Hadithi

Hakuna Muislamu yeyote atafikiwa na Sala ya lazima kisha akaufanya vizuri udhu wake, na Unyenyekevu wake na Rakaa zake, isipokuwa inakuwa ni kifuta madhambi yaliyo kuwa kabla ya Sala, kwa muda ambao hajafanya madhambi makubwa, na hivyo ndivyo ilivyo kila siku

Chanzo: HadeethEnc.com, Kiswahili v1.18.0

SahihiImepokelewa Imamu Muslim

Matini ya Kiarabu

عَنْ عُثْمَانَ رضي الله عنه قَالَ: سَمِعْتُ رَسُولَ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَقُولُ: «مَا مِنَ امْرِئٍ مُسْلِمٍ تَحْضُرُهُ صَلَاةٌ مَكْتُوبَةٌ فَيُحْسِنُ وُضُوءَهَا وَخُشُوعَهَا وَرُكُوعَهَا، إِلَّا كَانَتْ كَفَّارَةً لِمَا قَبْلَهَا مِنَ الذُّنُوبِ، مَا لَمْ يُؤْتِ كَبِيرَةً، وَذَلِكَ الدَّهْرَ كُلَّهُ».

Tafsiri

kutoka kwa Othmani Radhi za Allah ziwe juu yake- Amesema: Nilimsikia Mtume rehema na amani za Allah ziwe juu yake akisema: "Hakuna Muislamu yeyote atafikiwa na Sala ya lazima kisha akaufanya vizuri udhu wake, na Unyenyekevu wake na Rakaa zake, isipokuwa inakuwa ni kifuta madhambi yaliyo kuwa kabla ya Sala, kwa muda ambao hajafanya madhambi makubwa, na hivyo ndivyo ilivyo kila siku".

Ufafanuzi

Anabainisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa hakuna muislamu atakayekutwa na wakati wa swala ya faradhi akatawadha vizuri udhu wake na ukaukamilisha, kisha akawa na unyenyekevu ndani ya swala yake kiasi kwamba ukawa moyo wake na viungo vyake vyote vimeelekea kwa Mwenyezi Mungu akivuta picha ya utukufu wake, na akatimiza vitendo vya swala kama rukuu na sijida na vinginevyo, isipokuwa swala hii itakuwa ni kifutio cha madhambi madogo madogo yaliyokuwa kabla yake, madam hajafanya dhambi katika madhambi makubwa, na fadhila hii ni endelevu kwa muda wote na katika kila swala.

Mafunzo

  • Swala inayofuta madhambi ni ile ambayo mja katawadha vizuri udhu wake, na akaitekeleza kwa unyenyekevu akitafuta radhi za Mwenyezi Mungu kwa swala hiyo.
  • Fadhila za kudumu katika ibada, nakuwa ibada ni sababu ya kusamehewa madhambi madogo.
  • Fadhila za kutawadha vizuri, na kuswali vizuri pamoja na utulivu ndani yake.
  • Umuhimu wa kuyaepuka madhambi makubwa ili kusamehewa madhambi madogo.
  • Madhambi makubwa hayafutwi ila kwa toba.
Ufafanuzi: العربية

بَيَّنَ النبيُّ صلى الله عليه وسلم أنَّه ما مِن مُسلم يَدخل عليه وقت الصلاة المفروضة فيحسن وضوءها ويُتِمُّه، ثم يَخشع في صلاته بحيث يكون قلبُه وجوارحُه كلُّها مُقبلةً على الله مستحضرةً عظمتَه، ويُتم أفعالَ الصلاةِ كالركوعِ والسجود وغيرِهِ، إلا كانت هذه الصلاةُ مُكفِّرَةً لما قبلها من المعاصي الصغائر، ما لم يعمل كبيرة من كبائر الذنوب، وهذا الفضل مُمْتَدٌّ على مَرِّ الزمان وفي كل صلاة.

  • الصلاة المكفرة للذنوب هي التي أحسن العبد وضوءَها، وأدَّاها خاشعًا يبتغي بها وجه الله تعالى.
  • فضل المداومة على العبادات، وأنها سبب لمغفرة صغائر الذنوب.
  • فضل إحسان الوضوء، وإحسان الصلاة والخشوع فيها.
  • أهمية اجتناب كبائر الذنوب لمغفرة الذنوب الصغائر.
  • كبائر الذنوب لا تُكَفَّر إلا بالتوبة.

Mada

Ripoti kosa

Zaidi