Hadithi

Katika uzuri wa uislamu wa mtu: Ni kuacha kwake yale yasiyomuhusu

Chanzo: HadeethEnc.com, Kiswahili v1.18.0

Amesema Imamu Nawawi: Hadithi hii ni hasanImepokelewa naTirmidhiy na wengineo

Matini ya Kiarabu

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «مِنْ حُسْنِ إِسْلَامِ المَرْءِ تَرْكُهُ مَا لَا يَعْنِيهِ».

Tafsiri

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Amesema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Katika uzuri wa uislamu wa mtu: Ni kuacha kwake yale yasiyomuhusu".

Ufafanuzi

Amebainisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake: Ya kuwa miongoni mwa mazuri ya ukamilifu wa Uislamu wa Muislamu na ukamilifu wa imani yake, ni kujiweka kwake mbali na yale yasiyomuhusu na yale yasiyo na faida kwake miongoni mwa kauli na matendo, au katika yale yasiyomuhusu miongoni mwa mambo ya dini na dunia, mtu kushughulika na yale yasiyomuhusu huenda likamshughulisha akaacha yale yanayomuhusu, au likampelekea katika yale yanayomlazimu kuyaepuka; kwani mwanadamu ataulizwa kuhusu matendo yake siku ya Kiyama.

Mafunzo

  • Watu wanatofautiana katika Uislamu wao, na kwamba Uislamu huzidi uzuri kwa baadhi ya matendo.
  • Kuacha upuuzi na mambo yasiyo na faida miongoni mwa maneno na matendo ni dalili ya ukamili wa Uislamu wa mtu.
  • Himizo la mtu kushughulika na yale yanayomuhusu katika mambo ya dini yake na dunia yake, ikiwa miongoni mwa uzuri wa Uislamu wa mtu ni kuacha yale yasiyomuhusu, basi katika uzuri wake pia ni kushughulika na yale yanayomuhusu.
  • Amesema bin Qayyim Mwenyezi Mungu amrehemu: Na amekusanya Mtume rehema na amani ziwe juu yake unyenyekevu wote katika neno moja, akasema: "Katika uzuri wa Uislamu wa mtu: Ni kuacha kwake yale yasiyomuhusu", hii inakusanya kuacha yale yasiyomuhusu: Miongoni mwa maneno na kutazama, na kusikiliza, na kushika, na kutembea, na kufikiria, na harakati zote za wazi na za siri, neno hili linatosheleza sana katika unyenyekevu.
  • Amesema bin Rajab: Hadithi hii ni msingi miongoni mwa misingi ya adabu.
  • Himizo la kutafuta elimu; kwa sababu kupitia elimu mwanadamu anajua yanayomuhusu na yasiyomuhusu.
  • Kuamrisha mema na kukataza maovu na kutoa nasaha ni miongoni mwa mambo yanayomuhusu mwanadamu; kwa sababu ameamrishwa kufanya hivyo.
  • Inaingia katika ujumla wa maana ya hadithi: Kujiweka mbali na yale yasiyomuhusu, yale aliyoyaharamisha Mwenyezi Mungu Aliyetakasika na kutukuka na yale aliyoyachukia Mtume rehema na amani ziwe juu yake, na vile vile yale asiyoyahitajia miongoni mwa mambo ya Akhera kama uhalisia wa ghaibu na ufafanuzi wa hukumu ya kuumbwa na amri, na miongoni mwake ni kuuliza na kutafuta kuhusu mambo ya kukadiria na kuchukulia, hali yakuwa bado hayajatokea, au pengine hayawezi kutokea kabisa, au hayapo kabisa.
Ufafanuzi: العربية

بين النبي صلى الله عليه وسلم: أن من كمال محاسن إسلام المسلم وتمام إيمانه، ابتعاده عما لا يعنيه ولا يخصه ولا يهمه وما لا يفيده من الأقوال والأفعال، أو مما لا يعنيه من أمور الدين والدنيا، فالاشتغال بما ليس للإنسان ربما شغله عما يعنيه، أو أداه إلى ما يلزمه اجتنابه؛ فإن الإنسان مسؤول عن أعماله يوم القيامة.

  • الناس يتفاوتون في الإسلام، وأنه يزداد حسنًا ببعض الأعمال.
  • ترك اللغو والفضول من الأقول والأفعال دليل على كمال إسلام المرء.
  • الحث على الاشتغال فيما يعني المرءَ من شؤون دِينه ودنياه، فإذا كان مِن حُسن إسلام المرء تركه ما لا يعنيه، فمِن حُسنه إذًا اشتغالُه فيما يعنيه.
  • قال ابن القيم رحمه الله : وقد جمع النبي صلى الله عليه وسلم الورع كله في كلمة واحدة، فقال: «من حسن إسلام المرء: تركُه ما لا يعنيه»، فهذا يعم الترك لما لا يعني: من الكلام، والنظر، والاستماع، والبطش، والمشي، والفكر، وسائر الحركات الظاهرة والباطنة، فهذه كلمة شافية في الورع.
  • قال ابن رجب: هذا الحديث أصل من أصول الأدب.
  • الحث على طلب العلم؛ لأن به بعرف الإنسان ما يعنيه مما لا يعنيه.
  • الأمر بالمعروف والنهي عن المنكر والنصيحة مما تعني الإنسان؛ لأنه مأمور بها.
  • يدخل في عموم معنى الحديث: الابتعاد عما لا يعني مما حرم الله عزوجل وما كرهه النبي صلى الله عليه وسلم، وكذلك ما لا يحتاج إليه من أمور أخروية كحقائق الغيب وتفاصيل الحكم في الخلق والأمر، ومنها السؤال والبحث عن مسائل مقدرة ومفترضة لم تقع، أو لا تكاد تقع، أو لا يتصور وقوعها.

Mada

Ripoti kosa

Zaidi