutoka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake, basi hakuzichukua, na akawapa bure.
Ufafanuzi: العربية

سَمِعَ جابرُ بن عبدِ الله رضي الله عنهما النبيَّ صلى الله عليه وسلم يقول عامَ الفَتْح، وهو بمكة: إن الله ورسوله حَرَّم بيعَ الخمر والميتة والخنزير والأصنام، فقيل: يا رسول الله، هل يَحِلُّ أنْ نبيعَ شحومَ الميتة؟ لأنها يُطْلَى بها السُّفُن، ويُدهَن بها الجلود، ويُوقِد بها الناسُ سُرُجَهم، فقال: لا، بيعُها حرام، ثم قال صلى الله عليه وسلم عند ذلك: أَهْلَكَ اللهُ اليهودَ ولعنَهم؛ إن الله لمّا حرّم عليهم شحوم البهائم أذابوها، ثم باعوا دُهنَها فأكلوا ثَمَنَه.

  • قال النووي: الميتة والخمر والخنزير: أجمع المسلمون على تحريم بيع كلِّ واحدٍ منها.
  • قال القاضي: تَضَمَّنَ هذا الحديث أن ما لا يَحِلُّ أكلُه والانتفاع به لا يجوز بيعه، ولا يحل أكل ثمنه، كما في الشحوم المذكورة في الحديث.
  • قال ابن حجر: وسياقُه مُشْعِرٌ بِقُوَّة ما أوّله الأكثر أن المراد بقوله: "هو حرام" البيع لا الانتفاع.
  • كلُّ حِيْلةٍ يُتَوَصَّل بها إلى تحليل مُحَرَّمٍ فهي باطلة.
  • قال النووي: قال العلماء: وفي عموم تحريم بيع الميتة أنه يحرم بيع جُثَّة الكافر إذا قتلناه وطَلَبَ الكفّارُ شراءَه، أو دَفْع عِوَضٍ عنه، وقد جاء في الحديث: أنّ نوفل بن عبد الله المخزومي قتله المسلمون يوم الخندق، فبذل الكفار في جسده عشرة آلاف درهم للنبي صلى الله عليه وسلم فلم يأخذْها، ودَفَعَه إليهم.

Mada

Ripoti kosa

Zaidi