Hadithi

Wana nini watu waliosema kadhaa wa kadhaa? lakini mimi ninaswali na ninalala na ninafunga na ninakula, na ninaoa wanawake; atakayeuchukia muongozo wangu basi hayuko nami

Chanzo: HadeethEnc.com, Kiswahili v1.18.0

SahihiWamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake

Matini ya Kiarabu

عَنْ أَنَسٍ رضي الله عنه: أَنَّ نَفَرًا مِنْ أَصْحَابِ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ سَأَلُوا أَزْوَاجَ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ عَنْ عَمَلِهِ فِي السِّرِّ؟ فَقَالَ بَعْضُهُمْ: لَا أَتَزَوَّجُ النِّسَاءَ، وَقَالَ بَعْضُهُمْ: لَا آكُلُ اللَّحْمَ، وَقَالَ بَعْضُهُمْ: لَا أَنَامُ عَلَى فِرَاشٍ، فَحَمِدَ اللهَ وَأَثْنَى عَلَيْهِ، فَقَالَ: «مَا بَالُ أَقْوَامٍ قَالُوا كَذَا وَكَذَا؟ لَكِنِّي أُصَلِّي وَأَنَامُ، وَأَصُومُ وَأُفْطِرُ، وَأَتَزَوَّجُ النِّسَاءَ، فَمَنْ رَغِبَ عَنْ سُنَّتِي فَلَيْسَ مِنِّي».

Tafsiri

Imepokelewa kutoka kwa Anas -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe ju yake-: Ya kwamba kuna kundi miongoni mwa wanafunzi wa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- waliwauliza wake za Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- kuhusu amali zake za siri? (walipojibiwa) wakasema baadhi yao: Mimi sitooa wanawake. Na wakasema baadhi yao: Na mimi sitokula nyama. Na wakasema baadhi yao: Sitolala juu ya godoro. Hilo likamfikia Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- akamshukuru Mwenyezi Mungu na akamsifia, na akasema: "Wana nini watu waliosema kadhaa wa kadhaa? lakini mimi ninaswali na ninalala na ninafunga na ninakula, na ninaoa wanawake; atakayeuchukia muongozo wangu basi hayuko nami".

Ufafanuzi

Lilikuja kundi la Maswahaba radhi za Allah ziwe juu yao, katika nyumba za wake za Mtume rehema na amani ziwe juu yake, wakiuliza kuhusu ibada zake za siri ndani ya nyumba yake, walipoelezwa wakawa kana kwamba za kwao wameziona ndogo, wakasema: Na tuko wapi sisi na Mtume rehema na amani ziwe juu yake? hali yakuwa amekwisha samehewa yaliyotangulia katika madhambi yake na yajayo, ukilinganisha na ambaye hajajua hata kupatikana kwa msamaha, huyu anahitaji kupitiliza katika kufanya ibada huenda akaupata msamaha huo. Kisha wakasema baadhi yao: Sitooa wanawake. Na wakasema baadhi yao: Sitokula nyama. Na wakasema baadhi yao: Sitolala katika godoro. Hilo likamfikia Mtume rehema na amani ziwe juu yake, akachukia, na akawahutubia watu, akamhimidi Mwenyezi Mungu na akamtukuza, na akasema: Wana nini watu fulani waliosema kadhaa wa kadhaa?! Wallahi mimi ndiye ninayemuhofu sana Mwenyezi Mungu kuliko watu wote na ndiyo mchamungu wenu, lakini ninalala ili nipate nguvu ya kusimama, na ninafungua ili nipate nguvu ya kufunga, na ninaoa wanawake, atakayeipuuza njia yangu, na akaona njia nyingine ndio iliyokamilika, na akachukua njia ya asiyekuwa mimi, huyu hayuko nami.

Mafunzo

  • Mapenzi ya kheri kwa Maswahaba radhi za Allah ziwe juu yao, na shauku yao juu yake, na kwa baadhi yao kumuiga Mtume rehema na amani ziwe juu yake.
  • Upole wa sheria hii na wepesi wake, kwa kuchukua kutoka katika matendo ya Nabii wao na muongozo wake.
  • Kheri na baraka iko katika kumuiga Mtume rehema na amani ziwe juu yake, na kwa kufuata hali zake tukufu.
  • Kemeo la kuitilia mkazo nafsi katika ibada kwa yale isiyoyaweza, nakuwa hili ni katika hali za wazushi.
  • Amesema bin Hajari: Kuchukua kwa mkazo katika ibada kunapelekea katika uchovu unaokata asili yake, na kudumu na kuishia katika faradhi peke yake, na kuacha kufanya sunna kunapelekea kuamsha uvivu, na kukosa uchangamfu katika ibada, na jambo bora ni la kati na kati.
  • Hapa kuna fundisho la kufuatilia hali za wakubwa kwa ajili kuiga kutoka katika matendo yao, nakuwa inaposhindikana kulijua hilo kutoka kwa wanaume inafaa kulibaini hilo kutoka kwa wanawake.
  • Hapa kuna mawaidha na kutoa maswala ya kielemu na kubainisha hukumu kwa watu wazima, na kuondoa utata kwa wale wenye kujitahidi.
  • Amri ya kujihurumia katika ibada, ikiwa ni pamoja na kuihifadhi na kuzihifadhi faradhi na sunna; ili muislamu achunge haki za mtu mwingine.
  • Katika hadithi kuna dalili juu ya fadhila za ndoa na himizo lake.
Ufafanuzi: العربية

جَاءَ نَفَرٌ من الصحابة رضي الله عنهم إلى بيوت أزواج النبي صلى الله عليه وسلم، يسألون عن عبادته في السر داخل بيته، فلما أُخبروا كأنهم تَقَالُّوها، فقالوا: وأين نحن من النبي صلى الله عليه وسلم؟ قد غُفر له ما تقدم من ذنبه وما تأخر، بخلاف مَن لم يعلم بحصول المغفرة له فيحتاج إلى المبالغة في العبادة عسى أن يَحصُل عليها. ثم قال بعضهم: لا أتزوج النساء. وقال بعضهم: لا آكل اللحم. وقال بعضهم: لا أنام على فراش. فبلغ ذلك النبيَّ صلى الله عليه وسلم، فغضب، وخطب الناس، فحمد الله وأثنى عليه وقال: ما شَأْنُ أقوامٍ قالوا كذا وكذا؟! والله إني لأخشاكم لله وأتقاكم له، لكني أنام لأتقوى على القيام، وأفطر لأتقوَّى على الصوم، وأتزوج النساء، فمن أعرض عن طريقتي ورأى الكمال في غيرها، وأخذ بطريقة غيري فليس مني.

  • حب الصحابة رضي الله عنهم للخير، ورغبتهم فيه وفى الاقتداء بنبيهم صلى الله عليه وسلم.
  • سماحة هذه الشريعة ويسرها، أخذًا من عمل نبيها صلى الله عليه وسلم وهديه.
  • الخير والبركة في الاقتداء بالنبي صلى الله عليه وسلم، واتباع أحواله الشريفة.
  • الزَّجْر عن التشديد على النفس في العبادات بما لا تطيق، وأن هذا من حال المبتدعين.
  • قال ابن حجر: الأخذ بالتشديد في العبادة يُفضي إلى المَلَل القاطِع لأصلها، وملازمة الاقتصار على الفرائض مثلًا، وترك التنفُّل يفضي إلى إيثار البطالة، وعدم النشاط إلى العبادة، وخير الأمور الوسط.
  • فيه تتبُّع أحوال الأكابر للتأسِّي بأفعالهم، وأنه إذا تعذَّرت معرفته من الرجال جاز استكشافه من النساء.
  • فيه الوعظ وإلقاء مسائل العلم وبيان الأحكام للمكلَّفين، وإزالة الشبهة عن المجتهدين.
  • الأمر بالترفُّق في العبادة، مع المحافظة عليها وعلى الفرائض والنوافل؛ ليراعي المسلم حقوق غيره عليه.
  • في الحديث دلالة على فضل النكاح والترغيب فيه.

Mada

Ripoti kosa

Zaidi