Hadithi

Sema: Ewe Mwenyezi Mungu niongoze na unisimamie, na kumbuka kwa uongofu ni kuongoka kwako njia, na kusimamiwa ni kusimamiwa kupatia (katika kila jambo lako mithili ya) mshale

Chanzo: HadeethEnc.com, Kiswahili v1.18.0

SahihiImepokelewa Imamu Muslim

Matini ya Kiarabu

عَنْ عَلِيٍّ رضي الله عنه قَالَ: قَالَ لِي رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «قُلِ اللهُمَّ اهْدِنِي وَسَدِّدْنِي، وَاذْكُرْ بِالْهُدَى هِدَايَتَكَ الطَّرِيقَ، وَالسَّدَادِ سَدَادَ السَّهْمِ».

Tafsiri

Kutoka kwa Ally -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Alisema kuniambia mimi Mtume -rehema na amani ziwe juu yake: "Sema: Ewe Mwenyezi Mungu niongoze na unisimamie, na kumbuka kwa uongofu ni kuongoka kwako njia, na kusimamiwa ni kusimamiwa kupatia (katika kila jambo lako mithili ya) mshale".

Ufafanuzi

Mtume rehema na amani ziwe juu yake alimuamrisha Ally bin Abii Twalib radhi za Allah ziwe juu yake amtake Mwenyezi Mungu na amuombe na aseme: "Ewe Mwenyezi Mungu niongoze" na unielekeze na unijulishe "na unisimamie" na uniafikishe, na unifanye kuwa na msimamo katika mambo yangu yote. Uongofu: Ni kuijua haki kwa ujumla na kwa ufafanuzi, na kuwezeshwa kuifuata kwa wazi na kwa siri. Na kusimamiwa: Ni kuwezeshwa na kuwa na msimamo katika mambo yote katika yale ya kweli juu ya haki, nayo ni njia iliyonyooka katika kauli na vitendo na itikadi. Na hii ni kwa sababu jambo lisiloonekana hueleweka wazi kupitia jambo linaloonekana; Hivyo kumbuka unapokuwa unaomba dua hii kuwa: "Uongofu: Ni kuongozwa njia" Hivyo, hudhurisha moyo wako nawe ukiwa unaomba uongofu mfano wa uongofu wa aliyesafarini, kwani huwa hatoki nje ya njia si kulia wala kushoto; na hii ni ili asalimike na kupotea, na kwa hilo anapata usalama, na atafika haraka katika lengo lake. "Na kuafikishwa nakupatia: Ni kupatia kwa mshale" Wewe chunguza wakati wa kulenga kwako mshale katika uharaka wa kufika kwake na kukipata ulichokusudia kukipiga, mrusha mishale anaporusha katika lengo basi huhakikisha ameulenga vizuri mshale katika kile alichokikusudia, hivyo hivyo na wewe unamuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu kuwa yote unayoyakusudia basi yawe katika mfano wa mshale; utakuwa katika kuomba kwako umeomba kiwango cha juu zaidi cha uongofu, na mwisho wa kusimamiwa. Vuta picha ya maana hii kwa moyo wako ili umuombe usimamizi Mwenyezi Mungu na kupatia katika mambo yako, ili yale unayoyanuia katika hilo yawe katika mfano wa namna unavyofanya mshale.

Mafunzo

  • Muombaji anatakiwa apupie kupatia katika amali yake na kuinyoosha kwa kushikamana na sunna na kutakasa nia.
  • Sunna ya kuomba dua kwa maneno haya yaliyokusanya kuwezeshwa na kusimamiwa katika mambo.
  • Ni wajibu kwa mja kutaka msaada kutoka kwa Mwenyezi Mungu katika mambo yake yote.
  • Kupiga mifano wakati wa kufundisha.
  • Kukusanya kati ya kutaka uongofu na kutengenezewa na hali, na kudumu juu yake na kutopotoka hata chembe ndogo na kutengemaa kwa mafikio, hivyo kauli yake: "Niongoze" Ili nitembee juu ya njia ya uongofu, na kauli yake: "Na unisimamie" ni katika kupatia na kutopotoka wakati wa uongofu uliomfika.
  • Muombaji anatakiwa aitilie maanani dua yake, na avute picha ya maana ya maombi yake ndani ya moyo wake; kwani hili huleta msukumo mkubwa wa kujibiwa dua.
Ufafanuzi: العربية

أَمَرَ النبيُّ صلى الله عليه وسلم عليَّ بن أبي طالب رضي الله عنه أنْ يَدعوَ اللهَ ويسألَه فيقول: (اللهم اهدني) وأرشدني ودلني (وسددني) ووفقني، واجعلني مستقيمًا في جميع أموري. فالهُدَى: هو مَعرفةُ الحقِّ تفصيلًا وإجمالًا، والتوفيق لاتّباعه ظاهرًا وباطنًا. والسّداد: هو التوفيق والاستقامة في جميع الأمور بما يكون صوابًا على الحق، وهو الطريق المستقيم في القول والفعل والاعتقاد. ولأن الأمر المعنوي يَتَّضِح بالمَحْسُوس؛ تَذَكَّر وأنت تدعو هذا الدعاء بأنَّ: (الهدى: هدايتك الطريق) فأحضِر بقلبِك وأنت تسأل هدايةً كهداية مَن سافر، فإنه لا يَنحرِف عن الطريق يَمْنة أو يسرة؛ وذلك لِيَسْلَمَ مِن الضياع، وبذلك يَنال السلامة، ويَصِل إلى غايته سريعًا. (والسداد: سداد السهم) فأنت تلاحظ عند تَسْديدِك السَّهْمَ في سرعة وصوله وإصابته للهدف، فالرامي إذا رمى غرضًا سدَّد بالسهم نحو الغَرَض، فكذلك تسأل الله تعالى أنَّ ما تَنويه من السداد على شاكلة السهم؛ فتكون في سؤالك طالبًا غاية الهدى، ونهاية السداد. فأحضر هذا المعنى بقلبك حتى تسأل الله السداد ليكون ما تنويه من ذلك على مشاكلة ما تستعمله من الرمي.

  • الداعي ينبغي أن يَحرِص على تسديد عملِه وتقويمه بلزوم السنة وإخلاص النية.
  • استحباب الدعاء بهذه الكلمات الجامعة للتوفيق والسداد.
  • ينبغي على العبد الاستعانة بالله تعالى في جميع أموره.
  • ضرْب المثال في مقام التعليم.
  • الجمع بين طلب الهداية وصلاح الحال، والاستمرار عليها وعدم الزيغ عنها طرفة عين وصلاح المآل، فقوله: "اهدني" بأن يكون سائرًا على دَرْبِ الهداية، وقوله: "وسددني": من الإصابة وعدم الزيغ عند الهداية التي اعتلاها.
  • الداعي ينبغي له أن يهتمَّ بدعائه، ويستحضر معاني دعواته في قلبه؛ فهذا أَدْعَى للقبول.

Mada

Ripoti kosa

Zaidi