Chanzo: HadeethEnc.com, Kiswahili v1.18.0
Matini ya Kiarabu
عَنْ جَابِرِ بْنِ عَبْدِ اللَّهِ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُمَا قَالَ: كُنَّا فِي غَزَاةٍ فَكَسَعَ رَجُلٌ مِنَ المُهَاجِرِينَ رَجُلًا مِنَ الأَنْصَارِ، فَقَالَ الأَنْصَارِيُّ: يَا لَلْأَنْصَارِ، وَقَالَ المُهَاجِرِيُّ: يَا لَلْمُهَاجِرِينَ، فَسَمَّعَهَا اللَّهُ رَسُولَهُ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: «مَا هَذَا؟» فَقَالُوا: كَسَعَ رَجُلٌ مِنَ المُهَاجِرِينَ رَجُلًا مِنَ الأَنْصَارِ، فَقَالَ الأَنْصَارِيُّ: يَا لَلْأَنْصَارِ، وَقَالَ المُهَاجِرِيُّ: يَا لَلْمُهَاجِرِينَ، فَقَالَ النَّبِيُّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «دَعُوهَا فَإِنَّهَا مُنْتِنَةٌ» قَالَ جَابِرٌ: وَكَانَتِ الأَنْصَارُ حِينَ قَدِمَ النَّبِيُّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ أَكْثَرَ، ثُمَّ كَثُرَ المُهَاجِرُونَ بَعْدُ، فَقَالَ عَبْدُ اللَّهِ بْنُ أُبَيٍّ: أَوَقَدْ فَعَلُوا، وَاللَّهِ لَئِنْ رَجَعْنَا إِلَى المَدِينَةِ لَيُخْرِجَنَّ الأَعَزُّ مِنْهَا الأَذَلَّ، فَقَالَ عُمَرُ بْنُ الخَطَّابِ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ: دَعْنِي يَا رَسُولَ اللَّهِ أَضْرِبُ عُنُقَ هَذَا المُنَافِقِ، قَالَ النَّبِيُّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «دَعْهُ، لاَ يَتَحَدَّثُ النَّاسُ أَنَّ مُحَمَّدًا يَقْتُلُ أَصْحَابَهُ».
Tafsiri
Kutoka kwa Jaabir bin Abdillaah -radhi za Allah ziwe juu yao (yeye na baba yake), amesema: Tulikuwa vitani, mtu mmoja katika Muhajirina akampiga mmoja katika Answari, Answari akasema: Maanswari naombeni msaada!, na akasema Mhajiri (mtu wa Makka): Naombeni msaada enyi Muhajirina!, Mwenyezi Mungu akamsikilizisha sauti zile Mtume wake rehema na amani ziwe juu yake, akasema: "Nini hiki?" Wakasema: Mtu mmoja miongoni mwa Muhajirina kampiga mtu katika Maanswari, akasema Answari: Naombeni msaada enyi Maanswari, na akasema Mhajiri: Naombeni msaada enyi Muhajirina, akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Achaneni (na ubaguzi) kwani una nuka" Amesema Jabiri: Na Maanswari walikuwa wengi kipindi alipofika Mtume rehema na amani ziwe juu yake, kisha Muhajirina wakawa wengi baada ya hapo, akasema Abdallah bin Ubaiyi: Vipi wamepigana? Na Wallahi tukirejea Madina watukufu watawafurusha madhalili, akasema Omari bin Khattwabi: Naomba uniache mimi ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu nikate shingo ya huyu mnafiki, akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Muache ili watu wasiseme Muhammadi anauwa Maswahaba zake".
Ufafanuzi
Mtume rehema na amani ziwe juu yake alikuwa safarini katika vita na akiwa pamoja na Maswahaba zake miongoni mwa Muhajirina na Maanswari radhi za Allah ziwe juu yao, mtu mmoja katika Muhajirina akampiga mgongoni mtu mmoja miongoni mwa Maanswari kwa mkono wake. Answari akasema: Nipeni msaada enyi Maanswari, na akasema Muhajiri: Nipeni msaada enyi Muhajirina, akawasikia Mtume rehema na amani ziwe juu yake, akasema: Nini hiki?. Wakasema: Mtu mmoja katika Muhajirina kampiga mtu katika Maanswari kwa mkono wake, Answari akasema: Nipeni msaada enyi Maanswari, na Muhajiri akasema: Nipeni msaada enyi Muhajirina. Akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: Achaneni na desturi hii ya kijinga, kwani ni mbaya inachukiza na ina udhi; nayo ni kwamba mtu akizidiwa na mgomvi wake anawaita watu wake wanaanza kumsaidia sawa sawa awe kadhulumu au kadhulumiwa, kwa sababu ya ujinga wao, na ubaguzi wao. Amesema Jabiri: Na Maanswari wakati amefika Mtume rehema na amani ziwe juu yake mji wa Madina walikuwa wengi, kisha Muhajirina wakawa wengi baada ya hapo. Akasema kiongozi wa unafiki Abdallah bin Ubai bin Saluli: Jambo limefikia huko?! Wallah tukirejea Madina watukufu (anajikusudia yeye na watu wake) watawatoa katika mji wa Madina madhalili (anakusudia Mtume rehema na amani ziwe juu yake na watu wake). Akasema Omari bin Khattwab radhi za Allah ziwe juu yake: Hebu, niache ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu nikate shingo ya huyu mnafiki, akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: Muache, ili watu wasiseme kuwa Muhammadi anauwa wafuasi wake, hata kama ni kwa dhahiri.
Mafunzo
- Katazo la destuir za kijinga mbaya pamoja na tamaduni zake, iwe ni kauli au kitendo, Uislamu ulikuja kuwaweka watu mbali na hayo, na kuwaongoza katika yale yaliyo sawa na haki kwao.
- Kuchukua tahadhari dhidi ya kuwa na kundi la batili, na kuliepuka ni sawa na kukiepuka kitu kibaya kinachonuka.
- Katazo la kila chenye kuamsha uadui na chuki.
- Amesema Nawawi: Mtume rehema na amani ziwe juu yake kukiita kwake kitendo kile kuwa ni madai ya kijinga ni kwa sababu ya kukichukia, kwa sababu ni vitendo walivyokuwa navyo zama za ujinga, kama kupeana nguvu kwa makabila katika mambo ya kidunia na yahusianayo na dunia, na zama za ujinga walikuwa wakichukua haki zao kwa ukoo na makabila, Uislamu ukaja kuyabatilisha haya, na kusuluhisha kesi zote kwa hukumu za kisheria, hivyo, mtu akimtendea ubaya mwenzake hakimu atawahukumu, na atamlazimisha lolote kulingana na uadui wake alioufanya, kama ilivyothibitshwa katika kanuni za Uislamu.
- Amesema Sandi: Akabainisha kuwa usaidizi madamu ni kutoka katika kabila lake basi ni batili, hakuna haja ya kuita kila mmoja kabila lake, na ama kuitetea haki ni jambo linahitajika bali ni lazima kwa kila muumini sawa sawa awe ni kabila lake au la.
- Hali waliyokuwa nayo wanafiki kama kuwa na ulimi mchafu na ujasiri kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake na kwa Maswahaba zake radhi za Allah ziwe juu yake.
- Upole mkubwa wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake na subira yake kwa maudhi ya wanafiki anayoyapata.
- Tahadhari ya kila jambo ambalo ndani yake linawakimbiza watu katika Uislamu, na ndio mana alikataa Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwaua wanafiki, ili watu wasiseme: Kuwa Muhammadi anauwa Maswahaba zake.
Ufafanuzi: العربية
كان النبي صلى الله عليه وسلم مسافرًا في غزوة ومعه أصحابه من المهاجرين والأنصار رضي الله عنهم، فضرب رجل من المهاجرين دبر رجل من الأنصار بيده. فقال الأنصاري: أغيثوني أيها الأنصار، وقال المهاجري: أغيثوني أيها المهاجرون، فسمعها رسول صلى الله عليه وسلم قال: ما هذا؟ فقالوا: ضرب رجل من المهاجرين دبر رجل من الأنصار بيده، فقال الأنصاري: أغيثوني أيها الأنصار، وقال المهاجري: أغيثوني أيها المهاجرون. فقال النبي صلى الله عليه وسلم: دعوا هذه العادة الجاهلية فإنها قبيحة كريهة مؤذية؛ وهي أن الرجل إذا غلب عليه خصمه نادى قومه فيبتدرون إلى نصرته ظالمًا كان أو مظلومًا جهلًا منهم وعصبية. قال جابر: وكانت الأنصار حين قدم النبي صلى الله عليه وسلم المدينة مهاجرًا أكثر، ثم كثر المهاجرون بعد. فقال رأس النفاق عبد الله بن أبي بن سلول: أوقد وصل الأمر لهذا الحد؟! والله لئن رجعنا إلى المدينة ليخرجن الأعزاء -يعني نفسه ومن معه- من المدينة الأذلاء -يعني النبي صلى الله عليه وسلم ومن معه-. فقال عمر بن الخطاب رضي الله عنه: دعني يا رسول الله أضرب عنق هذا المنافق، قال النبي صلى الله عليه وسلم: دعه، لا يتحدث الناس أن محمدًا يقتل أتباعه ولو في الظاهر.
- النهي عن عادات الجاهلية المذمومة وتقاليدها، قولًا أو فعلًا، فالإسلام جاء لإبعاد الناس عن ذلك، وهدايتهم إلى ما هو الصواب والحق لهم.
- التحذير من التحزب الباطل والحذر منه كالحذر من الشيء النتن القبيح.
- النهي عن كل ما يثير العداوة والشحناء.
- قال النووي: تسميته صلى الله عليه وسلم ذلك دعوى الجاهلية فهو كراهة منه لذلك، فإنه مما كانت عليه الجاهلية من التعاضد بالقبائل في أمور الدنيا ومتعلقاتها، وكانت الجاهلية تأخذ حقوقها بالعصبات والقبائل، فجاء الإسلام بإبطال ذلك، وفصل القضايا بالأحكام الشرعية، فإذا اعتدى إنسان على آخر حكم القاضي بينهما، وألزمه مقتضى عدوانه كما تقرر من قواعد الإسلام.
- قال السندي: فبين أن النصرة لكونه من قبيلته كما عليه أهل الجاهلية باطل، فلا وجه لاستدعاء كل أحد قبيلته، وأما نصرة الحق فمطلوب لازم على كل مؤمن سواء كان من قبيلته أو لا.
- ما كان عليه المنافقون من بذاءة اللسان والجراءة على النبي صلى الله عليه وسلم وعلى أصحابه رضي الله عنهم.
- ما كان النبي صلى الله عليه وسلم عليه من شدة الحلم والصبر على ما يناله من أذية المنافقين.
- التحذير من كل عمل فيه تنفير الناس عن الدخول في الإسلام، ولذلك امتنع النبي صلى الله عليه وسلم من قتل المنافقين لئلا يقول الناس: إن محمدًا يقتل أصحابه.