Hadithi

Ni haki kwa kila muislamu aoge katika kila siku saba walau siku moja, aoshe ndani yake kichwa chake na mwili wake

Chanzo: HadeethEnc.com, Kiswahili v1.18.0

SahihiWamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake

Matini ya Kiarabu

عن أبي هريرة قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم: «حَقٌّ عَلَى كُلِّ مُسْلِمٍ أَنْ يَغْتَسِلَ فِي كُلِّ سَبْعَةِ أَيَّامٍ يَوْمًا، يَغْسِلُ فِيهِ رَأْسَهُ وَجَسَدَهُ».

Tafsiri

Na imepokelewa katika sahihi Bukhari kutoka kwa Abuu Huraira Amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Ni haki kwa kila muislamu aoge katika kila siku saba walau siku moja, aoshe ndani yake kichwa chake na mwili wake".

Ufafanuzi

Ameeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: Ni haki iliyotiwa mkazo kwa kila muislamu aliyebalehe mwenye akili timamu aoge katika kila siku saba za wiki siku moja, aoshe katika siku hiyo kichwa chake na mwili wake, kwa kutafuta twahara na usafi, na siku bora katika siku hizi ni siku ya Ijumaa, kama inavyojulikana kutoka katika baadhi ya riwaya, na kuoga siku ya Ijumaa kabla ya swala ni sunna iliyotiwa mkazo, hata kama atakuwa alioga siku ya Alhamisi kwa mfano, na kinachoiondoa katika uwajibu ni kauli ya Aisha -Radhi za Allah ziwe juu yake-: "Watu walikuwa wakifanya kazi na shughuli mbali mbali za kimaisha, na walikuwa wanapokwenda katika Ijumaa wanakwenda katika muonekano wao huo huo: Wakaambiwa: Basi mngeoga (Ingekuwa kheri)", kaipokea Bukhari, na katika riwaya yake nyingine: "Wakiwa na harufu" Yaani: Harufu ya jasho na mfano wake, lakini pamoja na hivyo wakaambiwa (Lau mgeoga ingekuwa bora), hivyo kwa wasiokuwa Masahaba wanahaja kubwa ya kulitekeleza hili.

Mafunzo

  • Kutilia umuhimu na kujali kwa Uislamu swala la usafi na twahara.
  • Kuoga siku ya Ijumaa kumependekezwa sana tena kwa mkazo kwa ajili ya swala.
  • Kimetajwa kichwa, pamoja nakuwa kutajwa mwili kungetosha kukusanya na kichwa; Lakini ni kwa ajili ya kukitilia maanani.
  • Ni wajibu kuoga kwa kila aliyepatwa na harufu mbaya, inayo waudhi watu.
  • Siku muhimu zaidi kwa ajili ya kuoga ni siku ya Ijumaa; kwa sababu ya fadhila zake.
Ufafanuzi: العربية

أَخْبَرَ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم: أنه حقٌّ متأكد على كل مسلم بالغ عاقل أنْ يغتسلَ في كل سبعة أيام من الأسبوع يومًا، فيغسل في هذا اليوم رأسَه وجسدَه، طلبًا للطهارة والنظافة، وأَولى هذه الأيام يومُ الجمعة، كما يُفهم من بعض الروايات، والاغتسال يوم الجمعة قبل الصلاة مستحب استحبابًا مؤكدًا، ولو كان اغتسل يوم الخميس مثلًا، والصارف عن الوجوب قول عائشة رضي الله عنها: "كان الناسُ مَهَنَةَ أنفسهم، وكانوا إذا راحوا إلى الجمعة راحوا في هيئتهم: فقيل لهم: لو اغتسلتم"، رواه البخاري، وفي رواية له: "لهم أرواح" أي رائحة العَرَقِ ونحوِه، ومع ذلك قيل لهم "لو اغتسلتم"، فغيرُهم من باب أولى.

  • اهتمام وعناية الإسلام بالنظافة والطهارة.
  • غسل الجمعة مستحب استحبابًا مُؤكدًا للصلاة.
  • ذِكْر الرَّأس وإن كان ذِكْر الجسد يشمله؛ للاهتمام به.
  • ﻳﺠﺐ ﺍﻟﻐﺴﻞ ﻋﻠﻰ ﻛﻞ ﻣﻦ ﻭُﺟِﺪﺕْ ﺑﻪ ﺭﺍﺋﺤﺔٌ ﻛﺮﻳﻬﺔٌ ﻳﺘﺄﺫﻯ ﺑﻬﺎ ﺍﻟﻨﺎس.
  • آكَدُ يومٍ للاغتسال يوم الجمعة؛ لفضله.

Mada

Ripoti kosa

Zaidi