Hadithi

Kumtukana Muislamu ni ufasiki (kutoka nje ya mipaka), na kupigana naye ni ukafiri

Chanzo: HadeethEnc.com, Kiswahili v1.18.0

SahihiWamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake

Matini ya Kiarabu

عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بنِ مَسْعُودٍ رضي الله عنه أَنَّ النَّبِيَّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: «سِبَابُ المُسْلِمِ فُسُوقٌ، وَقِتَالُهُ كُفْرٌ».

Tafsiri

Kutoka kwa Abdallah bin Masoud -radhi za Allah ziwe juu yake- yakwamba Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Kumtukana Muislamu ni ufasiki (kutoka nje ya mipaka), na kupigana naye ni ukafiri."

Ufafanuzi

Mtume rehema na amani ziwe juu yake amemkataza muislamu kumshutumu na kumtukana ndugu yake muislamu, nakuwa hilo ni katika ufasiki ambao ni kutoka nje ya utiifu wa Mwenyezi Mungu na Mtume wake rehema na amani ziwe juu yake, nakuwa muislamu kukabiliana na ndugu yake muislamu ni katika matendo ya ukafiri, lakini ni ukafiri mdogo.

Mafunzo

  • Ulazima wa kuheshimu heshima ya muislamu na damu yake.
  • Ukubwa wa hatima ya kumtukana muislamu pasina haki; mwenye kutukana pasina haki ni muovu.
  • Kumtukana muislamu na kupigana naye kunadhoofisha imani na kuipunguza.
  • Baadhi ya matendo huitwa ukafiri; hata yasipofika katika ukafiri mkubwa wenye kumtoa mtu katika Uislamu.
  • Makusudio ya ukafiri hapa ni ukafiri mdogo usiomtoa mtu katika Uislamu kwa makubaliano ya watu wa sunna; kwa sababu Mwenyezi Mungu Mtukufu ameuthibitisha udugu wa kiimani kwa waumini wakati wa kupigana kwao, akasema Mtukufu: "Na ikiwa makundi mawili ya waumini yatapigana basi wasuluhisheni baina yao" mpaka katika kauli yake: "Hakika waumini wote ni ndugu".
Ufafanuzi: العربية

نَهَى النبيُّ صلى الله عليه وسلم المُسلمَ أنْ يَشْتُمَ ويَسُبَّ أخاه المسلمَ، وأنَّ ذلك من الفسوق وهو الخروج عن طاعة الله ورسوله صلى الله عليه وسلم، وأنَّ مُقاتَلَةَ المسلمِ أخاه المسلمَ من الأعمال الكُفْرِيّة، لكنه كُفْرٌ أصغر.

  • وجوب احترام عِرْضِ المسلم ودمِهِ.
  • عِظَم مآل سابِّ المسلم بغير حق؛ فالسابُّ بغير حق فاسق.
  • سباب المسلم وقتاله يُضْعِفُ الإيمان وينقصه.
  • بعض الأعمال تُسمى كُفْرًا؛ وإنْ لم تَصِل إلى الكفر الأكبر المخرج عن مِلَّة الإسلام.
  • المراد بالكفر هنا الكفر الأصغر الذي لا يُخْرِج مِن المِلّة باتفاق أهل السنة؛ لأن الله عز وجل أثبت أُخُوَّةَ الإيمان للمؤمنين حال اقتتالِهم ونزاعِهم، فقال تعالى: (وَإِنْ طَائِفَتَانِ مِنَ الْمُؤْمِنِينَ اقْتَتَلُوا فَأَصْلِحُوا بَيْنَهُمَا) إلى قوله: ( إِنَّمَا الْمُؤْمِنُونَ إِخْوَةٌ).

Mada

Ripoti kosa

Zaidi