Chanzo: HadeethEnc.com, Kiswahili v1.18.0
Matini ya Kiarabu
عَنِ أبي زُهير عُمَارَةَ بْنِ رُؤَيْبَةَ رضي الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللهِ صلى الله عليه وسلم: «لَنْ يَلِجَ النَّارَ أَحَدٌ صَلَّى قَبْلَ طُلُوعِ الشَّمْسِ وَقَبْلَ غُرُوبِهَا»
Tafsiri
Kutoka kwa Abuu Zuhairi Umara bin Ruaiba radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Amesema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Kamwe, hatoingia motoni mtu yeyote aliyeswali kabla ya kuchomoza Jua na kabla ya kuzama kwake"
Ufafanuzi
Anaeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake: Kuwa hatoingia motoni mtu yeyote aliyeswali swala ya Alfajiri, na swala ya Lasiri, na akadumu nazo; na amezitaja maalumu swala hizi mbili; kwa sababu ndizo swala nzito zaidi, na kwa sababu wakati wa Alfajiri huwa ni wakati wa usingizi na ladha yake, na wakati wa Lasiri huwa ni wakati wa kushughulishwa na kazi za mchana na biashara zake, na atakayezihifadhi swala hizi mbili pamoja na kupatikana tabu ndani yake, basi bila shaka ataweza kuzihifadhi swala zingine zilizobakia.
Mafunzo
- Ubora wa swala mbili, Alfajiri na Lasiri, ni lazima kuzihifadhi.
- Na atakayezitekeleza swala hizi mara nyingi nafsi yake huepukana na uvivu na kujionyesha na hupenda ibada.
Ufafanuzi: العربية
يُخْبِرُ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم: أنه لن يدخلَ النارَ، أحدٌ صلّى صلاة الفجر، وصلاة العصر، وداوم عليهما؛ وخَصَّ هاتين الصلاتين؛ لأنهما أثقلُ الصلوات، ولأنّ وقت الصبح يكون عند النوم ولَذَّتِه، ووقت العصر يكون عند الاشتغال بأعمال النهار وتجارته، ومَن حافَظَ على هاتين الصلاتَين مع وُجودِ المَشقّة فسيحافظ على بَقيّة الصلوات.
- فضل صلاتي الصبح والعصر، فينبغي المحافظة عليهما.
- مَن أدَّى هذه الصلوات يكون غالبًا خالي النفس من الكَسَل والرياء مُحِبًّا للعبادة.