Hadithi

Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, mimi sijaacha dhambi yoyote wala maasi yoyote isipokuwa nimeyafanya, akasema: "Hivi wewe hautamki neno la shahada "Ash-hadu an-laa ilaaha illa llahu wa anna Muhamadan rasuulullah?

Chanzo: HadeethEnc.com, Kiswahili v1.18.0

SahihiImepokelewa na Abu Yaala, Twabarani na Dhwiyau Almaqidisi

Matini ya Kiarabu

عَنْ أَنَسٍ رضي الله عنه قَالَ: جَاءَ رَجُلٌ إِلَى النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فَقَالَ: يَا رَسُولَ اللهِ، مَا تَرَكْتُ حَاجَّةً وَلَا دَاجَّةً إِلَّا قَدْ أَتَيْتُ، قَالَ: «أَلَيْسَ تَشْهَدُ أَنْ لَا إِلَهَ إِلَّا اللهُ وَأَنَّ مُحَمَّدًا رَسُولُ اللهِ؟» ثَلَاثَ مَرَّاتٍ. قَالَ: نَعَمْ، قَالَ: «فَإِنَّ ذَلِكَ يَأْتِي عَلَى ذَلِكَ».

Tafsiri

Imepokelewa kutoka kwa Anas -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe ju yake- amesema: Alikuja mtu mmoja kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-akasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, mimi sijaacha dhambi yoyote wala maasi yoyote isipokuwa nimeyafanya, akasema: "Hivi wewe hautamki neno la shahada "Ash-hadu an-laa ilaaha illa llahu wa anna Muhamadan rasuulullah?" Akarudia mara tatu. Akasema: Ndiyo, akasema: "Kwa hakika tamko hilo hufuta makosa hayo yote."

Ufafanuzi

Alikuja mtu mmoja kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-akasema: @Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, mimi sijaacha dhambi yoyote wala maasi yoyote madogo wala makubwa isipokuwa nimeyafanya, je mimi nitakuwa ni mwenye kusamehewa? Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akasema kumwambia: Hivi wewe hautamki neno la shahada "Ash-hadu an-laa ilaha illa llahu wa anna Muhamadan rasuulullah? Akarudia kumwambia hivyo mara tatu, Basi akajibu: Ndiyo nashuhudia, Basi Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akampa habari ya ubora na utukufu wa shahada mbili na namna inavyofuta makosa, na kuwa toba hufuta makosa yaliyopita.

Mafunzo

  • Utukufu wa shahada mbili na namna inavyoyashinda madhambi kwa yule atakayesema maneno hayo kwa dhati kutoka moyoni mwake.
  • Uislamu hufuta makosa yaliyopita huko nyuma.
  • Tauba ya kweli hufuta makosa yaliyopita huko nyuma.
  • Kurudia rudia katika kujifunza ni miongoni mwa miongozo ya bwana Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-.
  • Utukufu wa shahada mbili, na kuwa shahada mbili ni sababu ya kuepuka kukaa Motoni milele.
Ufafanuzi: العربية

جاء رجلٌ إلى النبي صلى الله عليه وسلم فقال: يا رسول الله، إني قد فعلت من كل الذنوب والمعاصي، ولم أترك صغيرة ولا كبيرة إلا فعلتها، فهل يُغفَر لي؟ فقال له النبي صلى الله عليه وسلم: ألست تشهد أن لا إله إلا الله وأن محمدًا رسول الله؟ كررها له ثلاث مرات، فأجابه: نعم أشهد، فأخبره النبي صلى الله عليه وسلم بفضل الشهادتين وتكفيرها للسيئات، وأن التوبة تجب ما قبلها.

  • عِظم الشَّهادتين ورُجحانها على الذّنوب لمن قالها صادقًا من قلبه.
  • الإسلام يجُبُّ ما قبله.
  • التّوبة الصّادقة تمحو ما قبلها.
  • التّكرار في التّعليم مِن هدي النبي صلى الله عليه وسلم.
  • فضل الشهادتين، وأنهما سبب للنجاة من الخلود في النار.

Mada

Ripoti kosa

Zaidi