Hadithi

Hana swaumu atakayefunga milele, na funga ya siku tatu ni sawa na kufunga mwaka mzima

Chanzo: HadeethEnc.com, Kiswahili v1.18.0

SahihiWamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake

Matini ya Kiarabu

عَنْ عَبْدَ اللَّهِ بْنِ عَمْرِو بْنِ العَاصِ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُمَا، قَالَ: قَالَ النَّبِيُّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «إِنَّكَ لَتَصُومُ الدَّهْرَ، وَتَقُومُ اللَّيْلَ؟»، فَقُلْتُ: نَعَمْ، قَالَ: «إِنَّكَ إِذَا فَعَلْتَ ذَلِكَ هَجَمَتْ لَهُ العَيْنُ، وَنَفِهَتْ لَهُ النَّفْسُ، لاَ صَامَ مَنْ صَامَ الدَّهْرَ، صَوْمُ ثَلاَثَةِ أَيَّامٍ صَوْمُ الدَّهْرِ كُلِّهِ»، قُلْتُ: فَإِنِّي أُطِيقُ أَكْثَرَ مِنْ ذَلِكَ، قَالَ: «فَصُمْ صَوْمَ دَاوُدَ عَلَيْهِ السَّلاَمُ، كَانَ يَصُومُ يَوْمًا وَيُفْطِرُ يَوْمًا، وَلاَ يَفِرُّ إِذَا لاَقَى».

Tafsiri

Imepokelewa kutoka kwa Abdullahi bin Amru -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake-amesema: Amesema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-: "Hakika wewe unafunga milele, na unasimama usiku?", Nikasema: Ndiyo, akasema: "Hakika wewe ukifanya hivyo macho yatadhoofu, na nafsi itanyongeka, Hana swaumu atakayefunga milele, na funga ya siku tatu ni sawa na kufunga mwaka mzima", Nikasema: Hakika mimi ninaweza zaidi ya hapo, akasema: "Basi funga swaumu Daudi amani iwe juu yake, alikuwa akifunga siku moja na anafungua siku moja, na wala hakimbii anapokutana (na adui)".

Ufafanuzi

Ilimfikia habari Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa Abdallah bin Amri radhi za Allah ziwe juu yake alikuwa akiunganisha swaumu na wala hafungui mwaka mzima, na anaswali usiku mzima wala halali, akamkataza hilo na akamwambia: Funga na ufungue, na simama na ulale. Na akamkataza kuunganisha swaumu na kusimama usiku mzima, na akamwambia: Hakika wewe ukifanya hivyo macho yako yatadhoofika na yatabonyea, na itanyong'onyea kwa hilo nafsi yako na itachoka nakuwa na unyonge; hana swaumu atakayefunga mwaka mzima; kiasi ambacho hakupata malipo ya swaumu kwa kwenda kinyume na katazo, na hakufungua kwa sababu aliendelea. Kisha akamuelekeza kufunga siku tatu katika kila mwezi, hizo ni sawa na swaumu ya mwaka mzima; kwa sababu kila siku moja ni sawa na siku kumi, ambayo ndiyo ziada ndogo zaidi ya mema. Akasema Abdullah: Hakika mimi ninaweza zaidi ya hizo. Akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: Basi funga swaumu ya Daudi amani iwe juu yake na ndiyo swaumu bora, alikuwa akifunga siku moja na anafungua siku moja, na alikuwa hakimbii anapokutana na adui; kwa sababu namna ya swaumu yake haikudhoofisha mwili wake.

Mafunzo

  • Kufunga siku tatu katika kila mwezi ni kama kufunga mwaka mzima, na hii ni kwa sababu jema moja hulipwa mara kumi mfano wake, zinakuwa siku thelathini, akifunga katika kila mwezi siku tatu anakuwa kana kwamba kafunga mwaka mzima.
  • Miongoni mwa njia za ufikishaji ujumbe wa Mwenyezi Mungu ni kuhamasisha katika amali na kueleza thawabu zake na thawabu za kudumu na amali hiyo
  • Amesema Khattwabi: Muhutasari wa kisa cha Abdallah bin Amri nikuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu hajamuwekea ibada ya swaumu pekee mja wake, bali kamuwekea aina mbali mbali za ibada, hata angemaliza juhudi zake zote angepunguza katika ibada zingine, jambo bora ni kuwa kati na kati ili abakishe baadhi ya nguvu kwa ajili ya ibada zingine, na limeashiriwa hilo katika kauli yake rehema na amani ziwe juu yake kwa Daudi amani iwe juu yake: "Na alikuwa hakimbii anapokutana na adui"; kwa sababu alikuwa akipata nguvu kwa kufungua kwa ajili ya Jihadi.
  • Katazo la kuzama na kujikalifisha katika ibada, na kheri inakuwa kwa kushikamana na sunna.
  • kauli ya jopo la wanachuoni ni kuchukiza kufunga milele, na inakuwa ni haramu atakapoipa tabu nafsi na akaidhuru, na akaibebesha mzigo mzito, na akaachana na sunna ya Nabii wake rehema na amani ziwe juu yake, na akaitakidi kuwa isiyokuwa sunna yake ndiyo bora kuliko sunna.
Ufafanuzi: العربية

بَلَغَ النبيَّ صلى الله عليه وسلم أنَّ عبدَ الله بن عمرو رضي الله عنهما كان يَسْرُدُ الصومَ ولا يُفطر طوال السنة، ويصلي الليل كله ولا ينام، فنهاه عن ذلك وقال له: صم وأفطر، وقم ونم. ونهاه عن سَرْدِ الصيام وقيام الليل كله، وقال له: إنك إن فعلت ذلك ضَعُفَتْ له عينُك وغارَتْ ودَخَلَتْ، ونَفِهَتْ له نفسُك وتَعبِتْ وكَلَّتْ؛ فلا صام من صام السنة؛ حيث إنه لم يحصل على أجر الصوم لمخالفة النهي، ولم يفطر لأنه أمسك. ثم أرشده إلى صيام ثلاثة أيام من كل شهر فهو صوم السنة؛ لأن كل يوم بعشرة أيام وهو أقل المضاعفة للحسنة. فقال عبدالله: إني أستطيع أكثر من ذلك. قال صلى الله عليه وسلم: إذن فصم صوم داود عليه السلام وهو أفضل الصيام، كان يصوم يومًا ويفطر يومًا، وكان لا يَفِرُّ إذا لاقى العدو؛ لأن طريقة صومه لم تُضعِفْ بدنَه.

  • صيام ثلاثة أيام من كلِّ شهر كصيام السنة كلها، وذلك لأنَّ الحسنة بعشرة أمثالها، فتكون ثلاثين يومًا، فإذا صام من كل شهر ثلاثة أيام فكأنه صام السنة كلَّها.
  • من أساليب الدعوة إلى الله الترغيب في العمل وذكر ثوابه وثواب المواظبة عليه.
  • قال الخطابي: مُحَصَّل قصة عبد الله بن عمرو أن الله تعالى لم يَتَعَبَّد عبدَه بالصوم خاصة، بل تعبده بأنواع من العبادات، فلو استفرغ جهده لَقَصَّرَ في غيره، فالأولى الاقتصاد فيه ليستبقي بعض القوة لغيره، وقد أشير إلى ذلك بقوله عليه الصلاة والسلام في داود عليه السلام: "وكان لا يفر إذا لاقى"؛ لأنه كان يتقوى بالفطر لأجل الجهاد.
  • النهي عن التعمق والتكلف في العبادة، والخير التزام السنة.
  • مذهب جمهور أهل العلم كراهية صوم الدهر، ويكون حرامًا إذا شَدَّدَ على نفسه وأَضَرَّ بها وحَمَل عليها، ورَغِبَ عن سنة نبيه صلى الله عليه وسلم، واعتقد أن غير سنته أفضل منها.

Mada

Ripoti kosa

Zaidi