Hadithi

Hebu nielezeni lau kama Mto ungelikua mlangoni kwa mmoja wenu akioga humo kila siku mara tano, unasemaje kuhusu hilo, kunaweza kubaki na uchafu katika mwili wake?

Chanzo: HadeethEnc.com, Kiswahili v1.18.0

SahihiWamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake

Matini ya Kiarabu

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه أَنَّهُ سَمِعَ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَقُولُ: «أَرَأَيْتُمْ لَوْ أَنَّ نَهَرًا بِبَابِ أَحَدِكُمْ يَغْتَسِلُ فِيهِ كُلَّ يَوْمٍ خَمْسًا، مَا تَقُولُ ذَلِكَ يُبْقِي مِنْ دَرَنِهِ؟» قَالُوا: لَا يُبْقِي مِنْ دَرَنِهِ شَيْئًا، قَالَ: «فَذَلِكَ مِثْلُ الصَّلَوَاتِ الخَمْسِ، يَمْحُو اللَّهُ بِهِ الخَطَايَا».

Tafsiri

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- yakuwa yeye alimsikia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akisema: "Hebu nielezeni lau kama Mto ungelikua mlangoni kwa mmoja wenu akioga humo kila siku mara tano, unasemaje kuhusu hilo, kunaweza kubaki na uchafu katika mwili wake?" Wakasema: Hautobakiza uchafu wowote, akasema: " Huu ndio mfano wa swala tano, Mwenyezi Mungu hufuta makosa kwa swala hizo".

Ufafanuzi

Amefananisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- swala tano za kila usiku na mchana katika kuondoa kwake na kufuta kwake madhambi madogo ni sawa na Mto ulioko mlangoni kwa mtu akioga humo kila siku mara tano, hautobakiza chochote katika uchafu wake.

Mafunzo

  • Fadhila hizi ni maalum kwa kufuta madhambi madogo, ama makubwa hayo ni lazima kuwe na toba.
  • Fadhila za kutekeleza swala tano na kuzihifadhi kwa sharti zake na nguzo zake na wajibu wake na sunna zake.
Ufafanuzi: العربية

شَبَّهَ النبيُّ صلى الله عليه وسلم الصلواتِ الخمس في كلِّ يومٍ وليلةٍ في إزالتِها وتكفيرِها لصغائر الذنوب والخطايا بِنَهْرٍ على بابِ الإنسان يَغتسلُ منه كلَّ يومٍ خمسَ مرات، فلا يبقى مِن دَرَنِهِ ووَسَخِهِ شيءٌ.

  • هذا الفضلُ خاصٌّ بتكفير الصغائر، أما الكبائر فلا بُد من التوبة منها.
  • فضل أداء الصلوات الخمس والمحافظة عليها بشروطِها وأركانِها وواجباتِها وسننِها.

Mada

Ripoti kosa

Zaidi