Chanzo: HadeethEnc.com, Kiswahili v1.18.0
Matini ya Kiarabu
عَنْ عَبْدِ اللهِ بنِ مَسْعُودٍ رَضيَ اللهُ عنهُ قَالَ: نَامَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ عَلَى حَصِيرٍ، فَقَامَ وَقَدْ أَثَّرَ فِي جَنْبِهِ، فَقُلْنَا: يَا رَسُولَ اللهِ، لَوِ اتَّخَذْنَا لَكَ وِطَاءً، فَقَالَ: «مَا لِي وَلِلدُّنْيَا، مَا أَنَا فِي الدُّنْيَا إِلاَّ كَرَاكِبٍ اسْتَظَلَّ تَحْتَ شَجَرَةٍ ثُمَّ رَاحَ وَتَرَكَهَا».
Tafsiri
Kutoka kwa Abdallah bin Masudi radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Alilala Mtume rehema na amani ziwe juu yake katika mkeka, akasimama mkeka ukiwa umemuathiri katika ubavu wake, tukasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, lau tungelikuandalia godoro: Akasema: "Nina haja gani mimi na dunia, kwani mimi katika dunia hii ni kama msafiri aliyeshuka chini ya mti kisha akaondoka akauacha".
Ufafanuzi
Ameeleza Abdallah bin Masudi radhi za Allah ziwe juu yake ya kwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake alilala juu ya busati dogo lililoshonwa kutokana na baadhi ya mimea, akasimama ukiwa tayari mkeka umeathiri katika ngozi ya ubavu wake, tukasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, lau tungelikuandalia godoro laini basi ingelikuwa bora kuliko kujilaza kwako juu ya mkeka mgumu, akasema rehema na amani ziwe juu yake: Sina mapenzi wala hamu ya dunia mpaka niwe na tamaa nayo, kwani mfano wangu mimi na kubakia katika dunia ni kama msafiri aliyejikinga kivulini kwa muda mfupi kisha akaondoka akakiacha.
Mafunzo
- Kumebainishwa hali aliyokuwa nayo Mtume rehema na amani ziwe juu yake katika kuipa nyongo na kuipuuza dunia.
- Hadithi haijamaanisha kuacha mambo ya lazima katika dunia, bali imemaanisha kuishughulikia zaidi kuliko akhera, kwani mtu kakaa chini ya kivuli cha mti na akafaidika nacho kwa ajili ya kufika anakokwenda, na wala hakubweteka hapo.
- Kuchukua mazingatio kwa hali ya Mtume rehema na amani ziwe juu yake, kwani yeye ndiye kiigizo chema, na kwamba atakayeiga nyenendo zake ataongoka, na atafaulu katika dunia na akhera.
- Pupa ya Maswahaba radhi za Allah ziwe juu yao juu ya Mtume rehema na amani ziwe juu yake na mapenzi yao kwake.
- Sheria ya kupiga mifano katika ufikishaji ujumbe na ufundishaji.
Ufafanuzi: العربية
ذكر عبد الله بن مسعود رضي الله عنه أن النبي صلى الله عليه وسلم نام على بِساط صغير مَنْسُوْج من بعض النبات، فقام وقد أثّر الحصير في جلد جنبه، فقلنا: يا رسول الله، لو اتخذنا لك فراشًا ليّنًا لكان أحسن من اضطجاعك على هذا الحصير الخشن، فقال صلى الله عليه وسلم: ليس لي محبة وأُلْفة مع الدنيا حتى أرغب إليها، فما مثلي والبقاء في الدنيا إلا كراكب استظل تحت شجرة ثم راح وتركها.
- بيان ما كان عليه النبي صلى الله عليه وسلم من الزهد في الدنيا والإعراض عنها.
- ليس في الحديث ترك ما لا بد منه من الدنيا، وإنما الانشغال بها عن الآخرة، فإن الرجل استظل بالشجرة واستفاد منها من أجل وصوله، ولم يركن إليها.
- الاعتبار بحال النبي صلى الله عليه وسلم، فإنه الأسوة الحسنة، وأن من اقتفى آثاره اهتدى، وأفلح في الدنيا والآخرة.
- حرص الصحابة رضي الله عنهم على رسول الله صلى الله عليه وسلم ومحبتهم له.
- مشروعية ضرب الأمثال في الدعوة والتعليم.