Hadithi

Vaeni katika nguo zenu nguo nyeupe, kwani hizo ni katika nguo zenu bora, na wavisheni kwazo maiti wenu

Chanzo: HadeethEnc.com, Kiswahili v1.18.0

SahihiImepokelewa na Abu Daud, Tirmidhiy na Ibn Majah

Matini ya Kiarabu

عَنِ ابْنِ عَبَّاسٍ رَضيَ اللهُ عنهُما قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «البَسُوا مِنْ ثِيَابِكُمُ البَيَاضَ، فَإِنَّهَا مِنْ خَيْرِ ثِيَابِكُمْ، وَكَفِّنُوا فِيهَا مَوْتَاكُمْ».

Tafsiri

Imepokelewa kutoka kwa bin Abbas radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -rehema na amani ziwe juu yake-: "Vaeni katika nguo zenu nguo nyeupe, kwani hizo ni katika nguo zenu bora, na wavisheni kwazo maiti wenu".

Ufafanuzi

Anawaelekeza Mtume rehema na amani ziwe juu yake wanaume kuvaa nguo zenye rangi nyeupe na kuwavisha maiti pia; kwani ni katika nguo bora.

Mafunzo

  • Sunna ya kuvaa nguo nyeupe, na inafaa pia kuvaa rangi nyingine tofauti na hiyo.
  • Sunna ya kuwavisha maiti nguo nyeupe.
  • Amesema Shaukani: Na hadithi inaonyesha sheria ya kuvaa nguo nyeupe na kuwavisha nazo maiti pia; kwakuwa ni safi zaidi na ni nzuri zaidi, ama kuwa kwake ni nzuri hili liko wazi, na ama kuwa kwake ni safi ni kwa sababu kitu chochote hata kikwa kidogo kikidondokea juu yake huonekana, ndio maana inapendekezwa.
Ufafanuzi: العربية

يرشد النبي صلى الله عليه وسلم الرجال بلبس الثياب ذات اللون الأبيض وتكفين الموتى فيها؛ فإنها من خير الثياب.

  • استحباب لبس الثوب الأبيض، ويجوز غيره من الألوان.
  • استحباب تكفين الموتى بالبياض.
  • قال الشوكاني: والحديث يدل على مشروعية لبس البياض وتكفين الموتى به؛ كونه أطهر من غيره وأطيب، أما كونه أطيب فظاهر، وأما كونه أطهر فلأن أدنى شيء يقع عليه يظهر فيفضل.

Mada

Ripoti kosa

Zaidi